KUWEKA MKONO WAKO JUU YA KICHWA CHA MKEO NA KUMUOMBEA

Inampasa mume , wakati wa kufunga ndoa na mkewe kabla ya kumuingilia kuweka mkono wake juu ya kichwa chake (sehemu ya utosi) na kutaja jina la Allaah na kuomba baraka za Allaah kama katika kauli ya mtume
" Anapofunga ndoa mmoja wenu na mwanamke au anapomuajiri mfanyakazi basi amuekee mkono katika kipaji cha uso wake ataje jina la Allaah utosini mwake na kusema
"Ewe Allaah hakika mimi nakuomba kheri ya (mke) huyu na kheri uliyomumbiya na najilinda kwako na shari yake, na shari uliyomuumbiya na anaponunua ngamia (kipando) na aseme hivyo hivyo" { Al-Bukhary katika " af'aalul-'ibaad, Abuu Daawuud)

0 Comments