HUKMU YA MUZIKI KWA MUJIBU WA QURAN NA SUNNAH

Hukmu Ya Muziki Katika Qur-aan Na Sunnah

Ewe Upendaye Nyimbo Na Muziki, Haujafika Wakati Wa Kuogopa Adhabu Kali Za Allaah?
Muziki ni haraam kutokana na dalili dhahiri tulizopewa katika Qur-aan na Hadiyth za Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).
Baadhi ya watu katika Jamii yetu bado hawajatambua uharamu wa jambo hili, tunasikia wengi bado wanaimba taarabu au miziki mbalimbali, na mara kwa mara unapomnasihi nduguyo Muislamu kuacha maasi haya, jibu mara nyingi huwa: "Tena nyinyi mmezidi! Wapi inasema kuwa nyimbo haramu" Au wengine waliobobea katika maradhi haya hunena: "Mimi yote naweza kuacha lakini nyimbo utaniua", husema hivyo bila ya kujali amri ya makatazo ya Mola Mtukufu ambaye ni Muweza wa kuyaua masikio yake awe kiziwi na asiweze kusikia tena hizo nyimbo.


Inafika hadi Muislam hawezi kulala hadi alazwe kwa muziki, hawezi kula ila muziki uwe unapigwa, hawezi kufanya kazi za nyumbani bila muziki kufunguliwa, hawezi mtu kutembea bila kuwa na walkman au mp3 yake ikicheza muziki, hawezi kufanya kazi akiwa kazini…hawezi kusafiri…hawezi hata kufanya mazoezi ya ndani bila kuwepo na muziki wa kumchochea na kumtia hamasa (kama wanavyoitakidi) ya lile analolifanya kwa wakati huo! ‘Alaa kulli haal, muziki umekuwa ni sehemu kiungo kikubwa cha maisha ya mwanaadam kwa wakati huu!
Hivyo tumeona kuna umuhimu mkubwa wa kuwakumbusha ndugu zetu waepukane na haramu hii ili wajiokoe na ghadabu za Mola Mtukufu, ghadhabu kali ambazo zinafika kumgeuza mtu awe nyani au nguruwe kama tutakavyosoma katika hizi dalili za wazi wazi zenye uhakika.


Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) katika suuratu Luqmaan:
(( ﻭَﻣِﻦَ ﺍﻟﻨَّﺎﺱِ ﻣَﻦ ﻳَﺸْﺘَﺮِﻱ ﻟَﻬْﻮَ ﺍﻟْﺤَﺪِﻳﺚِ ﻟِﻴُﻀِﻞَّ ﻋَﻦ ﺳَﺒِﻴﻞِ ﺍﻟﻠَّﻪِ ﺑِﻐَﻴْﺮِ ﻋِﻠْﻢٍ ﻭَﻳَﺘَّﺨِﺬَﻫَﺎ ﻫُﺰُﻭًﺍ ﺃُﻭﻟَﺌِﻚَ ﻟَﻬُﻢْ ﻋَﺬَﺍﺏٌ ﻣُّﻬِﻴﻦٌ ))
((Na miongoni mwa watu wapo wanaonunua maneno ya upuuzi, ili wawapoteze watu na njia ya Mwenyezi Mungu pasipo kujua, na wanaichukulia ni maskhara. Hao watapata adhabu ya kuwafedhehesha)) [Luqmaan: 6]
Ibn Mas'uud (Radhiya Allaahu 'anhu) amesema kuhusu Aayah hii "Naapa kwa Allaah hii inamaanisha ni kuimba (nyimbo na miziki)" [At-Twabariy 20:127]
ﻭﻋﻦ ﺍﺑﻦ ﻋﺒﺎﺱ ﻗﺎﻝ ﻋﻦ ﺁﻳﺔ : )) ﻭﻣﻦ ﺍﻟﻨﺎﺱ ﻣﻦ ﻳﺸﺘﺮﻱ ﻟﻬﻮ ﺍﻟﺤﺪﻳﺚ (( ، ﻗﺎﻝ : ﺍﻟﻐﻨﺎﺀ ﻭﺃﺷﺒﺎﻫﻪ ﺇﺳﻨﺎﺩﻩ ﺻﺤﻴﺢ - ﺍﻟﻤﺤﺪﺙ : ﺍﻷﻟﺒﺎﻧﻲ
Na Ibn 'Abbaas (Radhiya Allaahu 'anhuma) pia amesema kuhusu Aayah hii : ((Na miongoni mwa watu wapo wanaonunua maneno ya upuuzi)) "Ni nyimbo na maneno ya yanayofanana (ya upuuzi)" [Isnaad Sahiyh kutoka kwa Shaykh Al-Albaaniy]


