Hizi ndio Hekma za Mtume swalallah aleyh wasalaam kukataza ufugaji wa mbwa


Siku baada ya siku,chunguzi za kielimu zathibitisha ukweli wa mtume Muhamadi-rehema na amani za Allah zimshukie-.
Daima katika mafundisho ya mtume Muhamadi-rehema na amani zimshukie-kumekuwa na faida,kinga juu yetu na hifadhi dhidi ya madhara mbali mbali.
Kwani yeye ni mwenye huruma juu yetu.

Kama alivyo tueleza Allah ndani ya kitabu chake kitukukfu cha Qur ani:
(لَقَدْ جَاءَكُمْ رَسُولٌ مِّنْ أَنفُسِكُمْ عَزِيزٌ عَلَيْهِ مَا عَنِتُّمْ حَرِيصٌ عَلَيْكُم بِالْمُؤْمِنِينَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ)
(Hakika amekwisha kujieni Mtume kutokana na nyinyi wenyewe; yanamhuzunisha yanayo kutaabisheni; anakuhangaikieni sana. Kwa Waumini ni mpole na mwenye huruma)
Qur ani 9:128
Kwani anatutakia afya bora na kheri.
Kutokana na hivyo akatukataza kufuga mbwa-isipokuwa kutokana na hali maalumu zilizo elezwa katika sheria ya kiislamu-,
mtume hakuishia kukataza kufuga tu,bali akawazingatia mbwa kuwa ni viumbe najisi.
Wataalamu hivi sasa wametambua mambo mengi kuhushu mbwa,na hili hapa ndilo lililofikiwa hivi karibuni,
Katika uchunguzi wa hivi karibuni uliofanywa na wataalamu kutoka University of Munich,wamegundua ya kuwa ufugaji wa mbwa wazidisha asilimia za kupatwa na saratani ya matiti.
Uchunguzi huo umeonesha ya kuwa asilimia 80 ya wanawake waliopatwa na saratani ya matiti,nyumbani kwao kulikuwa kukifugwa mbwa.Na hii ni kutokana na kufanana kukubwa kuliopo baina ya saratani ya matiti kwa mbwa na kwa binadamu.Uchunguzi huo ukionesha ya kuwa watu ambao walikuwa wakifuga paka hawajapatwa na saratani ya aina hii.
Katika uchunguzi huo wakatambua baadhi ya virusi ambavyo vimekuwa vikimpata binadamu na mbwa,na virusi vimekuwa na uwezo wa kutoka kwa mbwa na kuelekea kwa binadamu.Aina hii ya virusi imekuwa na nafasi kubwa katika kusababisha saratani hii ya titi.
Si hili tu bali kuna chunguzi zinazo onesha ya kuwa udenda wa mbwa,damu yake na manyoya yake ni hifadhi ya vimelea vya maradhi na virusi mbali mbali.

0 Comments