NAMNA YA KUOGA JANABA (josho la kisheria)


1). Unaanza kwa kutia Niyyah
(walakin tufahamu kwamba Niyyah haitamkwi isipokuwa mahala pake ni moyoni....kwani kule kukusudia tu inatosha)

2). Kisha unanawa mikono yako kabla ya kuitumbukiza katika chombo,halafu unaosha sehemu zako za siri
3). Kisha unatawadha wudhuu kaamil wa swalah......kama tunavyo fahamu kuhusu namna ya kutawadha ni wazi kwamba katika wudhuu kuna kusema "BismiLlaahi"....hivyo basi ukiwa chooni BismiLlaahi utaitamka moyoni pasi kudhihirisha na ukamilishe wudhuu wako
4). Baada ya wudhuu unajimwagia maji kichwani mara tatu na uingize au upitishe vidole vyako katika nywele hadi uhakikishe maji yamefika katika ugozi wa kichwa
5). Mwisho unakamilisha kwa kujimwagia maji kiwiliwili chote huku ukianzia upande wa kulia mara tatu,vile vile upande wa kushoto mara tatu (yaani uhakikishe maji yameenea kila sehemu ya kiwiliwili chako imma kwa kujisugua au kutojisugua)
Kufikia hapo josho lako limekamilika na unaweza kuswali namna hiyo
TANBIHI MUHIMU
Kwa kuwa josho la kisheria wudhuu unapatikana ndani yake,hivyo unapomaliza kuoga unaweza kuswali namna hiyo haikulazimu kutawadha tena endapo hukugusa utupu wako au hakikukupata chenye kutengua wudhuu (mfano: madhiy,wadiy,kinyesi,mkojo,ushuzi)...walakin ikiwa baada ya kukamilisha josho ikakupata hadathi,basi ni sharti utawadhe tena walakin haitokulazimu kurudia kuoga kwa sababu hadathi ndogo haitengui josho
MAELEZO YA ZIADI MUHIMU KWA MWANAMKE
1. Ama anavyooga mwanamume janaba ndivyo vivyo hivyo anavyooga mwanamke....halkadhalka,hedhi na nifasi utartibu ni huo huo wa janaba kama ulivyo hapo juu isipokuwa mwanamke unapotaka kujitwaharisha hedhi au nifasi itakulazimu ufumue nywele zako endapo umesuka lakini ikiwa ni janaba sio lazima kufumua
2. Mwanamke Itakapokoma damu ya hedhi au nifasi,ili kutambua au kuhakikisha utwahara umedhihiri......utachukua pamba au kitambaa safi,kisha utumbukize katika uke wako kitakapo toka imma kikavu au kikatoka na maji maji meupe au maji ya njano au maji maji ya rangi nyeusi basi yote haya ni dalili ya utwahara.
3. Baada ya josho unaweza tumia miski au aina yeyote ya manukato kuondoshea athari au harufu ya damu...kama tunavyofahamu jinsi gani hii damu ilivyokuwa na harufu mbaya
Na Allah Ndiye Ajuaye Zaidi.

0 Comments