NAMNA YA KUTUMIA TUNDA LA TUFAHA (APPLE ) KATIKA KUPUNGUZA KITAMBI/UZITO MKUBWA NA KUBORESHA KINGA YA MWILI WAKO

Basi leo nimesukumwa kukupa elimu kuhusu tunda hili ambalo ni kati ya matunda yenye bei sana hapa Tanzania baada ya matunda kama strawberries na cranberries na ni tunda linalopendwa sana na wadada zetu basi napenda leo ujifunze vitu vifuatavyo kuhusu tunda hili.
1. Tunda hili ni miongoni mwa matunda yenye vitamin nyingi sana na viondoa sumu mwilini (ant oxidants) na mbali zaidi apple ni miongoni mwa tunda tunaloshauriwa kula na maganda yake kwani viondoa sumu hivi na vitamini vingi vinapatikana na ganda la tunda hili la apple.
Unapotaka kuwa mlaji mzuri wa tunda hili hakikisha unachagua tunda ambalo una uhakika limelimwa kienyeji kabisa kwani tunda hili ni miongoni mwa matunda yanayoongoza duniani kwa kumwagiwa dawa za viua watududu na kemikali mbali mbali. Na kumbuka dawa nyingi za viua wadudu ni LIPOPHILIC (Ni marafiki na mafuta yapatikanayo kwenye tunda) hivyo basi dawa za wadudu huwa zinapenya ganda la matunda haya na kuingia ndani haraka sana hivyo unakiwa kuwa makini na kuhakikisha tunda lako ni asili kabisa (organic).
CHAGUA APPLE YENYE SIFA HIZI.
• Haina kabisa kemikali
• Apple yenye mng'ao mzuri asili sio yenye rangi iliyofifia(Dull color)
• Chakua apple ambayo haina michubuko yoyote,shimo na ngumu (firm)
Nina imani utafurahia utafurahia ulaji wa tunda hili kwani ni tunda ambalo limeonesha kukulinda dhidi ya maradhi mbali mbali nitakayo kwenda kuelezea.
2. Tunda la apple ni miongoni mwa matunda ambayo yana nyuzi (fiber) nyingi sana ndani yake.
Basi kwa sababu hio napenda nikwambie kuwa aina ya fiber ipatikanayo katika tunda hili ni adimu sana na huwezi kuipata katika tunda lolote lile aina hii huitwa PECTIN fibers.
KAZI YA FIBERS(NYUZI) KATIKA MIILI YETU
• Inafanya shughuri za umeng'enyaji chakula kufanyika katika kiwango kinachostahili.
Unapokula fibers kwa wingi zinakusaidia mfumo wa umeng'enyaji chakula kufanyika polepole na hivyo hii hali itakufanya ukae muda mrefu ukiwa huna njaa kabisa tumbo limejaa.
Hivyo kwa wale wanaopenda kupunguza uzito, na wale ambao ni sugar addicted (walevi wa vyakula na vinywaji vya sukari) basi tunda hili linaweza kukata kabisa tatizo hilo na kufurahia. Watu wengi wanaotumia tunda hili sambamba na mlo wao huwasaidia sana kupunguza ulaji sana na kuwafanya muda wote wameshiba na kuwasaidia kupunguza uzito kiasi na kumaintain miili yao.
2. Vyakula vya fibers (nyuzi) husaidia kuondoa sumu mbali mbali za vyakula kwenye kuta za utumbo wa chakula na kukuzuia kupata magonjwa kama kansa ya utumbo mpana na mengineyo.
• Pia tunda hili linasaidia kuondoa constipation (choo kigumu) na kukuepusha kupata magonjwa ya mfumo wa chakula kama bawasili (vinyama sehemu za siri) kutokana na constipation ya muda mrefu.
