Mkate Wa Mayai

Vipimo

Mayai                                           4
Sukari                                          ¼  Kikombe
Unga wa Ngano                            Vijiko 5 ½ vya chakula
Hiliki ya kusaga                            ½  kijiko cha chai
Baking powder                             ½  Kijiko cha chai
Zabibu kavu                                ¼  kikombe
 
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Chukua bakuli la kiasi, weka sukari, hiliki na vunja juu yake mayai  yote manne.
  2. Changanya sukari,  hiliki na mayai   kwa kutumia mashine ya kukorogea keki (cake mixer), mpaka sukari ivurugike yote na kuumuka.
  3. Washa jiko lako (oven) 350F lianze kupata moto.
  4. Weka baking powder kwenye unga na uanze kuuchanganya kidogo kidogo kwenye mchanganyiko  wa mayai na sukari. Hakikisha kila ukiweka unga kidogo unauchanganya vyema usiwe na madonge.
  5. Mimina unga  ndani ya sufuria ya kuchomea keki ya kiasi.
  6. Tupia zabibu  juu ya mchanganyiko wako.
  7. Ingiza sufuria   ndani ya jiko (oven) kwa dakika 20 kisha utoe.
  8. Uhakikishe mkate wako kama umeiva kwa kijiti cha kuchomea mshikaki au toothpick. Ingiza kijiti  katikati ya mkate kisha kitoe na ukiguse uangalie kama kikavu mkate umeiva kama bado kuna ubichi basi rudisha mkate kwa dakika 5 nyingine kisha ukague.
  9. Wacha mkate upoe kisha utoe ndani ya sufuria na uweke kwenye sahani tayari kwa kuliwa.

0 Comments