MLANGO WA PILI
VYOMBO:
Vyombo ni vifaa ambavyo huifadhiwa ndani yake maji na vitu vingine,vyombo hivi huwa vimetengenezwa kwa bati,udongo n.k
Asili ndani ya dini yetu ni halali kutumia vifaa hivi,kutokana na kauli yake Allah Mtukufu:
(هُوَ الَّذِي خَلَقَ لَكُم مَّا فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا)
(Yeye ndiye aliye kuumbieni vyote vilivyomo katika ardhi)
Surat Al baqara:29
Kwa kuwa vitu vyote Allah katuumbia,basi ni halali kwetu kuvitumia isipokuwa kile ambacho yamepokelewa makatazo ya kuwa kitu hiki ni haramu.

Mlango wa kwanza:Vyombo
vilivyotengenezwa kwa madini ya dhahabu na fedha:
Haijuzu kutumia vyombo vilivyotengenezwa kwa dhahabu na fedha,na yajuzu kutumia vyombo vingine ambavyo havijatengenezwa kwa dhahabu na fedha,muda wa kuwa vyombo hivyo ni twahara.
Uharamu huu wa kutumia vyombo vilivyotengenezwa kwa dhahabu na fedha wajumuisha matumizi yote,sawa iwe ni kulia,kunywea na matumizi mengineyo.
Dalili ya uharamu wake:
Amesema mtume-swala Allahu alayhi wasallam-
(Msinywe katika vyombo vya dhahabu na fedha,wala msile kwa kutumia sahani zake,kwani ni vyao{makafiri}duniani,na vitakuwa ni vyenu{waislamu} akhera)Hadithi imepokelewa na Bukhari:5426 na Muslimu 2067.
Pia mtume-rehema na amani zimshukie-anasema:
(Yule ambaye anakunywa kwa kutumia vyombo vya dhahabu na fedha,basi moto wa jahannam utakuwa waunguruma katika tumbo lake{pindi atakapotupwa motoni})Hadithi imepokelewa na Bukhari:5634 na Muslimu 2065.
Imamu Nawawi-Allah amrehemu-katika kusherehesha kwake sahihi Muslimu amesema:Wamesema watu wetu{wa madhehebu ya imamu Shafii},wanazuoni wamekubaliana ya kuwa ni haramu kulia,kunywea na matumizi yote kwa kutumia vyombo vya dhahabu na fedha…ama kutajwa kwa matumizi ya kulia na kunywea katika hadithi,hakumaanishi ya kuwa matumizi mengine yanajuzu,lakini hadithi zimetaja matumizi ambayo yamekuwa yakitumiwa zaidi na vyombo hivyo nayo ni kulia na kunywea.
Hata hivyo kuna baadhi ya wanazuoni wanaona ya kuwa uharamu wa kutumia vyombo hivi vya dhahabu na fedha,ni uharamu katika kulia na kunywea tu,ama matumizi mengine yajuzu,na ndiyo maana katika hadithi yametajwa wazi matumizi haya ya kulia na kunywea,hali hii ikajulisha ya kuwa matumizi mengine kama vile kutawadhia yajuzu.

Somo la pili:Hukumu ya
kutumia chombo kilichoungwa kwa dhahabu au fedha:
Chombo kilichovunjika au kutoboka,kikiunganishwa/kikizibwa kwa kutumia dhahabu,ni haramu kukitumia kutokana na kuingia kwake katika makatazo ya hadithi zilizopita.
Ama chombo kilichovunjika au kutoboka kikaunganishwa kwa madini ya fedha kidogo,basi yajuzu kutumia,kutokana na hadithi ya Anasi-radhiya Allahu anhu-amesema:
(Kilipata ufa kikombe cha mtume-swala Allahu alayhi wasallam-ikazibwa sehemu ya ufa kwa {madini ya} fedha)
Hadithi imepokelewa na imamu Bukhari:3109.

