SWALI:
Je,
inafaa mtoto wa kike kumfanyia Hajj na kumtolea sadaqah mama
yake aliyefariki ambaye hakuwa akiswali katika uhai wake? Nini
hukmu ya jambo hili ikiwa mtoto anataka kutimiza wajibu wake (wa
kufawanyia wema wazazi) kama alivyopata mafunzo katika
dini yetu ya Kiislam?
JIBU:
Yeyote
anayeacha Swalah makusudi kwa sababu hadhani kuwa ni
fardhi kwake, atakuwa amekufuru kutokana na rai waliyokubaliana
Maulamaa. Na yeyote anayeacha kuswali kwa sababu ya uvivu au
kudharau, basi naye pia atakuwa amekufuru kutokana na wengi wa
Maulamaa na rai mbili za Maulamaa. Hii ni kwa sababu Mtume
(Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
(( إن العهد الذي بيننا و بينهم الصلاة فمن تركها فقد كفر )) أخرجه أصحاب السنن
((Mafungamano baina yetu na wao (Makafiri) ni Swalah, atakayeiacha amekufuru)) [Abu Dawwuud, At-Tirmidhy, An-Nasaaiy na Ibnu Maajah]
Juu ya hivyo, dalili nyingine kutoka katika Qur-aan na Sunnah zimethibiti hukmu hiyo.
Kwa hiyo, haipasi kumfanyia Hajj au kumtolea sadaqah mtu
mwingine aliyekufa ambae hakuwa akiswali, kama ilivyokuwa haifai
kumfanyia Hajj au kutoa sadaqah kwa ajili ya Kafiri.
Na kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) ndio yako mafanikio
yote na Rahma na Amani zimfikie Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa
aalihi wa sallam) na Swahaba zake.
Halmashauri ya kudumu ya Utafiti Wa Kiislaam Imejumuisha:
Kiongozi Mkuu: Shaykh 'Abdul 'Aziyz ibn 'Abdullaah ibn Baaz
Msaidizi Kiongozi Mkuu: Shaykh ‘Abdur-Razzaaq 'Afiyfiy
Mjumbe: Shaykh 'Abdullaah Ibn Ghudayyaan
Mjumbe: Shaykh 'Abdullaah ibn Qu'uud
Fataawa
Al-Lajnatud-Daaimah lil-buhuuthil-'Ilmiyyah wal-Iftaa Mjalada
11, Uk. 113, Swali Namba 2 ya Fatwa Namba 6178
Post a Comment