BI. KARLA EVANS AMESILIMU BAADA YA KUTAZAMA KIPINDI KATIKA CHANNEL YA KIISLAMU

Bibi Karlas Evans ni mmarekeni pia ni msomi mwenye macho ya blue na nywele za blond, ambaye alikuwa mkirsto aliacha dini yake na kuifuata dini hii ya haki dini ya Kiislamu ambapo watu wengi wasio Waislamu wanaituhumu kuwa ni dini ambayo inamdhalilisha mwanamke.

Tumuache Karlas azungumzie mwenyewe. Anaanza kwa kuelezea kwa kutoridhika kwake kwa nadharia ya kwamba `Jesus as a God` (Yaani yesu ni Mungu). Na jinsi gani alivyogundua ukweli wa mwanamke wa kiislam ambao ndio uliomfanya kufuata dini ya Kiislamu.


Anaanza kwa kusema kuwa mpangilio wangu wa kutoka katika ukristo na kuingia katika Uislamu, ulichukuwa muda mrefu sana zaidi ya miaka 20. Ulianza tokea nina umri wa miaka 12. Nilikuwa nikisoma katika Private school (shule ya kulipia). Tulikuwa tukifundishwa masoma ya dini tofauti. Na nilikuwa na vitabu vya dini tofauti, kama vile vitabu vya dini ya kikristo, kitabu kimoja cha dini ya kiyahudi, kitabu kimoja cha Quran (dini ya Kiislamu), kitabu cha dini ya kihindu na Kibudha.


Anasema ninakumbuka jinsi nilivyo vutiwa na kitabu cha dini ya Kiislamu (Quran) na nikaelewa kwamba, Waislamu hawakuwa wanafki kama wakristo (anamaanisha ameelewa hayo baada ya kusoma vitabu vya dini zote).


Nilikumbuka mambo mawili ambayo yamenivutia katika Quran. Jambo la kwanza ni kumuabudu Mwenyeezi Mungu mmoja pekee. Daima Nilikuwa nina jiuliza Kwanini wakristu wanaamini kwamba jesus (yanni Nabii Issa) ni mungu na jinsi gani wanakwenda kinyume na maarisho ya Mwenyeezi Mungu. Jambo la pili ni Kuhusiana na swala, si kwa sababu uislamu au wauslamu wana swali swala tano kwa siku lakini kwa jinsi yawafuasi wengi wa dini ya kislamu wanavyoswali na kumuabudu Mwenyezi Mungu mmoja pekee. Katika Ukiristo au dini ya kikristo swala ni kama kutaka kitu kwa Mwenyeezi Mungu, Kwa Kusema Mungu nipe hiki na kile basi si kufanya ibada kama katika Uislamu.

Anaedelea Karlas kwa kuelezea, nilikwenda kusoma katika college mjini Washington DC, ambapo huko kuna idadi kubwa ya wafuasi wa dini ya Kiislamu. Mvuto wangu kwa dini ya Kiislamu ulikuwa bado uko palepele lakini nilikuwa ninaona aibu kumwambia mtu yoyote nchini Marekani. Nilikuwa nikienda msikitini, katika vituo vya Kiislamu (Islamic center) lakini niliona aibu kuingia ndani. Nilikuwa nikiona darasa za dini na watu wanaoupenda Uislamu lakini nilishindwa kufanya kama wao, mwisho nikaamua kununua Quran na kuisoma mwenyewe nyumbani. Nilishangazwa sana, kila nilicho kisoma katika Quran nilihisi kinaniingia katika moyo wangu. Na jambo kubwa la kushangaza ni kuona jinsi mwanamke katika Uislamu alivyo pewa haki na usawa. Nafikiri watu wengi watanicheka lakini kwa mtu ambaye amesoma Biblia atajuwa kuwa katika Quran kuna haki mwanamke ambazo amepewa ambazo katika biblia hakupewa. Katika Quran mwanamke anahaki ya kumkataa mwanamume katika ndoa au kumkubali kuolewa nae. Wakati katika ukristo hasa katika utamaduni wa Magharibi katika wakati wa miaka ya nyuma (600CE), wanawake waliangaliwa kuwa ni mali ya mzee (baba yake). Baba yake ndio anahaki ya kuamua kumuozesha mtoto wake wa kike, na kuhusiana na urithi alikuwa hapati ila mtoto wa kiume mkubwa, haki hii haikuwepo nchini Marekani ila katika karne ya 19 (akimaanisha Uislamu ulisha fundisha hayo tokea zaidi ya miaka 1400 iliyo pita.)


Siku moja nilipokuwa nikitazama T.V. niliona kipindi kinahusiana na (الدعوة) ulinganiaji. kipindi hiki kilikuwa kinaonyesha jinsi mwanamke wa kimagharibi anavyolinganiwa katika Uislamu kwa njia yeyote ile. Nilikuwa nikikifuatilia sana kipindi hiki, na siku ambayo sikuwepo nyumbani nilikuwa nikikirikodi. Kipindi hiki kilikuwa kikiletwa kila siku ya ijumaa, lakini sikumbuki kilikuwa kikiletwa na chanel gani? Daima kipindi hiki kilianza kwa kusema BismiLahi Rahmaani Raheem (kwa jina la Mwenyeezi Mungu mwingi wa rehema na mwingi wa ukarimu). Na mwisho kabla ya kumalizika kipindi alikuwa akionyeshwa huyo mtu aliyelinganiwa akitamka shahada (akisilimu). Na mimi nikaitamka shahada kama ilivyokuwa ikionyeshwa katika T.V. Ni kasema katika nafsi yangu kwa uwezo wa Allah hivi mimi nimeshakuwa Muislamu kwa kuigiza kuitamka shahada! nikajisemea katika nafsi yangu sijui! kwa bahati mbaya nilikuwa simjui Muislamu yoyote ili anielezee kuhusu Uislamu na nilikuwa ninaogopa kwa familia yangu na marafiki zangu wasijue kuwa mimi nimekuwa au ninataka kuwa Muislamu.


