Dua ya Swalatul-Istikhara (Swala ya kuomba
ushauri kutoka kwa Allah)
ushauri kutoka kwa Allah)
Amesema Jaabir Bin Abdillah رضى الله عنه “alikuwa
Mtume wa Mwenyezi Mungu akitufundisha Swala ya
Istikhara kama vile anavyotufunza sura ya
Qur’an. Anasema صلى الله عليه وسلم ‘Akikusudia mmoja
wenu kufanya jambo, aswali rakaa mbili zisizo za
faradhi, kisha aseme:
اللّهُـمَّ إِنِّـي أَسْتَخيـرُكَ بِعِاْـمِك، وَأسْتَقْـدِرُكَ بِقُـدْرَتِـك، وَأَسْـألُـكَ مِنْ فَضْـلِكَ العَظـيم،
فَإِنَّـكَ تَقْـدِرُ وَلا أَقْـدِر، وَتَـعْلَـمُ وَلا أَعْلَـم، وَأَنْـتَ عَلاّمُ الغُـيوب، اللّهُـمَّ إِنْ كُنْـتَ
تَعْـلَمُ أَنَّ هـذا الأمْـرَ (وَيُسَـمِّي حاجته) خَـيْرٌ لي في دينـي وَمَعـاشي وَعاقِـبَةِ
أَمْـري، ( عَاجِلِهِ و آجِلِه) فَاقْـدُرْهُ لي وَيَسِّـرْهُ لي ثـمَّ بارِكْ لي فيـه، وَإِنْ كُنْـتَ
تَعْـلَمُ أَنَّ هـذا الأمْـرَ شَـرٌ لي في دينـي وَمَعـاشي وَعاقِـبَةِ أَمْـري، ( عَاجِلِهِ و
آجِلِه) فَاصْرِفْـهُ عَنّيِ وَاصْرِفْني عَنْـهُ وَاقْـدُرْ ليَ الخَـيْرَ حَيْـثُ كانَ ثُـمَّ أَرْضِـني
بِِـه .
“Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi nakutaka ushauri
(muelekezo) kwa ujuzi Wako, na nakuomba uniwezeshe kwa
uwezo Wako, na nakuomba fadhila Zako kubwa, hakika Wewe
unaweza, nami siwezi, nawe unajua nami sijui, nawe nimjuzi wa
yale yaliyofichikana. Ewe Mwenyezi Mungu iwapo jambo hili
kutokana na ujuzi wako (utalitaja jambo lako) lina kheri na mimi
katika dini yangu na maisha yangu na mwisho wa jambo langu
(karibu na mbali ) basi nakuomba uniwezeshe nilipate, na
unifanyie wepesi, kisha unibariki, na iwapo unajua
kwamba jambo hili ni shari kangu katika dini yangu namaisha
yangu na mwisho wa jambo langu (karibu na mbali) basi
liepushe na mimi naminiepushe nalo, na nipangie jambo
jengine lenye kheri nami popote lilipo, kisha niridhishe kwalo”
Post a Comment