090 - Al-Balad

 الْبَلَد
Al-Balad: 90بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ


لَا أُقْسِمُ بِهَـٰذَا الْبَلَدِ ﴿١﴾
1. Naapa kwa mji huu (wa Makkah).


وَأَنتَ حِلٌّ بِهَـٰذَا الْبَلَدِ ﴿٢﴾
2. Nawe (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) uko huru na vikwazo vya mji huu.


وَوَالِدٍ وَمَا وَلَدَ ﴿٣﴾
3. Na Naapa kwa mwenye kuzaa (Aadam) na aliowazaa (wana Aadam).


لَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنسَانَ فِي كَبَدٍ ﴿٤﴾
4. Kwa yakini Tumemuumba mwana Aadam katika tabu, mashaka ya kuendelea.


أَيَحْسَبُ أَن لَّن يَقْدِرَ عَلَيْهِ أَحَدٌ ﴿٥﴾
5. Je, anadhani kwamba hakuna yeyote atakayemweza?


يَقُولُ أَهْلَكْتُ مَالًا لُّبَدًا ﴿٦﴾
6. Anasema: “Nimeangamiza mali tele.”


أَيَحْسَبُ أَن لَّمْ يَرَهُ أَحَدٌ ﴿٧﴾
7. Anadhani kwamba hakuna yeyote anayemuona?


أَلَمْ نَجْعَل لَّهُ عَيْنَيْنِ ﴿٨﴾
8. Je, kwani Hatukumjaalia macho mawili?


وَلِسَانًا وَشَفَتَيْنِ ﴿٩﴾
9. Na ulimi na midomo miwili?


وَهَدَيْنَاهُ النَّجْدَيْنِ ﴿١٠﴾
10. Na Tukambainishia njia mbili (ya haki na upotofu)?


فَلَا اقْتَحَمَ الْعَقَبَةَ ﴿١١﴾
11. Basi hakujiingiza kwa juhudi njia ya tabu na mashaka. 


وَمَا أَدْرَاكَ مَا الْعَقَبَةُ ﴿١٢﴾
12. Na nini kitakachokujulisha nini hiyo njia ya tabu na mashaka.


فَكُّ رَقَبَةٍ ﴿١٣﴾
13. Ni kuacha huru mtumwa.


أَوْ إِطْعَامٌ فِي يَوْمٍ ذِي مَسْغَبَةٍ ﴿١٤﴾
14. Au kulisha katika siku ya ukame.


يَتِيمًا ذَا مَقْرَبَةٍ ﴿١٥﴾
15. Yatima aliyekuwa jamaa wa karibu.


أَوْ مِسْكِينًا ذَا مَتْرَبَةٍ ﴿١٦﴾
16. Au maskini aliye hohehahe.


ثُمَّ كَانَ مِنَ الَّذِينَ آمَنُوا وَتَوَاصَوْا بِالصَّبْرِ وَتَوَاصَوْا بِالْمَرْحَمَةِ ﴿١٧﴾
17. Kisha akawa miongoni mwa wale walioamini, na wakausiana kusubiri na wakausiana huruma.


أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ الْمَيْمَنَةِ ﴿١٨﴾
18. Hao ndio watu wa kuliani.


وَالَّذِينَ كَفَرُوا بِآيَاتِنَا هُمْ أَصْحَابُ الْمَشْأَمَةِ ﴿١٩﴾
19. Na wale waliokufuru Aayaat Zetu wao ndio watu wa kushotoni.


عَلَيْهِمْ نَارٌ مُّؤْصَدَةٌ ﴿٢٠﴾
20. Juu yao ni moto uliofungiwa kila upande.


0 Comments