Pilipili manga ni mbegu ndogondogo zenye umbo la mviringo zenye rangi
nyeusi.mbegu hizi hutoa ladha ya muwasho mfano kama pilipili na kutumika
sana majumbani hasa upande wa jikoni, wapo wanaotumia kiungo hiki
kikiwa kizima au kimesagwa inategemea na mtumiaji anavyopendelea.
Wanawake
wengi wa pwani hutumika pilipili manga katika vyakula ili kunogesha na
kukipa ladha iliyo nzuri chakula, kitoweo hata kinywaji. Pia wapo
wanaotumia pilipili manga kuramba endapo watahisi kifua kinawabana.
Licha ya kuwa pilipili manga si dawa ya kifua ila kwa mazoea tumeipa
nafasi pilipili manga kuwa ina uwezo wa kutibu kifua kama ifanyavyo
tangawizi.
Faida ya matumizi ya pilipili manga kwa wanawake.
Pilipili
manga ina faida kubwa kwa mwanamke ambaye ameshajifungua, hivyo ni vema
uji anaokunywa uwekwe unga wa pilipili manga kwani humsaidia kutoa
uchafu utakaokuwa upo kwenye kizazi ambao umebakia.
Humuondolea
maumivu ya mwili pamoja na tumbo, humsaidia kutoshika mimba katika
kipindi hicho ambacho analea mtoto wake mchanga. Wapo baadhi ya watu
wakila chakula au mchuzi rosti wa biriani ambayo inakuwa haijachanganywa
na kiungo hiki hupata ugonjwa wa kuharisha au kupata maumivu makali ya
tumbo.
Lakini endapo utaweka pilipili manga kiasi kidogo basi mtu
huyo hatoweza kuharisha wala kuumwa na tumbo hivyo kwa upande mwingine
kiungo hiki huisaidia kutibu tumbo kwa mlaji. Katika matumizi ya watu
wengi inashauriwa itumike pilipili manga ambayo ni nzima ili mtu ambaye
inamdhuru akiwa anakula chakula ni lazima ataona vitumba vya pilipili
manga na kuviondoa.
Madhara ya matumizi ya pilipili manga;
Kwa
mwanamke anayehitaji kupata mtoto haruhusiwi kutunmia kiungo hicho kwa
wingi kwani kinaweza kumsababishia kushindwa kushika ujauzito na hivyo
kuhangaika kwa muda mrefu licha ya kutumia dawa za kila aina. Mwanamke
yeyote ambaye anahitaji kupata mtoto anatakiwa ajichunge sana na vyakula
anavyokula kwani viko vyakula vingine vina uwezo wa kumsababishia
kushindwa kushika ujauzito kwa urahisi.
Usitumie pilipili manga
kutibu kifua. Kiungo hiki kinapoliwa na mgonjwa wa kifua humsababishia
kukohoa mara mbili zaidi ya hapo awali. Kutokana na muwasho, kiungo hiki
kuingia moja kwa moja kwenye mapafu na kusababisha mkwanguo ambao
unaweza kuleta madhara ya mgonjwa kukohoa damu.
Wapo wanaotumia maji
ya limao na pilipili manga pindi wanapokohoa. Ni vema waache mara moja.
hii ni hatari sana. Pia kiungo cha pilipili manga husababisha ugonjwa wa
vidonda vya tumbo hasa kwa ambao hupenda kunywa uji uliotiwa pilipili
manga kwa wingi wakitumia kama ndio kifungua kinywa.
Elewa kuwa
utumbo ni laini sana hivyo ni vizuri kujijali hasa katika matumizi ya
vyakula vyenye pilipili chache na nyingi kabla ya kula chakula chochote.
Hukatazwi kunywa uji wenye pilipili manga ila unatakiwa kuweka kiasi
kidogo sana cha kiungo hicho ili kukuepusha na madhara ya vidonda vya
tumbo.
Angalizo:
Wanawake waliokuwa ndani ya ndoa punguzeni
matumizi ya pilipili manga na hatimaye ongezeni matumizi ya mdalasini.
Mdalasini unaweza kutumiwa kwa jinsi zote ukiwa mapande mapande au
umesagwa na kuwa unga. Unga wa mdalasini huchanganywa na asali kisha
watumiaji wale kijiko kimoja cha chakula asubuhi, mchana na jioni. Hii
itamsaidia sana katika suala la kupata mtoto, watu waliogundua matumizi
ya pilipili manga katika kipindi cha kujifungua hawakuwa wajinga kwani
kiungo hiki kilikuwa kinatumika enzi na enzi za babu na bibi zetu.
Meat Tarts With White Sauce
-
Ingredients:
Dough:
1½ cups flour
½ tsp salt
½ cup chilled butter pieces
4-5 Tbsp cold water
The filling:
Cooked minced meat (or chicken pieces), ...
Post a Comment