IMAAM IBN BAAZ : HUKMU YA ANAYESWALI SWALA YA IJUMAA PEKEE NA KUACHA SWALAAH ZILIZOBAKI

Hukmu Ya Anayeswali Ijumaa Pekee Na Kuacha Swalaah Zilizobaki

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)SWALI:
Kuna mtu anaswali Ijumaa pekee bila kuswali Fardhi zilizobaki, je, inakubaliwa Swalaah yake?JIBU:
Haikubaliwi Swalaah yake, kwa hakika amekuwa Kafiri kwa hilo.

Swalaah yake ya Ijumaa, Swawm yake, na matendo yake yote ni batili.

Anasema Aliyetukuka:
"Na kama wangemshirikisha bila shaka yangebatilika yale waliyokuwa wakitenda." [Al-An'aam: 88]

Na Anasema Aliyetakasika:
"Na yeyote atakayekufuru iymaan; basi kwa yakini zimebatilika 'amali zake; naye Aakhirah atakuwa miongoni mwa waliokhasirika." [Al-Maaidah: 5]

Basi yule anayekufuru kufru kubwa au shirki kubwa, huporomoka matendo yake.
Tunamuomba Allaah afya (Atulinde).
Na kuacha Swalaah ni kufru kubwa."

[Nuwr 'Alaa Ad-Darb, 13/339]

https://play.google.com/store/apps/details?id=com.muislamu.blog

0 Comments