Kisa Cha Nabii Swaaalih عليه السلام Sehemu ya 1

DA'AWA NA WATU WA THAMUUD

Nabii Swaalih عليه السلام alikuwa ni Mtume katika kabila maarufu   ambalo jina lake linatokana na jina la Babu yao Thamuud ambaye ni katika ukoo wa Nabii Nuuh عليه السلام .  Kwa hivyo jina lake ni Swaalih ibn 'Ubayd ibn Maasih ibn 'Ubayd ibn Haajir ibn Thamuud, ibn 'Aabir ibn Iram, ibn Saam, ibn Nuuh.
Naye Swaalih na watu wake wa Thamuud  ni waarabu waliokuwa wakiishi Hijr ambayo iko baina ya Hijaaz na Tabuuk  (Kaskazini magharibi ya Madiynah)   ambako siku moja Mtume صلى الله عليه وآله وسلم  alipita wakati wanaelekea kwenda kwenya vita  vya Tabuuk  kama tutakavyoelezea mwisho wa kisa hiki.  
Hiki ndio kisa chake Nabii Swaalih عليه السلم    na watu wake kama tulivyoelezewa katika aya mbali mbali za Qur'aan
Watu wa Thamuud walikuwa ni watu baada ya Nabii Huud عليه السلام ambao walikuwa wakiabudu masanamu na baada ya kuletewa  Nabii Huud    عليه السلاna kumkanusha Allaah سبحانه وتعالى   Aliwaangamiza. Na baada ya miaka, watu wa Thamuud wakaibuka na kuwa na nguvu na ufahari. Nao pia waliabudu masanamu, kwa hivyo Allaah سبحانه وتعالى  Akawatumia mjumbe miongoni mwao naye ni Nabii Swaalih عليه السلام  ambaye naye kama kawaida ya Mitume alikuja na wito uleule wa kuwaita watu katika Tawhiiyd ya Allaah سبحانه وتعالى yaani kumuabudu Yeye pekee bila ya kumshirikisha na kitu, na kuwanasihi waache ibada ya masanamu na pia kuwataka watubu kwa Mola wao kwa kufuru wanayoifanya.  
}}وَإِلَى ثَمُودَ أَخَاهُمْ صَالِحًا قَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُواْ اللّهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَهٍ غَيْرُهُ هُوَ أَنشَأَكُم مِّنَ الأَرْضِ وَاسْتَعْمَرَكُمْ فِيهَا فَاسْتَغْفِرُوهُ ثُمَّ تُوبُواْ إِلَيْهِ إِنَّ رَبِّي قَرِيبٌ مُّجِيبٌ {{ 
 {{Na kina Thamud tuliwapelekea ndugu yao Swaalih. Akasema: Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna Mungu ila Yeye. Yeye ndiye aliyekuumbeni katika ardhi, na akakuwekeni humo. Basi mwombeni msamaha, kisha mtubu kwake. Hakika Mola wangu Mlezi yupo karibu, anaitikia maombi}} Huud: 61
Kwa maana kwamba: Amekujaalieni kuwa makhalifa baada ya watu wengine (kina 'Aad na wa nyuma yao)  ili mfikiri na mtambue ubaya wao waliotenda, na nyinyi msiwe kama wao, na Akakujaalieni katika hii ardhi na kukuneemesheni  neema mbali mbali kama za mashamba na matunda na majumba ya fahari mkastarehe, basi Yeye Pekee ndiye anayestahiki kuabudiwa bila ya kumshirikisha,  vile vile mkabilini Mola wenu kwa kumshukuru na kufanya amali njema wala msjije kumkhalifu amri Zake  na kutoka nje ya mipaka kwa kutokumtii, basi rudini kwake kwa kutubia na Yeye Allaah سبحانه وتعالى       yuko tayari kupokea tawbah zenu.      
Aya ifuatayo inaeleza zaidi neema hizo walizojaaliwa na pia kuonesha ukumbusho wa Swaalih عليه السلام  kwa hao watu wa Thamuud kwa kuwaita kwao kwenye dini ya haki.
