Vipimo
Vipapatio (Chicken wings) 2LB
Chumvi kiasi
Pilipilimanga 1 kijiko cha chai
Vitu vya Sosi
Kitunguu saumu/thomu iliyosagwa 2 vijiko vya supu
Pilipili mbichi iliyosagwa 1 kijiko cha chai
Chumvi kiasi
Paprika 1 kijiko cha chai
HP sauce (ikiwa utapenda) 2 vijiko vya supu
Ukwaju 3 vijiko vya supu
Asali 2 vijiko vya supu
Nyanya kopo 1 kijiko cha chai
Tomato Ketchup 2 vijiko vya supu
Pilipili nyekundu ya unga 1 kijiko cha chai
Mafuta 2 vijiko vya supu
Mafuta ya kukaangia vipapatio kiasi katika karai
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
1. Osha vizuri vipapatio kwa maji ya moto, chumvi na haldi (bizari ya manjano kukata harufu ya kuku.
2. Tia vipapatio chumvi na pilipili kisha ukaange katika mafuta mengi (deep fry) wakiiva na kubadilika rangi ya hudhurungi (golden brown) toa na uchuje mafuta.
3. Katika karai nyingine, tia mafuta vijiko 2 vya supu, kisha anza kukaanga thomu iliyosagwa kwa muda mdogo tu igeuke rangi kidogo.
4. Tia vitu vyote vingine vya sosi uendelee kukaanga kidogo tu. Ikiwa sosi nzito ongeza ukwaju.
5. Zima moto, changanya vipapatio vizuri na sosi, pakuwa katika sahani vikiwa tayari kuliwa.
0 Comments