Kababu Za Kuchoma Katika Vijiti

Vipimo
Nyama ya kusaga                                3 Lb
Kitunguu saumu (thomu/galic)              1 kijiko cha chakula        
Tangawizi                                            1 kijiko cha chakula
Chumvi                                               Kiasi
Kotmiri                                                1 msongo
Bizari ya kababu                                  ½ pakiti ya 100g
(Shan Chapplin Kabaab mix)
                                              
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika  
 
1.       Saga nyama pamoja na kotmiri mara mbili iwe laini kuliko ya  sambusa.
2.       Tia kwenye bakuli na changanya na vitu vyote pamoja.
3.       Viringisha kwenye vijiti vya kuchomea na acha kama muda wa saa.
4.       Choma (bake) katika oven kwa moto wa 350◦c  mpaka zigeuke rangi na kuiva.
5.       Zikishaiva ziweke kwenye sahani tayari kwa kuliwa na saladi, chips, mikate au wali.   
  
Kidokezo:
 
1.       Ni bora kuviroweka vijiti vya kuchomea na maji usiku nzima ili ukichoma  kababu vijiti visiungue.
2.       Tumia bizari zako mwenyewe upendazo ikiwa huna hiyo ya Shan Chapplin Kabaab Mix.

0 Comments