}}وَإِلَى ثَمُودَ أَخَاهُمْ صَالِحًا قَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُواْ اللّهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَهٍ غَيْرُهُ قَدْ جَاءتْكُم بَيِّنَةٌ مِّن رَّبِّكُمْ هَذِهِ نَاقَةُ اللّهِ لَكُمْ آيَةً فَذَرُوهَا تَأْكُلْ فِي أَرْضِ اللّهِ وَلاَ تَمَسُّوهَا بِسُوَءٍ فَيَأْخُذَكُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ{{
{{Na kwa Thamuud tulimpeleka ndugu yao, Swaalih. Akasema: Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna Mungu ila Yeye. Hakika imekwisha kukufikieni Ishara iliyo wazi kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Huyu ni ngamia jike wa Mwenyezi Mungu aliye ni Ishara kwenu. Basi mwachieni ale kwenye ardhi ya Mwenyezi Mungu, wala msimdhuru, isije kukushukieni adhabu chungu}}     Al-A'araaf: 73
}}وَاذْكُرُواْ إِذْ جَعَلَكُمْ خُلَفَاء مِن بَعْدِ عَادٍ وَبَوَّأَكُمْ فِي الأَرْضِ تَتَّخِذُونَ مِن سُهُولِهَا قُصُورًا وَتَنْحِتُونَ الْجِبَالَ بُيُوتًا فَاذْكُرُواْ آلاء اللّهِ وَلاَ تَعْثَوْا فِي الأَرْضِ مُفْسِدِينَ{{
{{Na kumbukeni alivyokufanyeni wa kushika pahala pa 'Aadi na akakuwekeni vizuri katika nchi, mnajenga majumba ya fakhari katika nyanda zake, na mnachonga majumba katika milima. Basi zikumbukeni neema za Mwenyezi Mungu wala msitende uovu katika nchi kwa ufisadi}} Al-A'araaf: 74
  Kama zilivyo umma zilizopita zilipojiwa na Mitume, wakaamini wachache miongoni mwao na wengi wakamkanusha.
}}وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا إِلَى ثَمُودَ أَخَاهُمْ صَالِحًا أَنِ اعْبُدُوا اللَّهَ فَإِذَا هُمْ فَرِيقَانِ يَخْتَصِمُونَ{{ 
 {{Na kwa kina Thamuud tulimtuma ndugu yao Swaalih kuwaambia: Muabuduni Mwenyezi Mungu. Basi wakawa makundi mawili yanayogombana}} An-Naml :45
Waliomkanusha walimhutumu kuwa anawaletea shari, na kwamba labda akili yake haiko sawa kwani hawakumtegemea yeye Swaalih عليه السلام  ambaye kwao alikuwa ni mtu mwema kabisa, aje kuwakataza kuacha waliyokuja nayo mababu zao na kutaka wamfuate hayo anayotaka yeye Swaalih عليه السلام?  Wakamwambia; 
}} قَالُواْ يَا صَالِحُ قَدْ كُنتَ فِينَا مَرْجُوًّا قَبْلَ هَذَا أَتَنْهَانَا أَن نَّعْبُدَ مَا يَعْبُدُ آبَاؤُنَا وَإِنَّنَا لَفِي شَكٍّ مِّمَّا تَدْعُونَا إِلَيْهِ مُرِيبٍ{{ 
{{ Wakasema: Ewe Swaalih! Hakika kabla ya haya ulikuwa unatarajiwa kheri kwetu. Je, unatukataza tusiwaabudu waliyokuwa wakiwaabudu baba zetu? Na hakika sisi tuna shaka na wasiwasi kwa hayo unayotuitia}} Huud: 62
Walikuwa na shaka kubwa juu ya yale Swaalih aliyowalingania nayo na kuyaona ni mapya! Swaalih عليه السلام akawajibu:
}}قَالَ يَا قَوْمِ أَرَأَيْتُمْ إِن كُنتُ عَلَى بَيِّنَةً مِّن رَّبِّي وَآتَانِي مِنْهُ رَحْمَةً فَمَن يَنصُرُنِي مِنَ اللّهِ إِنْ عَصَيْتُهُ فَمَا تَزِيدُونَنِي غَيْرَ تَخْسِيرٍ{{ 
 {{Akasema: Enyi watu wangu! Mwaonaje ikiwa ninazo dalili zilizo wazi kutokana na Mola wangu Mlezi, naye akawa kanipa rehema kutoka kwake - je, ni nani atakaye ninusuru kwa Mwenyezi Mungu nikimuasi? Basi nyinyi hamtanizidishia ila khasara tu}} Huud:63
}}قَالَ يَا قَوْمِ أَرَأَيْتُمْ إِن كُنتُ عَلَى بَيِّنَةً مِّن رَّبِّي{{
{{Akasema: Enyi watu wangu! Mwaonaje ikiwa ninazo dalili zilizo wazi kutokana na Mola wangu Mlezi}}    
