MAANA YA LAA ILAHA ILA LLAH

MAANA YA LAA ILAHA ILA LLAH

***“Hakuna apasae kuabudiwa ila Mwenyezi Mungu peke yake”. NA qurani inaendelea kutufahamisha “Na mimi (Mweneyezi Mungu) sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi” hapa limetajwa swala la IBADA je ibada ni kuswali kufunga na kutoa zaka tu?
Hapana IBADA ni jina lililokusanya kila alipendalo ALLAH na kulirizia ni ibada kwahiyo kuchinja, kukaa na watu vyema na mambo yote ambayo ALLAH anayarizia ni IBADA
NGUZO ZA LAA ILAHA ILA ALLAH
Neno hili LAA ILAHA ILLALLAH lina nguzo mbili: (Nafyu) Kukataa na (Ithbaatu) Kuthibitisha.
A)KUKATAA (Nafyu): Laa–Hapana, LAA ILAHA (hapana, hakuna wakuabudiwa)
**Nguzo ya kwanza ni kukataa kuabudu, kutegemea, kuomba, kutukuza, kiumbe chochote isipokuwa ALLAH. KWAHIYO NGUZO HII INAKUKATAZA YAFUATAYO
1 Kutambikia mizimu ya wababu, au kwenda makaburini kuwaomba waliokufa au kuwasemeza.
2 Kupiga ngoma za majini na kuwachinjia(Laa Ilaha illa Allah inakukataza kuchinja kwa ajili ya kiumbe chochote kile isipokuwa kwa ajili ya ALLAH
3 Kutumia hirizi au azima (Laa Ilaha illa Allah inakukataza)
B) KUTHIBITISHA (ITHBAAT) : ILA ALLAH (Isipokuwa Mwenyezi Mungu Allah peke yake)
***Nguzo ya pili ya LAA ILAHA ILLA ALLAH, ni ILLA ALLAH (ila Mwenyezi Mungu), kuthibitisha kwa mkazo kabisa kwamba ALLAH PEKE YAKE ndiye anastahiki kuabudiwa, bila mshirika. Kuthibitisha huku ni kwa KAULI, MOYO na VITENDO.
BAAZI YA AYA ZINAZOELEZEA SWALA LA KUMUABUDU NA KUMTEGEMEA ALLAH PEKEE YAKE KATIKA MAMBO YETU
1 “Na wale wanao jitenga na masanamu na mashet‟ani wasiyakurubie, na wakarejea kwa Mwenyezi Mungu katika mambo yao yote, wanayo bishara tukufu. Surat Zumar, 17
2 “Basi anaye mkataa Shet‟ani na akamuamini Mwenyezi Mungu bila ya shaka amekamata kishikio madhubuti, kisicho vunjika. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua”. Surat Baqara,256
3 “Na kila umma tuliwapelekea Mtume awaambie: Muabuduni Mwenyezi Mungu peke yake. Na jitengeni na Taaghuut (shetani)” Surat Nahl, aya 32

0 Comments