Kusimama Kwa Ajili Ya Rak’ah Ya Tatu, Kisha Ya Nne
Kisha, alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم)akinyanyuka kwa ajili ya Rak’ah ya tatu pamoja na takbiyr([1]) na alimuamrisha "aliyeswali vibaya" kufanya hivyo: “….kisha akifanya hivyo katika kila Rak’ah na Sajdah kama ilivyotangulia”
Na alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم)anaposimama kutoka kikao alisema takbiyr, kisha akasimama"([2]) na "Alikuwa akinyanyua (صلى الله عليه وآله وسلم)mikono yake([3]) pamoja na takbiyr mara nyingine.
Na alikuwa anapotaka kusimama kwa ajili ya Rak’ah ya nne, akisema: ((Allaahu Akbar))"([4]) na alimuamrisha "aliyeswali vibaya" hivyo kama kabla na alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akinyanyua mikono yake([5]) pamoja na takbiyr mara nyingine.
Alikuwa akiketi barabara juu ya mguu wake wa kushoto, kwa utulivu hadi kila mfupa ulirudi sehemu yake kisha akisimama, akijisaidia kwa mikono yake, alikunja ngumi([6]) na kutegemea mikono yake katika kuinuka.([7])
Alikuwa akisoma Suratul-Faatihah kaitka Rak’ah zote mbili na alimuamrisha "aliyeswali vibaya" kufanya hivyo. Katika Swalah ya adhuhuri aliongeza mara nyingine Aayah chache kama ilivyoelezewa katika 'Kisomo cha Swalah ya Adhuhuri'.
[1]Al-Bukhaariy na Muslim.
[2]Abu Ya'alaa katika Musnad yake (284/2) ikiwa na isnaad nzuri. Imetolewa katika Silsilatul Al- Ahaadiyth As-Swahiyhah (604).
[3] Al-Bukhaariy na Muslim.
[4]Kifungu kile kile kilichotajwa hapo mbeleni.
[5]Abu 'Awaanah na An-Nasaaiy ikiwa na isnaad Swahiyh.
[6]Ina maana 'kama mtu anayekanda unga'.
[7] Al-Harbiy katika Hadiyth Al-Ghariyb. Maana yake inapatikana katika Al-Bukhaariy na Abu Daawuud. Ama kuhusu Hadiyth kuwa 'alimkataza mtu kujisaidia kwa mikono yake anapoinuka katika Swalah', ni Munkar na sio Swahiyh kama nilivyoelezea katika Silsilatul-Ahaadityh Adhwa'iyfah (967).
Post a Comment