Mnamo mwaka 1990 au 1991 ubalozi wa Saudi Arabia ulifanya maonyesho ya Kiislamu ya kuandika na kuchora. Nilimuuliza mmoja kati ya watu waliokuwepo katika maonyesho ili anieleze kuhusu Uislamu. Akanijibu mtu huyo kuwa hana nafasi ya kunieleza chochote kutokana na msongamano wa watu, kwa hivyo sikujua niende wapi ili nipate mtu anieleze zaidi kuhusu Uislamu. Na kujibu maswali yangu kwani niliona aibu kwenda msikitini pia sikujua kama mwanamke anaruhusiwa kuingia msikitini na nivae vipi ili niweze kuingia msikitini au nitakuwa ni mimi peke yangu ambaye sijui kuongea kiarabu.
Basi nikawa naendelea kuisoma Quran na kumuomba Mwenyeezi Mungu Mtukufu na nikaaamini kuwa Mwenyeezi Mungu atanikubalia dua yangu.
Shauku yangu kwa kumtegemea Mwenyeezi Mungu haikuisha japokuwa niliamua kufuata dini ya ukristo. Lakini tatizo ni kwamba daima nilikuwa ninajiuliza kuhusu dini hii ya Kikristo. Hasa kuhusiana na utatu na utakatifu wa Yesu na kuwa yeye ni Mungu. Jambo ambalo nilikuwa ninahisi si la uhakika.


Ninakumbuka siku moja tulipokuwa kanisani tunajifundisha darasa la biblia nilimuuliza askofu kuhusu shaka yangu kuhusu Yesu kuwa ni Mungu na pia niliwauliza mapadri tofauti lakini wote walinijibu unatakiwa kuamini tu, na mpaka hapa nilikuwa sijasilimu lakini nilikuwa ninaamini kuwa Mwenyeezi Mungu ni mmoja na Mtume Mohammad (swala llahu alayhi wasalam) ni Mtume wa mwenyeezi Mungu.


Wakati nilipokuwa shuleni, nilikutana na wanafunzi wawili ambao ni ndugu walikuwa ni Waislamu. Nilizungumza nao lakini kwa bahati mbaya hawakujuwa kuwa mimi nilikuwa ninataka kusilimu. Kukutana nao kwao hakukuleta faida yoyote ile. Nilijihisi katika nafsi yangu kuwa mimi ni mfuasi wa dini zote, kwani nimesoma vitabu vya dini zote. nilivutiwa kidogo na dini ya kiyahudi kwani nilihisi inafanana na dini ya Kiislamu kidogo.


Baada ya miaka miwili nilijiunga na kampuni ya sasa. Katika kampuni hiyo kulikuwa na kijana mmoja tulikuwa tukifanya kazi pamoja. Mvulana huyu alikuwa muislamu lakini alikuwa analewa wala haswali na nilikuwa daima ninamuuliza kwa nini hufuati maamrisho ya dini? alikuwa hanijibu kitu. baada ya mwaka toka kuanza kufanya kazi nikamueleza kuhusu haja yangu ya kutaka kuwa muislamu.


Siku moja tukaenda katika kituo cha Kiislamu cha kitaifa. Kulikuwa hakuna mtu anayehusika na maswala ya uongozi ila mtu mmoja ambaye alituambia subirini hapo baada ya muda atakuja imaam kuswalisha swala ya isha. Lakini nikahisi uzito nikaondoka. Baada ya wiki nne nikajaribu tena kwenda kwa mara hii nikaitamka shahada mbele ya Imaam na kuwa muislamu. Na tokea hapo nikajifundisha kuswali jambo ambalo nilikuwa nishajifundisha kabla ya kusilimu kwangu, kwa kupitia internet na video, pia nikajaribu kujifundisha lugha ya kiarabu kwani nilitamani siku moja kujuwa kuisoma Quran kwa lugha ya Kiarabu. Lakini nilishangazwa kwa muda mfupi niliweza kujuwa kuisoma Quran ingawa lafidhu yangu si nzuri.


Tarehe 8 October 2001 ni siku nzuri kuliko zote katika maisha yangu kwani ndio siku ambayo niliamua kuvaa hijabu kwa mara ya kwanza. Watu wengi kazini waliniuliza je umesilimu? nikawajibu ndio na wengi walishangaa kwa msichana wa kimarekani ambaye ni msomi mwenye nywele za blond na macho ya bluu kusilimu. Waliniambia kuwa mwanamke wa Kiislamu anadhalilishwa nikawajibu kuwa Quran imempa haki mwanamke wa Kiislamu kuliko Biblia na hili ni miongoni mwa jambo muhimu ambalo limenifanya kuingia katika Uislamu.


Na mwisho nasema kwamba ninaamini kuwa hapana Mola apaswae kuabudiwa kwa haki ispokuwa Mwenyeezi Mungu Mtukufu na Mtume Muhammad (swala llahu alayhi wasalam) ni Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu.


Makala hii kwa Ihsani ya Tovuti ya Jamii Islam

0 Comments