UYOGA WA SOSI YA JIBINI


VIPIMO

Uyoga                                       12 au zaidi
Siagi                                                2 Vijiko vya supu

Kitunguu kilichokatwakatwa                       1

Nyanya iliyosagwa                                3 vijiko vya supu

kitunguu swaumu kilichosagwa              1 kijiko cha chai

Pilipili manga ya unga                             ½ kijiko cha chai
Oregano                                                                1 kijiko cha chai

Parsely kavu iliyosagwa                                          1 kijiko cha chai

Nanaa kavu iliyosagwa                                           1 kijiko cha chai

Mafuta                                                                   2 vijiko vya supu

Chumvi                                                                  kiasi

Jibini (cheese) ya mazorella*                                  250 gm


Namna Ya Kutayarisha Na Kupika  1. Osha uyoga vizuri, kisha weka siagi katika sufuria ishike moto. Tia uyoga ukaange kaange kidogo ili ulainike uyoga.

  1. Katika kisufuria kidogo, weka mafuta, kaanga kitunguu hadi vigeuke rangi.

  1. Tia thomu, kaanga zaidi kidogo, kisha tia nyanya na bizari zote kaanga tena kidogo.

  1. Panga uyoga katika treya ya kupikia katika oveni, kisha mwagia sosi juu yake.

  1. Kuna jibini ya mazorela umwagie juu yake pia.

  1. Pika (Bake) katika oveni moto wa kiasi hadi uyoga upikike zaidi na jibini iyayuke. Epua ukiwa tayari.


Kidokezo :

Ikiwa idadi ya uyoga ni kidogo, basi sosi itakayobakia unaweza kutumia katika Pizza au pasta.

* unaweza kutumia aina nyengine ya jibini   

0 Comments