MUUJIZA WA KISAYANSI NDANI YA QUR ANI MAENDELEO YA UJAUZITO NDANI YA TUMBO LA MAMA:


Mwenyezi Mungu Mtukufu anatueleza:
(Enyi watu! Ikiwa nyinyi mna shaka ya kufufuliwa basi kwa hakika Sisi tulikuumbeni kutokana na udongo, kisha kutokana na manii, kisha kutokana na kipande cha damu ilio gandana, kisha kutokana na kipande cha nyama chenye umbo na kisicho kuwa na umbo, ili tukubainishieni)Surat Alhajj:5

Mwenyezi Mungu Mtukufu ameamua kuelezea vipindi tunavyovipitia mpaka kuja kuzaliwa kwetu,hata hivyo vipindi hivi na maendeleo haya yaliyoelezewa ndani ya aya hii,yaliwashangaza sana wataalamu wa ujauzito miongoni mwao
profesa Keith L.Moore kutoka Kanada katika chuo kikuu cha Toronto,huyu ni miongoni mwa madaktari bingwa wa ujauzito,basi pindi aliposikia maneno haya hakuamini kuwa ni maneno yaliyotoka ndani ya Qur ani tukufu.
Na alipopata uhakika kuwa maneno haya yametoka ndani ya Qur ani,basi akafanya udadisi zaidi na kutaka kujua iwapo kama maneno haya yametajwa sehemu moja tu kama vile bahati mbaya,lakini pindi alipoona ya kuwa maneno mfano wa hayo yametajwa mara ishirini na tano ndani ya Qur ani kuhusu maendeleo ya ujauzito ndani ya tumbo la mama yake,basi hakusita kuwa msomi aliye shujaa na kutangaza rai yake wazi kwa kusema:
“Kwa hakika dalili hizi hapana shaka zimemshukia Muhamad kutoka kwa Mwenyezi Mungu,na hali hii yanithibitikia ya kuwa Muhamad ni mtume wa Mwenyezi Mungu”

0 Comments