Vipimo Vya Ugali:
Unga wa mahindi/sembe 4
Maji 6 takriban
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Chota unga kidogo katika kibakuli uchanganye na maji kidogo .
- Weka maji mengineyo katika sufuria kwenye moto.
- Changanya na mchanganyiko mdogo ufanya kama uji.
- Kisha kidogo kidogo unaongeza sembe huku unakoroga na kuusonga ugali hadi uive.
Vipimo Vya Mchuzi Wa Samaki Wa Nazi
Samaki nguru 5 vipande
Pilipili mbichi ilosagwa
Kitunguu maji kilosagwa 1 kimoja
Nyanya ilosagwa 2
Haldi/tumeric/bizari ya manjano ¼ kijiko cha chai
Chumvi kiasi
Ndimu 2 kamua
Tui la nazi zito 2 vikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Baada ya kumuosha samaki, weka katika sufuria.
- Tia chumvi, ndimu, pilipili mbichi ilosagwa.
- Tia vitunguu na nyanya zilosagwa
- Mkaushe kwa hivyo viungo, akianza kukauka tia tui la nazi.
- Acha kidogo tu katika moto tui liwive mchuzi ukiwa tayari.
Vipimo Vya Bamia
Bamia ½ kilo takriban
Nyanya kopo 1 kijiko cha chai
Methi/uwatu/fenugreek seeds ilosagwa 1 kijiko cha chai
Dania/corriander ilosagwa ½ kijiko cha chai
Chumvi kiasi
Mafuta 1 kikombe cha kahawa
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Katakata bamia kwa urefu.
- Weka mafuta katika karai, kisha tia bizari zote na nyanya kopo, kaanga kidogo.
- Tia bamia endelea kukaanga, kisha acha katika moto mdogomdogo ufunike.
Post a Comment