GHADHABU ZA ALLAAH KUWAANGAMIZA WAFANYAO MAASI HAYA (YA KUSIKILIZA NYIMBO NA MIZIKI

 
Vile vile ghadhabu za Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) ni kali mno za kuangamizwa pindi maasi haya yatakapodhihirika.


ﻋﻦ ﻋﻤﺮ ﺑﻦ ﺣﺼﻴﻞ ﻋﻦ ﺭﺳﻮﻝ ﺍﻟﻠﻪ ﺻﻠﻰ ﺍﻟﻠﻪ ﻋﻠﻴﻪ ﻭﺳﻠﻢ ﺍﻧﻪ ﻗﺎﻝ : )) ﻳﻜﻮﻥ ﻓﻰ ﺍﻣﺘﻰ ﻗﺬﻑ ﻭﻣﺴﺦ ﻭﺧﺴﻒ :(( ﻗﻴﻞ ﻳﺎﺭﺳﻮﻝ ﺍﻟﻠﻪ ﻭﻣﺘﻰ ﺫﻟﻚ ﻗﺎﻝ : )) ﺍﺫﺍ ﻇﻬﺮﺕ ﺍﻟﻤﻌﺎﺯﻑ … (( ﺍﺧﺮﺟﻪ ﺍﻟﺘﺮﻣﺬﻯ ﻭﺻﺤﺤﻪ ﺍﻟﻌﻼﻣﻪ ﺍﻻﻟﺒﺎﻧﻰ
 

Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kasema: ((Kutatokea katika Ummah huu maafa ya kuteremshiwa mawe kutoka mbinguni, kugeuzwa maumbile ya binaadamu [kugeuzwa kufanywa nyani na nguruwe] na mididimizo [ya ardhi]. Ikaulizwa: Ewe Mjumbe wa Allaah, lini yatatokea hayo? Akasema: ((Itakapodhihirika miziki … ))
[At-Trimidhy na ameipa daraja ya Sahiyh Shaykh Al-Albaaniy]
 

TUSIKILIZE NA KUSOMA QUR-AAN
Muziki na nyimbo humjaza mtu mapenzi makubwa moyoni, zimshughulishe zaidi hadi asiwe na muda wa kusoma maneno ya Mola wake Mtukufu ambayo hiyo ndio inayopasa kuifanya iwe midomoni na moyoni mwetu daima kwa kusoma kwa sauti nzuri ya kupendeza (Tajwiyd) kama tulivyoamrishwa na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).


SAUTI ZA NYIMBO (NA MIZIKI) ZIMELAANIWA DUNIANI NA AKHERA
ﻗﺎﻝ ﺭﺳﻮﻝ ﺍﻟﻠﻪ ﺻﻠﻰ ﺍﻟﻠﻪ ﻋﻠﻴﻪ ﻭﺳﻠﻢ : )) ﺻﻮﺗﺎﻥ ﻣﻠﻌﻮﻧﺎﻥ ﻓﻰ ﺍﻟﺪﻧﻴﺎ ﻭﺍﻻﺧﺮﻩ ﻣﺰﻣﺎﺭ ﻋﻨﺪ ﻧﻌﻤﻪ ﻭﺭﻧﻪ ﻋﻨﺪ ﻣﺼﻴﺒﻪ )) ﺍﻟﺒﺰﺍﺭ ﻭ ﺻﺤﺤﻪ ﺍﻟﻌﻼﻣﻪ ﺍﻻﻟﺒﺎﻧﻰ
Na kasema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Sauti mbili maluuni [zilizolaaniwa] duniani na Akhera; mizumari katika furaha na kuombeleza katika misiba)) [Al-Baazaar – na Shaykh Al-Albaaniy kaipa daraja ya Sahiyh]


