August 4, 2015

082 - Al-Infitwaar

الإِنْفِطَار
Al-Infitwaar: 82

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِإِذَا السَّمَاءُ انفَطَرَتْ ﴿١﴾
1. Mbingu zitakapopasuka.

وَإِذَا الْكَوَاكِبُ انتَثَرَتْ ﴿٢﴾
2. Na sayari zitakapoanguka na kutawanyika.


وَإِذَا الْبِحَارُ فُجِّرَتْ ﴿٣﴾
3. Na bahari zitakapolipuka.


وَإِذَا الْقُبُورُ بُعْثِرَتْ ﴿٤﴾
4. Na makaburi yatakapopinduliwa chini juu na kufichuliwa.


عَلِمَتْ نَفْسٌ مَّا قَدَّمَتْ وَأَخَّرَتْ ﴿٥﴾
5. Nafsi itajua yale iliyoyakadimisha na iliyoyaakhirisha.


يَا أَيُّهَا الْإِنسَانُ مَا غَرَّكَ بِرَبِّكَ الْكَرِيمِ ﴿٦﴾
6. Ee mwana Aadam! Nini kilichokughuri kuhusu Rabb wako Mkarimu?


الَّذِي خَلَقَكَ فَسَوَّاكَ فَعَدَلَكَ ﴿٧﴾
7. Ambaye Amekuumba Akakusawazisha (umbo sura, viungo) na Akakupima na kukulinganisha sawa.


فِي أَيِّ صُورَةٍ مَّا شَاءَ رَكَّبَكَ ﴿٨﴾
8. Katika sura Aliyotaka Akakutengeneza.


كَلَّا بَلْ تُكَذِّبُونَ بِالدِّينِ ﴿٩﴾
9. Laa hasha! Bali mnakadhibisha malipo.


وَإِنَّ عَلَيْكُمْ لَحَافِظِينَ ﴿١٠﴾
10. Na hakika juu yenu bila shaka kuna wenye kuhifadhi (na kuchunga).  


كِرَامًا كَاتِبِينَ ﴿١١﴾
11. Watukufu wanaoandika (amali).


يَعْلَمُونَ مَا تَفْعَلُونَ ﴿١٢﴾
12. Wanajua yale myafanyayo.


إِنَّ الْأَبْرَارَ لَفِي نَعِيمٍ ﴿١٣﴾
13. Hakika Waumini watendao mema kwa wingi bila shaka watakuwa katika neema (taanasa, furaha n.k).


وَإِنَّ الْفُجَّارَ لَفِي جَحِيمٍ ﴿١٤﴾
14. Na hakika watendao dhambi bila shaka watakuwa katika moto uwakao vikali mno.


يَصْلَوْنَهَا يَوْمَ الدِّينِ ﴿١٥﴾
15. Watauingia waungue Siku ya malipo.


وَمَا هُمْ عَنْهَا بِغَائِبِينَ ﴿١٦﴾
16. Nao hawatokosa kuweko humo.


وَمَا أَدْرَاكَ مَا يَوْمُ الدِّينِ ﴿١٧﴾
17. Na nini kitakachokujulisha Siku ya malipo?


ثُمَّ مَا أَدْرَاكَ مَا يَوْمُ الدِّينِ ﴿١٨﴾
18. Kisha nini kitakachokujulisha Siku ya malipo?


يَوْمَ لَا تَمْلِكُ نَفْسٌ لِّنَفْسٍ شَيْئًاۖ وَالْأَمْرُ يَوْمَئِذٍ لِّلَّـهِ ﴿١٩﴾
19. Siku ambayo nafsi haitokuwa na uwezo wowote juu ya nafsi nyingine; na amri Siku hiyo ni ya Allaah Pekee.


Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only