CHANGIA UJENZI WA MSIKITI KHERI ULIOPO SAENI KIBAHA MKOANI PWANI

Asalaam Alaikum Warahmatullahi wabarakaatuhu. Ndugu Muislamu. Tunauomba mchango wako kwa ajili ya Miradi yetu ya Ujenzi wa Msikiti wa Kheri na Kituo cha Kijamii. Ujenzi wa Msikiti umeshaanza na unaendelea. Lakini pia tuna lengo la kujenga Zahanati, Maktaba, Nyumba ya Imamu na Mwalimu wa Msikiti wa Kheri uliopo Saeni, Misugusugu, Kibaha, Mkoa wa Pwani. Hadi sasa, tumekwishafanikiwa kuchanga pesa na kununua kiwanja kwa ajili ya kuongezea eneo la Msikiti, na ndani ya mwezi mmoja tumeshaanza ujenzi wa Msikiti wetu kwa kuchangishana! 

Tunalileta Ombi letu kwako, ndugu yetu Mwislamu kwa sababu tunahitaji kutekeleza miradi yetu yote. Na kwa ushirikiano wako tutafanikiwa. Na pia kuna eneo linalouzwa Milioni moja na laki tano ambalo fikra yetu ni kuliongezea kwenye eneo la Msikiti wetu liwe sehemu ya Mradi wetu. Kwa hivyo ndugu yangu katika Uislamu, mchango wako wa hali na mali, unahitajika sana. Chochote unachotaka kuchangia, iwe vifaa au fedha, tafadhali sana, wasiliana nasi kupitia namba zifuatazo: +255 715 460 859 au +255 714 880 539. Na kwa wale walio nje ya Tanzania, wanaweza kutuma Misaada yao kwa Western Union au Money Gram au Bakaal. Na jina la Mpokeaji ni: Hassan Juma Mpondo. Na kwa maelezo zaidi, usisite kuwasiliana nasi kwa namba hizo hizo. Ni mimi mtumishi wenu Mratibu wa Mradi, Hassan Juma Mpondo (Shawaal). Asante sana.

0 Comments