Dalili za dhahiri zenye uhakika kabisa kwa yale anayowaitia kumuabudu kwamba Yeye ndiye Mola wa Viumbe wote na Mola wa mbingu na Ardhi na mwenye kupasa kuabudiwa kwa haki. 
}}وَآتَانِي مِنْهُ رَحْمَةً{{
{{naye akawa kanipa rehema kutoka kwake}}
Rahma kutoka kwa Allaah سبحانه وتعالى kumchagua yeye na kumpa uongofu na kumfanya Mjumbe Wake  Allaah   سبحانه وتعالى Aliyemtuma kwao kuwatoa katika upotofu. 
}}فَمَن يَنصُرُنِي مِنَ اللّهِ إِنْ عَصَيْتُهُ فَمَا تَزِيدُونَنِي غَيْرَ تَخْسِيرٍ{{
  {{je, ni nani atakaye ninusuru kwa Mwenyezi Mungu nikimuasi?}}
Nikiacha kukuiteni katika hakki ya kumuabudu Allaah سبحانه وتعالى   Pekee basi nyinyi hamtoweza kunifaa wala kuninusuru na adhabu yake Allaah سبحانه وتعالى atakaponiadhibu,  bali itakuwa ni hasara tu na kuangamia kwangu. 
Vile vile wakamwambia:
}}قَالُوا إِنَّمَا أَنتَ مِنَ الْمُسَحَّرِينَ{{
{{Wakasema: Hakika wewe ni miongoni mwa waliorogwa}}
Ashura:  153
Mujaahid kasema;  Wamemaanisha kuwa kaathirika na uchawi.
Wafasiri wengi wamefasiri kwamba ina maana;  Hujui unachokisema kutuita katika ibada ya mungu mmoja na  kuacha miungu mingine!
Hiyo ndio ilikuwa kawaida ya watu wa umma za nyuma, walipojiwa na Mitume yakawa majibu yao ni kuwaambia hao Mitume kuwa ni wachawi! kama alivyoambiwa vile vile Mtume  صلى الله عليه وآله وسلم  na makafiri wa ki-Quraysh.  Vile vile ni kawaida yao nyingine kuwadharau hao Wajumbe wa Allaah سبحانه وتعالى   kwa vile wao ni binaadamu tu kama wao. Na wakisema:
}}مَا أَنتَ إِلَّا بَشَرٌ مِّثْلُنَا{{
{{Wewe si chochote ila ni mtu kama sisi}} Ashura: 154
}}كَذَّبَتْ ثَمُودُ بِالنُّذُرِ{{
}} فَقَالُوا أَبَشَرًا مِّنَّا وَاحِدًا نَّتَّبِعُهُ إِنَّا إِذًا لَّفِي ضَلَالٍ وَسُعُرٍ{{
   }}أَؤُلْقِيَ الذِّكْرُ عَلَيْهِ مِن بَيْنِنَا بَلْ هُوَ كَذَّابٌ أَشِرٌ{{
 }} سَيَعْلَمُونَ غَدًا مَّنِ الْكَذَّابُ الْأَشِرُ{{
23. Thamudi waliwakanusha Waonyaji
24. Wakasema: Ati tumfuate binaadamu mmoja katika sisi? Basi hivyo sisi tutakuwa katika upotofu na kichaa!
25. Ni yeye tu aliyeteremshiwa huo ukumbusho kati yetu sote? Bali huyu ni mwongo mwenye kiburi!
26. Kesho watajua ni nani huyo mwongo mwenye kiburi.
Al-Qamar :  23-26
Kama kweli yeye ni Mtume basi wametaka miujiza ndio waweze kumuamini.
}}مَا أَنتَ إِلَّا بَشَرٌ مِّثْلُنَا فَأْتِ بِآيَةٍ إِن كُنتَ مِنَ الصَّادِقِينَ{{
{{Wewe si chochote ila ni mtu kama sisi. Basi lete Ishara ukiwa wewe ni miongoni mwa wasemao kweli}}
Ashu'araa: 154
Nabii Swalih عليه السلام  akajitenda nao kwani alikwishakata tamaa nao:
}}فَتَوَلَّى عَنْهُمْ وَقَالَ يَا قَوْمِ لَقَدْ أَبْلَغْتُكُمْ رِسَالَةَ رَبِّي وَنَصَحْتُ لَكُمْ وَلَكِن لاَّ تُحِبُّونَ النَّاصِحِين{{
{{Basi Swaalih akwaacha na akasema: Enyi watu wangu! Nilikufikishieni Ujumbe wa Mola wangu Mlezi, na nikakunasihini, lakini nyinyi hamwapendi wenye kunasihi}} Al-A'araaf:  79

Ishara au Miujiza waliyotaka kutoka kwa Nabii Swaalih عليه السلام   ni ngamia kama tutakavyoona:
                                                                                         
                                                                      
                                              Kisa kinaendelea ...../2

0 Comments