Na katika hekima za
kuharamishwa kutumia vyombo vilivyotengenezwa kwa madini ya dhahabu na fedha ni
kuto wavunja moyo masikini na kuondosha hali ya kiburi na majivuno inayoweza
sababishwa na matumizi ya vifaa hivi-Allah ndiye mjuzi zaidi-.
MLANGO WA TATU
KUKIDHI HAJA NA ADABU ZAKE:
KUKIDHI HAJA NA ADABU ZAKE:
Somo la kwanza:Kustanji na Kustijmari,na
kimoja ya hivyo viwili kushika nafasi ya mwenzake:
Mja akienda kukidhi haja viungo vyake hupatwa na najisi,na namna ya kuisafisha najisi hiyo kuna njia mbili:Kustanji au Kustijmari.
Kustanji ni nini?
Kustanji ni kusafisha kile chenye kutoka katika tupu mbili kwa kutumia maji.
Kustijmari ni nini?
Kustijmari ni kupangusa chenye kutoka katika tupu mbili kwa kutumia kitu kisafi kama vile mawe karatasi{Toilet paper} n.k
Kwa kutumia moja ya njia mbili hizo au zote mbili mja huwa amekwisha jitoharisha kutokana na najisi,na kama anahitaji kuswali basi kilichobaki huwa ni kuchukuwa udhu na kuwa twahara tayari kwa kufanya ibada.

Dalili:
Katika hadithi iliyosimuliwa na Anasi bin Maliki-radhi za Allah zimshukie-anasema:
(Alikuwa mtume-swala Allahu alayhi wasallam-akitaka kuelekea msalani ninambebea mimi na kijana aliyekuwa makamo yangu chombo cha maji na fimbo,akawa anastanji kwa maji)Hadithi imepokelewa na Muslimu:271
Na katika hadithi iliyosimuliwa na mama wa waumini bibi Aisha-radhiya Allahu anhaa-amesema:Hakika ya mtume-swala Allahu alayhi wasallam-amesema:
(Akienda mmoja wenu chooni basi ajipanguse kwa mawe matatu,kwa hakika yatamtosheleza)Hadithi imepokelewa na imamu Ahmad:6/108.
Kwa hiyo kwa mujibu wa hadithi hiyo ya hapo juu,swala la kujipangusa{Istijmari} latimia kwa kutumia mawe matatu au kitu chochote twahara chenye kushika nafasi yake kama vile karatasi{toilet paper},vibao n.k
Wala haitoshi kujipangusa chini ya mara tatu au kwa kutumia kinyesi{mfano cha mnyama} au kwa mifupa,kutokana na hadithi ya Salmani-radhiya Allahu ahnu-pindi alipo sema:
(Alitukataza-mtume-kustanji kwa mkono wa kulia,kujipangusa kwa chini ya mawe matatu na kujipangusa kwa kinyesi na mifupa) Hadithi imepokelewa na Muslimu: 262.

Somo la pili:Kugeukia kibla
au kuupa mgongo upande wa kibla wakati wa kukidhi haja:
Haijuzu kugeukia kibla wala
kuupa mgongo upande wa kibla wakati wa kukidhi haja iwapo kama muhusika atakuwa
anakidhi haja sehemu ya wazi pasina ya kizuizi.
Na hii ni kutokana na hadithi iliyosimuliwa na Abu Hurayra-radhi za Allah zimshukie-hakika ya mtume-swala Allahu alayhi wasallam-amesema:
(Pindi mmoja wenu atakapokaa kwa ajili ya kukidhi haja,basi asigeukie upande wa kibla wala kuupa mgongo)
Hadithi imepokelewa na imamu Muslimu:389.
Ama iwapo kama vyoo vitakuwa vimejengwa au vimo ndani ya majumba au mbele ya sehemu ya kukidhi haja kutakuwa na kizuizi,basi hakuna tatizo,kutokana na ushahidi wa hadithi ya Ibun Omar-radhiya Allahu anhumaa- hakika yake(Alimuona mtume-rehema na amni za Allah zimshukie- akikojoa katika choo kilichokuwapo nyumbani pake akiwa kageukia upande wa Sham huku akiwa kaupatia mgongo upande wa al kaaba{kibla})
Hadithi imepokelewa na Bukhari:148 na Muslimu:266.
Hata hivyo licha ya kujuzu huku kugeukia upande wa kibla wakati wa kukidhi haja katika vyoo vilivyojengwa au sehemu yenye kizuizi,ni bora kujiepusha kabisa kugeukia upande wa kibla au kuupa upande huo mgongo.
Na hili ni katika kuutukuza upande huu ambao tunaelekea wakati wa swala.Allah ndiye mjuzi zaidi.