NI SUNNAH KUZIBA MASIKIO UNAPOSIKIA MUZIKI BILA YA KUTAKA
ﻋﻦ ﻧﺎﻓﻊ ﺃﻧﻪ ﻗﺎﻝ : ﺳﻤﻊ ﺍﺑﻦ ﻋﻤﺮ ﻣﺰﻣﺎﺭﺍ، ﻗﺎﻝ : ﻓﻮﺿﻊ ﺃﺻﺒﻌﻴﻪ ﻋﻠﻰ ﺃﺫﻧﻴﻪ، ﻭﻧﺄﻯ ﻋﻦ ﺍﻟﻄﺮﻳﻖ، ﻭﻗﺎﻝ ﻟﻲ : ﻳﺎ ﻧﺎﻓﻊ ﻫﻞ ﺗﺴﻤﻊ ﺷﻴﺌﺎ؟ ﻗﺎﻝ : ﻓﻘﻠﺖ : ﻻ ! ﻗﺎﻝ : ﻓﺮﻓﻊ ﺃﺻﺒﻌﻴﻪ ﻣﻦ ﺃﺫﻧﻴﻪ، ﻭﻗﺎﻝ : ﻛﻨﺖ ﻣﻊ ﺍﻟﻨﺒﻲ ﺻﻠﻰ ﺍﻟﻠﻪ ﻋﻠﻴﻪ ﻭﺳﻠﻢ، ﻓﺴﻤﻊ ﻣﺜﻞ ﻫﺬﺍ ! ﻓﺼﻨﻊ ﻣﺜﻞ ﻫﺬﺍ - ﺣﺪﻳﺚ ﺻﺤﻴﺢ، ﺻﺤﻴﺢ ﺃﺑﻲ ﺩﺍﻭﻭﺩ ﻭﺭﺍﺟﻊ ﺍﻟﺴﻠﺴﻠﺔ ﺍﻟﺼﺤﻴﺤﺔ ﻟﻸﻟﺒﺎﻧﻲ
 

Kutoka kwa Naafi'i ambaye amesema, amesikia sauti ya muziki akaziba masikio yake kwa vidole vyake, kisha akamgeuza mnyama wake aliyempanda [arudi asiendelee kwenda sehemu hiyo iliyokuwa na muziki] akasema: "Ewe Naafi'i, umesikia kitu?" Akasema, nikajibu: "Hapana". Akaondosha vidole vyake masikioni mwake akasema: "[siku moja] Nilikuwa na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliposikia kama hivi [muziki] akafanya kama hivi [nilivyofanya mimi yaani kuziba masikio yake asisikie sauti ya mizumari] [Hadityh Swahiyh ya Abu Daawuud na Ikiwa katika Silsilatus-Swahiyha ya Shaykh Al-Albaaniy]

ﻭﻗﺎﻝ ﺭﺳﻮﻝ ﺍﻟﻠﻪ ﺻﻠﻰ ﺍﻟﻠﻪ ﻋﻠﻴﻪ ﻭﺳﻠﻢ : )) ﻟﻴﻜﻮﻧﻦ ﻣﻦ ﺃﻣﺘﻲ ﺃﻗﻮﺍﻡ ﻳﺴﺘﺤﻠﻮﻥ ﺍﻟﺤﺮ ﻭ ﺍﻟﺤﺮﻳﺮ ﻭ ﺍﻟﺨﻤﺮ ﻭ ﺍﻟﻤﻌﺎﺯﻑ، ﻭ ﻟﻴﻨﺰﻟﻦ ﺃﻗﻮﺍﻡ ﺇﻟﻰ ﺟﻨﺐ ﻋﻠﻢ، ﻳﺮﻭﺡ ﻋﻠﻴﻬﻢ ﺑﺴﺎﺭﺣﺔ ﻟﻬﻢ، ﻳﺄﺗﻴﻬﻢ ﻟﺤﺎﺟﺔ، ﻓﻴﻘﻮﻟﻮﻥ : ﺍﺭﺟﻊ ﺇﻟﻴﻨﺎ ﻏﺪﺍ، ﻓﻴﺒﻴﺘﻬﻢ ﺍﻟﻠﻪ، ﻭﻳﻀﻊ ﺍﻟﻌﻠﻢ، ﻭﻳﻤﺴﺦ ﺁﺧﺮﻳﻦ ﻗﺮﺩﺓ ﻭﺧﻨﺎﺯﻳﺮ ﺇﻟﻰ ﻳﻮﻡ ﺍﻟﻘﻴﺎﻣﺔ )) ﺭﻭﺍﻩ ﺍﻟﺒﺨﺎﺭﻱ
 

