May 29, 2016

JE, YAFAA MWANAMKE KUCHINJA NA MWANAMUME KULA KUTOKAMANA NA KICHINJO CHAKE?

Kuchinja ni miongoni mwa Ibadah, kwani zipo Ibadah ambazo wanashirikiana wanaume na wanawake,vile vile kuna Ibadah zinazowahusu imma wanaume pekee au wanawake pekee.....Ila katika kuchinja hii ni miongoni mwa Ibadah inayowajumlisha wote (mume na mke),sio kama vile wengi wetu tunavyodhani kwamba mwanamke hapaswi kuchinja na anapochinja inakuwa haraam kwa mwanamume kukila kichinjo kile,la hasha!! lazima ifahamike kwamba kuchinja ni Ibadah ya wote kwa kuzingatia masharti na adabu zilizoekwa na shari'ah za uchinjaji.
Kwa ushahidi wa kuonesha kwamba Ibadah ya kuchinja haijabainisha jinsia kwa mchinjaji,Anasema Allah ('Azza Wa Jallah):
((Basi Swali na uchinje kwa ajili ya Mola wako)) [Al-Kawthar: 2]

((Sema: Hakika Swalah yangu, na ibada zangu, na uhai wangu, na kufa kwangu, ni kwa ajili ya Allaah Mola wa viumbe vyote))
((Hana mshirika Wake. Na hayo ndiyo niliyoamrishwa, na mimi ni wa kwanza wa Waislamu)) [Al-An'aam: 162-163].
Amma tukizirudia aya hizo inatudhihirikia kwamba hakuna ubainisho wowote wa jinsia unaotajwa
Na Hadiyth iliyopokelewa toka kwa Yahya,kutoka kwa Ka'ab Ibn Maalik,Kutoka kwa Naafi,Kutoka kwa mwanamume wa kianswaar,kutoka kwa Muadh Ibn Sa'ad kwamba kijakazi mmoja wa kike alikuwa malishoni na kondoo wake katika Sai (mlima uliopo Madiyna) alichinja kondoo kwa kutumia jiwe lenye makali. Hivyo mtume (swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliuliza kuhusu hilo na akaamuru watu kula ile nyama. (Muslim: 24/2/4)
Kwa hivyo basi kutokana na hadiyth hiyo endapo kutapatikana vigezo hivi:
1) Mwanamke awe ni muislamu
2) Aanze kwa BismiLlaah (asome Basmala)
3) Apige Takbiyr (Allaahu Akbar) wakati wa kuchinja
Inakuwa halali hata wewe mwanamume kula.
Allaahu A'alam

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only