Somo la tatu:Mambo ya sunna
katika kukidhi haja:
Ni sunna kwa yule mwenye
kukidhi haja asome dua ya kuingilia chooni,nayo ni:
“BISMILLAHI ALLAHUMMA INNY AUUDHU BIKA MINAL KHUBUTHI WAL KHABAAITH”
“Kwa jina la Allah,ewe Mwenyezi Mungu,hakika yangu ninajilinda kwako na mashetani wa kiume na mashetani wa kike”
Na baada ya kukidhi haja wakati wa kutoka basi na asome dua hii:
“GHUFRAANAKA”
“Msamaha ni wako ewe Allah”

Imesimuliwa kutoka kwa
Ally-radhiya Allahu anhu-amesema:Amesema mtume-rehema na amani za Allah
zimshukie-:(Sitara iliyopo baina ya jini na na uchi wa mwanaadamu pindi
atakapoingia msalani ni kusema:Bismillahi)Ibun Majah: 297 na Tirmidhy:606.
Hata hivyo kwa kuwa haijuzu kutamka jina la Allah,mtu ukiwa msalani,basi Bismillahi pamoja na dua ya kuingilia mahali hapo unatakiwa utamke kabla ya kuingia msalani.
Hata hivyo kwa kuwa haijuzu kutamka jina la Allah,mtu ukiwa msalani,basi Bismillahi pamoja na dua ya kuingilia mahali hapo unatakiwa utamke kabla ya kuingia msalani.
Imesimuliwa kutoka kwa
Anasi-radhiya Allahu anhu-amesema:Alikuwa mtume-swala Allahu alayhi
wasallam-akiingia msalani anasema:
(Allahumma inny auudhu bika minal khubuthi wal khabaaith)Bukhari:142 Muslimu:375.
Pia hadithi ya bibi Aisha-radhiya Allahu anhaa-amesema:Alikuwa mtume-swala Allahu alayhi wasallam-akitoka msalani anasema:
(Ghufraanaka)Hadithi imepokelewa na Abudaud:17 na Tirmidhy:7.

Vile vile ni sunna
kutanguliza mguu wa kushoto wakati wa kuingia,na kutanguliza mguu wa kulia
wakati wa kutoka,
Pia muhusika asivue nguo zake isipokuwa atakapokaria sehemu ya kukidhia haja.
Imesimuliwa na Ibun Omara-radhiya Allahu anhumaa-amesema:(Alikuwa mtume-swala Allahu alayhi wasallam-pindi akihitaji kukidhi haja,basi hainui nguo zake mpaka aikaribie ardhi)Hadithi imepokelewa na Abu Daud:14
Na iwapo kama atakuwa anakidhia haja sehemu ya nje,basi aelekee sehemu ya mbali na ajisitiri ili asionwe.

Swahaba wa Mtume Jabir-radhi
za Allah zimshukie-amesema:Tulisafiri pamoja na mtume-swala Allahu alayhi
wasallam-akawa mtume hakidhi haja mpaka aelekee mbali na kuto onekana)Abu
Daud:2.Ibun Majah:335.
Somo la nne:Mambo ambayo ni
haramu kwa mwenye kukidhi haja:
1-Ni haramu kukojoa katika maji khususani yale yaliyo tuama,na hili ni kutokana na hadithi iliyosimuliwa na swahaba wa mtume Jabir-radhi za Allah zimshukie-kutoka kwa mtume-rehema na amani za Allah ziwe juu yake-(Hakika yake{mtume} alikataza kukojoa katika maji yaliyo tuama)Hadithi imepokelewa na Muslimu:281.

