SIASA KALI NI NINI?

Siasa kali maana yake nini?
Kwa mujibu wa wanafilosofia husema kwamba neno
siasa kali “extremist” kwa kifupi humaanisha kuwa
ni mtu anayeamini kitu Fulani kupita kiasi.
Yawezekana ikawa ni itikadi, dini, ama mfumo wa
maisha. Mtu mwenye siasa kali huishi maisha yake
akiitangaza fikra hiyo anayoiamini na yupo huwa
yupo tayari kwa lolote lile litakalomkuta katika
harakati za kuisambaza fikra ama itikadi hiyo.
Mafungu ya siasa kali hayana kipimo maalumu cha
mgawanyiko wake ila kwa kawaida katika
muktadha wa mfumo wa kibepari kuna siasa kali wa
kidini za kiilmaniya( zinazotofautisha kati ya dini na
siasa), siasa kali wanaotetea utaifa( nationalists) na
kundi la tatu liliozuka baada ya kuangushwa kwa
mfumo wa kikomunisti ulimwenguni ni kundi la
waislamu wa siasa kali. Makundi hayo 2 ya mwanzo
huwa kwa kawaida hayazungumziwi sana kwenye
vyombo vya habari na hata yakizungumziwa huwa
hayapewi muda mwingi na mda mwingine
hutafutwa hata maneno mepesi ili kuyapaka mafuta
mazuri.
Swali la kujiuliza katik makundi ya mwanzo
hupakwa mafuta ila makundi yanayotiwa makundi
ya kiislamu siasa kali huwa yanapakwa matope na
vyombo vy habari. Jibu lake ni rahisi ni kwamba
makundin hayo mawili ya mwanzo hayana sifa ya
kuweza kuleta mageuzi ya kimfumo ila makundi ya
kiislamu siasa kali yanayo kwa kuwa itikadi
waliyoibeba ya uislamu ni nidhamu kamili ambayo
ina mgongano wa kifikra na mfumo wa kibepari.
Vyombo vya habari hutumika kama mbinu kuu ya
mapambano kati ya mfumo wa kibepari na uislamu.
Propaganda nzito hutumika dhidi ya makundi
yanayopambana kuleta mabadiliko katika ummah.
Hata hivyo vyombo vya habari vinavyoitwa vya
kiislamu navyo hubeba mtazamo wa kisekula na
vimekuwa ni msumari kwa ummah wa waislamu
kwa kuwa waislamu wamekua wanavitegemea
kuwakomboa toka kwenye giza na kuwapeleka
kwenye nuru lakini kinyume chake ndio vinawatoa
kwenye nuru na kuwarudisha kwenye giza kwani
navyo vimekuwa ima vinazishambulia harakati
ambazo zenye lengo la kuusimamisha uislamu kwa
kuziita “magaidi”
Uislamu ni mfumo kamili na una siasa yake. Siasa ya
uislamu na sio kama siasa ya kidemokrasia ambayo
ni siasa fisidifu na ambayo hutumia njia za ulaghai ili
kufikia lengo ambalo msukumo wake huwa ni
maslahi. Tukichukulia mtazamo wa kuwa siasa kali ni
mtu ambaye anaiamini fikra ama itikadi Fulani
kidhani na yupo tayari kuisambaza bila ya kuangalia
madhara yanayowez kumkuta, basi muislamu siasa
kali ni muislamu safi ambaye mwenye lengo sahihi la
kusimamisha uislamu kama mfumo wa kuwatawala
ulimwengu na hayupo tayari kuchanganya haki na
batili. Waislamu wengi hushindwa kuelewa kipimo
cha uislamu poa kimeasisiwa na makafiri
wamagharibi kupitia vyuo walivyoanzisha katika miji
ya waislamu. Lengo la kuleta kipimo hico ni kuzidi
kuwatoa waislamu kwenye aqeedah ya kiislamu na
kuwafanya kuwa ni masekula na wanademokrasia.
Hutumia na baadhi ya wanazuoni ambao
wanaosambaza fikra ya kidemokrasia kuwa ni
waislamu mfano wa kuigwa na waislamu ambao
wenye kutaka uislamu utawale kuwa ni waislamu
siasa kali.
Kutangaza baadhi ya makundi ya kiislamu kama ni
ya siasa kali ni mbinu ya wamagharibi katika
kuwagawa waislamu ili waweze kuwatawala na
kusiwe na ana yoyote ya upinzani dhidi ya ukoloni
wao katika ardhi za waislamu. Pindi wanapofanya
hivyo huugawa ummah wa kiislamu na kutokana na
baadhi yao kutojua lengo nyuma ya wamagharibi
hujikuta wanaelemea upande wa wale wanaoitwa
waislamu poa ambao kiasili ni waislamu ambao
wanakubaliana na demokrasia na hawana tabu
nayo.
Njia iliyopo kukabiliana na tatizo hili si kukata tama
ama kuingia kwenye siasa za kidemokrasia ili kupata
unafuu kwani tumeona hakuna unafuu ndani ya
siasa hizi na mfano mzuri ni ndugu zetu muslim
brotherhood wa misri walioingia kwenye siasa za
kidemokrasia kwani hawajapata unafuu na ndio
wanazidi kuuliwa bila ya hatia yoyote. Suluhisho
pekee ni kujiunga ama kuasisi vyama vya kisiasa
ambavyo vitatabanni njia ya kisheria ambayo
aliyopiya mtume Muhammad(saw) na kuulingania
uislamu kama mfumo wa kisiasa na huku
wakiukosoa ubepari bila ya kuangalia maslahi ama
madhara ambayo yatawakuta

0 Comments