FADHILA ZA SIKU YA IJUMAA


1:Siku ya ijumaa ni katika siku bora.
Imesimuliwa kutoka kwa Abu Huraira-radhiya Allahu anhu-kutoka
Kwa Mtume –swalla Allahu alayhi wasllam-Amesema:
(Siku iliyo kuwa bora katika masiku ambayo limechomoza jua ni siku ya ijumaa.
Ndani ya siku hii aliumbwa Adam,na ndani ya siku hii aliingizwa peponi ,na ndani ya siku hii alitolewa peponi{na kushushwa ardhini},na wala hakito simama kiyama isipokuwa siku ya ijumaa).Hadithi imepokelewa na Muslimu.
2:Siku ya ijumaa ni siku ya waumini kukusanyika katika swala ya pamoja,swala ambayo inatofauti na swala tano,kwani swala hii hupendezwa zaidi kuswaliwa katika misikiti iliyo kuwa mikumbwa yenye kukusanya idadi kubwa ya waumini na kufunga misikiti midogo kama hakutokuwa na uzito juu ya suala hilo.
3:Siku ya ijumaa kuna saa ambayo dua hujibiwa :
Imesimuliwa kutoka kwa Abu Huraira-radhi za Allah ziwe juu yake-amesema:
Kasema Mjumbe wa Allah-rehema na amani ziwe juu yake:
(Hakika siku ya ijumaa kuna saa ambayo hato iafiki mja muumini akawa kasimama akiswali na kuomba Allah kitu ,isipokuwa Allah atampatia mja huyu kile kitu alicho kiomba) Hadithi imepokelewa na Bukhari na Muslimu.
Kutokana na hadithi na ushahidi mbali mbali , yaonesha rai yenye nguvu kuhusiana na saa hii ambayo hupokelewa dua:ni kwamba saa hii yapatikana kati ya swala ya alaasiri na magharibi.
4:Swadaka ndani ya siku ya ijumaa ni bora kulikoni masiku mengine:
Kama ilivyokuja katika hadithi liyo pokelewa na Kaabu(Swadaka ndani ya siku ya ijumaa ni bora kulikoni swadaka katika masiku mengine)
Anasema imamu Ibun al Kayyim-rahimahu LLAH-"Na swadaka ndani ya siku ya ijumaa ukilinganisha na masiku ya wiki ni kama vile kutoa swadaka ndani ya mwezi mtukufu wa ramadhani ukilinganisha na miezi mingine"
5:Siku ya ijumaa ni sukukuu ya wiki:
Kutokana na hivyo yapendeza kuoga na kuvaa nguo nzuri.
Mtume-swalla Allahu alayhi wasallama- anasema:(Hakika siku hii{ya ijumaa}ni siku ya iddi{sikuku}aliyo ijaalia Allah kwa waislamu,yule atakayekuwa anaelekea kuswali kwa ajili ya swala ya ijumaa basi na aoge)yaani:Allah kaifanya siku hii ya ijumaa kuwa ni sikukuu kwa waislamu.
6:Siku ya ijumaa ni siku ambayo waja husamehewa madhambi:
Imepokelewa kutoka kwa Salmani-radhi za Allah ziwe juu yake-amesema:
Amesema Mtume-swalla Allahu alayhi wasallam-(Haogi mtu siku ya ijumaa,na akajitoharisha kadri ya uwezo wake katika kujitoharisha,na akajipaka mafuta yake ,au akagusa{ akajipulizia} manukato ya nyumbani kwake,kisha akatoka kuelekea msikitini,akawa si mwenye kufarikisha kati ya watu wawili,kisha akaswali rakaa alizo andikiwa{pangiwa} kuziswali,kisha akawa ni mwenye kutulia na kukaa kimya pindi anapo zungumza imamu{khatwibu},isipokuwa mja huyu husamehewa madhambi yaliyo kati ya ijumaa hiyo na ijumaa nyingine)Hadithi imepokelewa na Bukhari.
Madhambi haya yanayo samehewa kati ya ijumaa na ijumaa nyingine ni madhambi madogo madogo,ama madhambi makubwa huitaji toba maalumu ya mja kwa kukaa na kutubia madhambi hayo makubwa,kama vile Kumshirikisha Allah,Kuuwa,Kuzini,kunywa pombe na mengineyo.Na kama dhambi aliyo ifanya ilikuwa ni kuiba mali ya mtu basi airudishe mali ile kwa wahusika.
Twamuomba Allah aturuzuku elimu yenye manufaa,na matendo mema.
Allahumma amiiyn.

0 Comments