2-Pia ni haramu kushika tupu kwa mkono wa
kulia wakati wa kukojoa wala asistanji kwa mkono huo wa kulia. Kwani
mtume-swala Allahu alayhi wasallam-amesema:
(Mmmoja wenu akikojoa basi asishike tupu yake kwa mkono wa kulia wala asistanji kwa mkono wa kulia) Hadithi imepokelewa na Bukhari:154 na Muslimu:267.

3-Vile vile ni haramu kukidhi
haja ndogo au kubwa njiani,katika kivuli,katika bustani,chini ya mti wa matunda
au sehemu ya kuchota maji.
Na dalili juu ya hili ni hadithi ya Muadhi-radhi za Allah zimshukie-amesema:Amesema mtume-swala Allahu alayhi wasallam-(Ziogopeni laana tatu:Kujisaidia sehemu ya uchotaji maji,njiani na kivulini)Hadithi imepokelewa na Abu Daudi:62.

Na katika hadithi
iliyosimuliwa na Abu Hurayra-radhi za Allah zimshukie-hakika ya mtume-swala
Allahu alayhi wasallam-alisema:(Ziogopeni laana mbili),maswahaba wakauliza:”Ni
zipi hizo laana mbili ewe mjumbe wa Allah?” akasema:(ni zile anazozipata yule
anayejisaidia katika njia ya watu au kivuli chao)Muslimu:269.
4-Pia ni haramu kusoma Qur
ani, kwani Qur ani ni maneno ya Allah,kwa hiyo haifai kuyasoma maneno ya Allah
ukiwa sehemu ya kukidhi haja.
5-Vile vile ni haramu
kujisafisha najisi kwa kutumia kinyesi cha wanyama au mifupa au chakula chenye
kuheshimiwa.
Kutokana na ushahidi wa hadithi ya Jabiri-radhiya Allahu anhumaa-amesema:(Alikataza mtume-swala Allahu alayhi wasallam-kujifuta kwa kutumia mfupa au kinyesi)
Muslimu:263.

6-Pia ni haramu kukidhi haja
makaburini.Kwani eneo hili ni eneo la maziko,vile vile kuna wale wanaokwenda
kudhuru makaburi.Kutokana na hivyo wataudhika kutokana na haja hiyo
iliyokidhiwa katika makaburi.
Somo la tano:Mambo ambayo ni
makruhu
{yenye kuchukiwa} kwa mwenye kukidhi haja:

1-Yachukiwa kwa mwenye kukidhi haja
kuelekea upande wa upepo pasina ya kuwepo kizuizi,ili mkojo usije ukamrudia.
2-Pia yachukiwa kwa mwenye
kukidhi haja kuzungumza akiwa anakidhi haja.
Kwani imepokewa ya kuwa mtume-rehema na amani zimfikie-alikuwa akikidhi haja ndogo akapita mtu mmoja na kumsalimu,mtume-swala Allah alayhi wasallam-hakujibu hakujibu salamu.Muslimu:370

3-Vile vile yachukiwa katika
sheria kukojolea mashimo,sehemu iliyopasuka na matundu kiujumla yaliyopo
ardhini.
Kutokana na ushahidi wa hadithi ya Katada kutoka kwa Abdallah bin Sarjis amesema:
(Hakika ya mtume-swala Allahu alayhi wasallam-alikataza kukojolea mashimo,katada akaulizwa:Mashimo yanatatizo gani? Akajibu:Yaelezwa ya kuwa ni makazi ya majini)Hadithi imepokelewa na Abudaud:29 na Nasai:34.
Yachukiwa kukojoa sehemu kama hizi au kukidhi haja kiujumla kwani ndani yake kunawezakuwa na mdudu akamdhuru au kunaweza kuwa na jinni likamzuru.

