Wajibu Wa Kumswalia Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم)
Alimsikia mtu (صلى الله عليه وآله وسلم) akiomba du’aa bila ya kumtukuza Allaahتعالى , wala kumswalia Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) hivyo akasema: ((Huyu mtu ameharakiza)). Kisha akamwita na kumwambia yeye na wengineo: ((Anaposwali mmojawenu, aanze kwa kumsifu Mola wake, (عزرجل) na kumtukuza kisha amswalie [katika usimulizi mmoja: amswalie] Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) kisha aombe anayotaka)).([1])
Pia, “alimsikia mtu akimtukuza na kumsifu Allaah na kumswalia Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Swalah, hivyo Mjumbe wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwambia: ((Omba na utaitikiwa, uliza utapewa))([2])
0 Comments