Na akasema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Watakuweko watu katika Ummah wangu watakaojaribu kuhalilisha zinaa, uvaaji wa hariri, pombe na muziki. Baadhi ya watu watakuwa pembeni mwa mlima na mchungaji wao atawajia jioni na kuwaomba haja [fulani]. Watasema: "Rudi kesho". Allaah Atawaangamiza usiku, Atawaangushia milima kisha Atawabadilisha waliobakia wawe nyani na nguruwe na watabakia hivyo hadi siku ya Qiyaamah))[Al-Bukhaariy]
Hadiyth hii inatuthibitishia kuwa madhambi yote hayo yako sawa sawa uharamu wake, kama vile zinaa na pombe ilivyo haramu, basi na muziki pia haramu sawa sawa. Sasa vipi Muislamu aone kuwa muziki sio maasi makubwa ya kujiepusha nayo?
Imaam Abu Haniyfah amesema: "Kuimba (nyimbo, ngoma) ni katika madhambi makubwa ambayo inatakiwa Muislamu kujiepusha nayo haraka"
Khofu zaidi imuingie Muislamu kuwa anaweza kupata adhabu ya kugeuzwa nyani au nguruwe kwa maasi haya kama tulivyoonywa katika Hadiyth ifuatayo:


ﻭﻗﺎﻝ ﺭﺳﻮﻝ ﺍﻟﻠﻪ ﺻﻠﻰ ﺍﻟﻠﻪ ﻋﻠﻴﻪ ﻭﺳﻠﻢ : )) ﻟﻴﺸﺮﺑﻦ ﺃﻗﻮﺍﻡ ﻣﻦ ﺃﻣﺘﻲ ﺍﻟﺨﻤﺮ ﻳﺴﻤﻮﻧﻬﺎ ﺑﻐﻴﺮ ﺍﺳﻤﻬﺎ ﻳﻌﺰﻑ ﻋﻠﻰ ﺭﺅﻭﺳﻬﻢ ﺑﺎﻟﻤﻌﺎﺯﻑ ﻭﺍﻟﻤﻐﻨﻴﺎﺕ ، ﻳﺨﺴﻒ ﺍﻟﻠﻪ ﺑﻬﻢ ﺍﻷﺭﺽ ﻭﻳﺠﻌﻞ ﻣﻨﻬﻢ ﻗﺮﺩﺓ ﻭﺧﻨﺎﺯﻳﺮ )) ﻗﺎﻝ ﺍﻟﺸﻴﺦ ﺍﻷﻟﺒﺎﻧﻲ - ﺭﺣﻤﻪ ﺍﻟﻠﻪ ﺗﻌﺎﻟﻰ - : ﺻﺤﻴﺢ
 

Na kasema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Watu katika Ummah wangu watakunywa pombe wakiipa jina jengine lisilokuwa hilo, miziki itapigwa kwa ajili yao na watakuweko waimbaji wanawake. Allaah Atawadidimiza ardhini na Atawageuza wawe nyani na nguruwe)) [Ibn Maajah na Shaykh Al-Albaaniy ameipa daraja ya Sahiyh]


ﻧﺴﺄﻝ ﺍﻟﻠﻪ ﺍﻟﻌﺎﻓﻴﺔ ﻭﺍﻟﺴﻼﻣﺔ

Tunamuomba allaah azilainishe nyoyo zetu tuwe ni wenye kusikia na kutii

0 Comments