4-Miongoni mwa mambo
yanachochukiwa{ni makruhu}kwa mwenye kukidhi haja ni kuingia na kitu chochote
ambacho ndani yake kina jina la Allah,kwani mtume-swala Allahu alayhi
wasallam-(Alikuwa akitaka kuingia msalani anavua pete yake)Hadithi imepokelewa
na Abudaud:19 na Tirmidhy:1746.
Na hii ni kutokana na kuwa katika pete ya mtume kulikuwa na jina la Allah.
Hata hivyo kukiwa na dharula na ulazima unaopelekea mja kuingia chooni na kitu kilichoandikwa jina la Allah basi hakuna tatizo,kama vile kuingia na pesa ambazo zimeandikwa jina la Allah,kwani mja akiziacha nje zinaweza kuibiwa au anaweza zisahau.

Ama kuhusiana na msahafu,ni
haramu kuingia nao chooni,kwani Qur ani ni maneno ya Allah,nayo ni maneno
yaliyo matukufu,na kuingia nayo chooni ni aina ya kuyadhalilisha.
MLANGO WA NNE:
MSWAKI NA SUNNA ZA KIMAUMBILE
MSWAKI NA SUNNA ZA KIMAUMBILE
Somo hili linajumuisha maswala mbali
mbali:
Kupiga mswaki:Ni kusafisha meno kwa kutumia mswaki wa mti au mfano wake,kwa ajili ya kuondoa mabaki ya chakula na harufu mbaya.

Somo la kwanza:Hukumu yake:
Kupiga mswaki ni sunna katika nyakati zote,mpaka kwa mfungaji anaruhusiwa kupiga mswaki wakati wowote,sawa iwe ni asibuhi au jioni.

Kwani mtume-swala Allahu
alayhi wasallam-amehimiza mahimizo yaliyo wazi pasina ya kutaja muda maalumu,
ametueleza kwa kusema:
(Kupiga mswaki ni twahara ya mdogo,ni sababu ya kupata radhi za Allah)Bukhari,mlango wa funga2/40.
Pia mtume-swala Allahu alayhi wasallam-amesema:
(Laiti kama nisingehofia kuwatilia uzito umati wangu,basi ningewaamrisha kupiga mswaki wakati wa kila swala)
Bukhari:887,Muslimu:202.

Somo la pili:
Ni wakati gani hukokotezwa kupiga mswaki?

Yakokotezwa zaidi au
yahimizwa zaidi kupiga mswaki wakati wa kutawadha,wakati wa kuamka kutoka
usingizini,pindi harufu ya mdomoni inapo badilika,wakati wa kusoma Qur ani na
wakati wa swala.Pia yahimizwa zaidi wakati wa kuingia msikitini na wakati wa
kuingia nyumbani,
Kutokana na hadithi ya
Mikdadi bin Shariih kutoka kwa baba yake amesema:Nilimwuliza Aisha-radhiya
Allahu anhaa-ni jambo gani ambalo mtume-rehema na amani za Allah
zimshukie-alikuwa akilianza pindi anapo ingia nyumbani kwake?
Akasema:Mswaki{jambo la kwanza lilikuwa ni kupiga mswaki}.Muslimu:203.

Pia yahimizwa zaidi kupiga mswaki
pindi mtu anapokaa kimya kwa muda mrefu au meno yanapobadilika na kuwa ya
njano,kutokana na dalili ya hadithi hizo zilizopita.
Alikuwa mtume-swala Allahu
alayhi wasallam-akiamka usiku akipitisha mswaki.Bukhari:245.Muslimu:255.
Kiujumla ni kuwa muislamu anatakiwa wakati wa kuingia katika ibada awe katika hali nzuri kiusafi na utwahara.