Hivyo furahia aina hii ya fiber yani pectin katika tunda hili la apple utakuwa umejiepusha na magonjwa yafutayo
• Uzito mkubwa kupita kiasi
• Kitambi na magonjwa ya moyo
• Kiharusi yani stroke
• Bawasiri
• Mzunguko mbaya wa hedhi
• Ulevi wa vinywaji na vyakula vyenye sukari na vionjo vya kemikali
• Kisukari
3. Apple ni tunda ambalo lina aina ya sukari ambayo hutumika kuzalisha nishati ya mwili ambayo inaitwa FRUCTOSE.
Kutokana na tafiti mbali mbali hapa duniani aina hii ya sukari imeonesha kuwa chanzo kikubwa kinacho sababidha UZITO MKUBWA KUPITA KIASI, MAGONJWA YA MOYO, KISUKARI nk hivyo basi tunda hili linatakiwa liliwe katika kiwango ambacho sio hatari kwa afya yetu. Ulaji wa tunda hili bila mpangilio ni kisababishi kikubwa cha uzito mkubwa, insulini(kichocheo kinasawazisha sukari mwilini) kutofanya kazi, na kisukari cha ukubwani.
KUTOKANA NA KIWANGO KINGI CHA AINA HII YA SUKARI AMBAYO IMEKUWA NI HATARI KWA AFYA YETU AMBAYO INAKADIRIWA KUWA NI GRAMU 9.5 KWA APPLE LENYE UMBO ZAIZI YA KATI.
NOTE: KAMA WEWE NI MGONJWA WA KISUKARI, UZITO MKUBWA, UNA BELLY FATS (NYAMA UZEMBE AMBAZO NI ISHARI YA KWAMBA INSULINI IMEANZA KUPATA KIPINGAMIZI KWENYE UTENDAJI)
Nakushauri kwa siku moja kiwango cha tunda hili usizidishe gramu 15 kwa siku ambayo ni sawa APPLE MOJA NA KIGANJA CHA ZABIBU (Kumbuka apple na zabibu yote ni matunda yenye chachu unaweza kula katika mlo mmoja)
LAKINI KAMA WEWE NI MZIMA MWENYE AFYA NJEMA yani hauna kisukari, huna uzito mkubwa, huna nyama uzembe (belly fats), huna mafuta mabaya kwenye moyo na mishipa ya damu (bad cholesteral)
Nakushauri kuwa unaweza kula mpaka apple 2-4 kwa siku lakini hakikisha UNAFANYA MAZOEZI YAKUTOSHA AU KUJIHUSISHA NA SHUGHULI NGUMU ZA KIMAISHA. UKIFANYA HIVYO HUWEZI KUPATA MARADHI YASABABISHWAYO NA AINA HII YA SUKARI NDANI YA TUNDA LA APPLE.
Nina IMANI KUBWA UMEJIFUNZA NAMNA GANI UNAWEZA KUANDAA TUNDA LAKO KIKUBWA NI KUZINGATIA KUWA MATUNDA MAZURI NI ORGANIC.
Hakikisha UNAFUATA SHERIA KUU SABA ZA UOASHAJI WA MATUNDA KULINGANA NA MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA
1. Osha mikono yako kwa sekunde 20 kwa maji ya uvugu vugu na sabuni kabla ya kuandaa tunda lako.
2. Ondoa kipande chochote ambacho kimeharibika kwenye tunda lako
3. Osha kwa kusafisha kwa nguvu kwa kutumia maji yanayo safisi (tape water)
4. Osha tunda lako vizuri kabla ya kumenya /kula
5. Kama ni matunda /mboga tumua brashi maalumu safi yenye kuondoa wadudu na kemikali mbali mbali.
6. Chukua kitambaa chako SAFI KAUSHA MATUNDA YAKO.
7. KAMA NI MBOGA KAMA KABEJI TUPA MAGANDA YA NJE NA UBAKIZE YA NDANI (Hupunguza kiwango cha kemikali, wadudu na madawa mbali mbali)
NOTE: KUMBUKA NJIA HIZO ZIMETOLEWA NA MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA DUNIANI, ZINASAIDIA KUPUNGUZA DAWA ZILIZOPULIZIWA KWENYE MATUNDA, ZINASAIDIA KUONDOA WADUDU (VIMELEA) NA KUKUFANYA ULETUNDA LAKO SALAMA


0 Comments