Sura 114 - SURA AN-NAS

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi Warehema, Mwenye Kurehemu.


114:1
قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ
Sema: Najikinga kwa Mola wa watu,
114:2
مَلِكِ النَّاسِ
Mfalme wa watu,
114:3
إِلَٰهِ النَّاسِ
Mungu wa watu,
114:4
مِنْ شَرِّ الْوَسْوَاسِ الْخَنَّاسِ
Na shari ya mwenye kutia wasiwasi mwenye kurejea nyuma,
114:5
الَّذِي يُوَسْوِسُ فِي صُدُورِ النَّاسِ
Anayetia wasiwasi katika vifua vya watu,
114:6
مِنَ الْجِنَّةِ وَالنَّاسِ
Kutokana na majini na watu.

0 Comments