Somo la tatu:Kupiga
mswaki/Kusafisha meno kwatimia kwa kutumia nini?
Ni sunna kusafisha meno kwa
kutumia mswaki wa mti mbichi,usiovurugika kwa harakaa wala haujeruhi mdomo.
Kwani mtume-swala Allahu alayhi wasallam-alikuwa akisafisha meno kwa kutumia mswaki wa mti wa Arak.
Wakatika wa kupiga mswaki anaweza kutumia mkono wa kulia au wa kushoto.Pia yajuzu kusafisha meno kwa kutumia miswaki ya plastiki ya kisasa.

Wakatika wa kutawadha mja akiwa hana
mswaki basi yafaa pia kutumia vidole vyake,kama lilivyopokelewa hilo na Ally
bin aby Twalibi-radhiya Allahu anhu-kuhusu namna ya udhu wa mtume-swala Allahu
alayhi wasallam-
Hadithi imepokelewa na imamu Ahmad 1/158.

Somo la nne:Faida za kupiga
mswaki:
1-Faida ya kwanza ni ile
tuliyo ielezea katika hadithi iliyopita,ya kuwa ni twahara ya mdomo duniani na
ridhaa kwa Mola kesho akhera.
Kutokana na hivyo yapendeza kwa mja ashikamane na sunna hii wala asiiache kutokana na faida yake.
Kuna baadhi ya watu wanaweza kaa hata mwezi pasina ya kupiga mswaki,bila shaka watu hawa wanapitwa na faida kubwa ya ujira,lakini pia hali hii haiendani na mafundisho ya dini yetu inayohimiza usafi.
Mtume-rehema na amani za Allah zimshukie-alikuwa akiihifadhi sunna hii na kuuhimiza umma wake.

2-Huondosha harufu mbaya
mdomoni
3-Miongoni mwa faida za kupiga mswaki ni kuimarisha meno na fizi.
4-Huyafanya meno yawe meupe.
5-Huisafisha sauti.
6-Humchangamsha mja.

Somo la tano:Sunna za
kimaumbile:
Sunna hizi zifuatazo zimeitwa
ya kuwa ni sunna za kimaumbile kutokana na kuwa mtendaji wake anasifika kwa
kufuata maumbile na asili ambayo Allah kawaumbia watu na kuwahimiza juu ya vitu
hivyo,ili waweze kuwa katika hali iliyokuwa nzuri na ukamilifu.
Imesimuliwa kutoka kwa Abu Hurayra-radhiya Allahu anhu-amesema:Amesema mjumbe wa Allah-rehema na amani za Allah zimfikie-:
(Mambo matano ni katika maumbile{na asili}:Kunyoa nywele za sehemu za siri,kutaili,kukata masharubu,kuondoa nywele za kwapani na kukata kucha)Hadithi imepokelewa na Bukhari:5889 na Muslimu:257.

1)KUNYOA NYWELE ZA SEHEMU ZA
SIRI:
Jambo lakwanza miongoni mwa maswala hayo ya kimaumbile ambalo mtume-swala Allahu alayhi wasallam-kaanza kwa kulitaja ni kuondosha nywele za sehemu za siri,hili lazingatiwa ni katika usafi.
2)KUTAILI:
Jambo la pili kipenzi chetu katueleza kuwa ni Kutaili.
Nako ni kuondosha ngozi ya juu katika utupu wa mwanamume.Jambo hili ni wajibu kwa wanamume.
Wanawake nao kutaili kwao ni kupunguza nyama kidogo sana katika kijinyama kilichozidi au kujitokeza sehemu husika.
Upande wa wanawake yaelezwa kuwa jambo hili ni sunna na wala si wajibu kwao.
HEKIMA YA KUTAILI:
Hekima katika kuwataili wanaume ni kuutoharisha utupu kutokana na najisi zinazoweza kujificha katika ngozi.Ama hekima upande wa wanawake ni kuwa yasaidi katika kupunguza ukali wa matamanio.
MUDA MZURI WA KUTAILI:
Yapendeza zaidi swala hili likatekelezwa siku ya saba tokea kuzaliwa kwa mtoto,kwani hali hii yapelekea kupona haraka,pia kumfanya mtoto akuwe katika hali ya ukamilifu.

