DUA BAADA YA KILA SALA YA FARADHI.

Allah Mtukufu ametuhimiza sana hasa sisi Waislamu kumuomba dua, kwasababu sisi binadamu ni dhaifu kwa mambo mengi na kwahiyo tunamhitajia Mola na wala Mola hatuhitajii sisi. Na sharti moja ya kukubaliwa dua yetu ni baada ya Sala za faridha. Ikiwa Mtume alikuwa akiomba dua katika kila baada ya Sala, na alikuwa akiwahimiza Masahaba wake kufanya hivyo. Basi jee sisi tusiokuwa Mitume ni binadamu wa kawaida tu hatuhitajii dua? Mtume ametufunza dua nyingi ambazo zimekuja katika Hadithi mbalimbali na yeye mwenyewe alikuwa akiziomba kama ifuatavyo:

1-Kutokana na Thaubaan Radhi  za allah ziwe juu yake amesema katika Hadithi iliyotolewa na Wanavyuoni wote ila L-Bukhari, "

"Alikuwa Mtume baada ya kumaliza Sala anastaghfiru (anaomba msamaha kwa kusema "Astaghfiru Llah") mara 3 kisha anasema,”
 
 
اللهم أنت السلام ومنك السلام تباركت ياذا الجلال والإكرام
.


ALLAHUMMA ANTA SSALAAMU WA MINKA SSALAAMU TABAARAKTA YA DHAL JALAALI WAL IKRAAM.
Maana yake, “Ewe Mwenyezi Mungu! Wewe ndiye Mwenye Salama, na Kwako iko Salama, umetukuka. Ewe Mola Mwenye utukufu na wema wote.”
2-Kutokana na Mughiyra bin Shu`ubah Radhi za Allaah ziwe juu yake amesema katika Hadithi iliyotolewa na L-Bukhari na Muslim, "“Alikuwa Mtume akisema kila baada ya Sala za faridha, "لا إله إلا الله وحده لا شريك له له الملك وله الحمد وهو على كل

شيء قدير اللهم لا مانع لما أعطيت ولا معطي لما منعت و لا ينفع ذا الجد منك الجد.LA ILAHA ILLA LLAHU WAHDAHU LA SHARIYKA LAHU, LAHUL MULKU WA LAHUL HAMDU WA HUWA ALAA KULLI SHAY`IN QADIYR. ALLAHUMMA LA MAANI`A LIMA AA`TAYTA WALA MU`UTI LIMA MANA`ATA WALA YANFAU DHAL JADDI MINKAL JADD.Maana yake, “Hakuna Mungu anayepaswa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah hana mshirika na Ndiye Mwenye Ufalme na Mwenye kustahiki shukrani zote; Naye ana uwezo wa kila kitu. Ewe Mwenyezi Mungu! Hakuna anayeweza kuzuia uliempa na hakuna anayeweza kumpa uliye mzuwilia, na haimfai mtu juhudi yake isipokuwa kwa uwezo Wako.” (Yaani juhudi haishindi kudra).


3-Kutokana na Muadh bin Jabal Radhi za allaah ziwe juu yake amesema katika Hadithi iliyotolewa na Ahmad na Abu Daud, "


"Siku moja Mtume alinishika mkono na akaniambia, "Ewe Muadh! Mimi nakupenda.” Na mimi nikamjibu, “Mimi pia nakupenda." Akasema, "Nakuusia ewe Muadh! Usiache kusema kila baada ya Sala, "


اللهم أعني على ذكرك وشكرك وحسن عبادتك.ALLAHUMMA A`INNIY `ALAA DHIKRIKA WA SHUKRIKA WA HUSNI `IBAADATIK."
Maana yake, "Ewe Mwenyezi Mungu nisaidie niweze kukukumbuka na kukushukuru na niweze kukuabudu vizuri."
4-Kutokana na Abi Umamah Radhi za Allaah ziwe juu yake kasema katika Hadithi iliyotolewa na Ahmad na Abu Daud Mtume kasema, "

“Mwenye kusoma Aayatul Kursiy kila baada ya Sala (ya faridha) hakuna kitu chochote kile kitakachomzuia kuingia Peponi isipokuwa kufikwa na mauti."


5-Kutokana na Uqbah bin `Aamur Radhi za allaah ziwe juu yake kasema katika Hadithi iliyotolewa na Ahmad na Abu Daud, ""Mtume aliniamrisha kusoma Muawwidhaatin baada ya kila Sala.” (Suratul Falaq na Suratun Nas).6-Kutokana na Abu Huraira Radhi za allaah ziwe juu yake kasema katika Hadithi iliyotolewa na L-Bukhari na Muslim na Abu Daud na Ahmad Mtume kasema" 
 
"Atakayesabbih katika kila Sala mara 33 (Kumtakasia kwa kumsifu kwa kusema, "Subhanallah") na atakaye Hammid mara 33 (Kumshukuru kwa kusema, "AL-Hamdu Lillah") na atakaye Kabbir mara 33 (Kumtukuza kwa kusema, "Allahu Akbar") na mwishowe akasema, "Laa Ilaaha Illa Llahu, Wahdahu La Shariika Lahu, Lahul Mulku Walahu Hamdu, Wa Huwa Alaa Kulli Shay-in Qadiyr."Maana yae, "Hakuna Mwenyezi Mungu anayestahiki kuabudiwa kwa haki ila Allah. Yeye ni peke Yake hana Mshirika yeyote yule. Ufalme wote ni Wake na shukrani zote ni Zake, na Ana uweza wa kila kitu. Basi mtu akisema hivi anafutiwa madhambi yake hata kama ni mengi kama mapovu ya bahari."


7-Kutokana na Muslim bin Haarith kutoka kwa baba yake kasema katika Hadithi iliyotolewa na Muslim na Ahmad na Abu Daud na L-Bukhari, "Kaniambia Mtume , "


“Utakaposali Asubuhi useme kabla hujazungumza na mtu yeyote yule: Allahumma Ajjirni Mina Nnaar mara 7 na ukifa mchana wa siku hiyo Mwenyezi Mungu anakuepusha na Moto.”Na utakaposali Magharibi useme kabla hujaongea na mtu yeyote yule: Allahumma Inniy As-alukal Jannah, Allahumma Ajjirni Mina Nnaar.""Ewe Mwenyezi Mungu! Mimi nakuomba Pepo. Ewe Mwenyezi Mungu! Nikinge na adhabu ya Moto."

Na ikiwa utakufa usiku huo, basi Mwenyezi Mungu anakuepusha na adhabu ya Moto.

0 Comments