3)KUKATA MASHARUBU:
Jambo la tatu ni kukata masharubu,kwa kufanya hivyo pia mja anakuwa anajipamba na kujisafisha na anakwenda kinyume na makafiri ambao hawana muongozo kama huu.
Zimepokelewa hadithi mbali mbali katika kuhimiza juu ya kukata masharubu na kuziacha ndevu na kuzikarimu kwa kuziweka katika mazingira mazuri.Kutokana na kuwa kubaki kwa ndevu kwaonesha uzuri wa madhhari ya uwanaume. Hata hivyo kwa masikitiko makubwa watu wengi wamefanya kinyume juu ya jambo hili,wanaacha masharubu na kunyoa ndevu au wanazipunguza,na katika hali zote hizo mbili kunyoa au kupunguza ni kwenda kinyume na sunna{mwenendo} na amri zilizo pokelewa juu ya uwajibu wa kuzifuga.
Allah Mtukufu anatueleza:
(وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانتَهُوا وَاتَّقُوا اللَّـهَ إِنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ)
(Na anacho kupeni Mtume chukueni, na anacho kukatazeni jiepusheni nacho. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu)
Surat Al hashri:7.
Na katika hadithi zilizokuja katika kutuhimiza juu ya swala zima la kunyoa masharubu na kufuga ndevu na hadithi iliyosimuliwa na Abu Hurayra-Allah amridhie-amesema:Amesema mjumbe wa Allah-rehema na amani za Allah zimshukie-:
(Nyoeni masharubu na ziacheni ndevu,nendeni kinyume na wamajusi)Hadithi imepokelewa na imamu Muslimu:260.
Pia hadithi ya Ibun Omar-radhiya Allahu anhumaa-kutoka kwa mtume-rehema na amani zimshukie-amesema:
(Tofautianeni na washirikina,fugeni ndevu na nyoeni masharubu)Hadithi imepokelewa na Bukhari:5892 na Muslimu:258 na tamko ni la Bukhari.
Kutokana na hivyo yatakikana kwa muislamu ashikamane na mwongozo huu wa mtume,aende kinyume na wasiokuwa waislamu na kujiweka mbali na kujifananisha na wanawake.

4)KUKATA KUCHA:
Jambo la nne ni kukata kucha,haitakiwi kuziacha kucha mpaka zikarefuka sana,bali yatakiwa kuzikata kila zinapokuwa.Na kuzikata kwazifanya zipendeze na kuondosha uchafu ambao hukaa chini yake.
Pia kuna baadhi ya waislamu wanaenda tofauti na mwongozo huu wa mtume,utawaona wanaacha kucha zao mpaka zinakuwa ndefu au baadhi ya kucha.Huu si mwongozo wetu bali tushikamane na mafundisho yetu.

5)KUONDOSHA NYWELE ZA
KWAPANI:
Yatakikana pia kuondosha nywele za kwapani kwa kuzinyofoa au kuzinyoa.Kwani kuziondosha nywele hizo ni katika usafi na kuondosha harufu mbaya ambayo huzidi kwa kukua kwa nywele za sehemu hiyo.

Hii ndiyo dini yetu
safi,ametuamrisha mambo haya,kwani kwa kufanya hivyo mja anakuwa katika hali
nzuri na usafi.Pia anakuwa mbali na kuiga tamatuni zinazoenda tofauti na
uislamu na kujifakharisha na dini yake ,akimtii mola wake na kufuata mwongozo
wa nabii wake-rehema na amani zimshukie-.
soma fiqih DARSA YA FIQHI 1
In
shaa Allah katika darsa letu lijalo tutaingia katika somo la udhu.
Post a Comment