JINSI YA KUPIKA PILAU YA NYAMA NA MTINDI

VIPIMO
 
Nyama iliyokatwa vipande                                       1 Ratili(LB)
Mchele Basmati                                                       2 Magi
Chumvi ya wali                                                        kiasi
Kitungu kilichokatwa katwa                                      1 kikubwa
Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi              1 kijiko cha supu  
Mtindi (yogurt)                                                       ½ kikombe
Mchanganyiko wa bizari ya pilau ya tayari                2 vijiko vya supu (Shan pilau biriani spice mix)
Mafuta kidogo yakukaangia
Rangi ya manjano (ukipenda)
 
 NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
 
1.    Osha mchele na roweka nusu saa .
2.    Weka mafuta katika sufuria na kaanga vitungu mpaka viwe rangi ya hudhurungi (brown).
3.    Tia thomu na tangawizi na ukaange kidogo.
4.    Kisha weka bizari ya pilau halafu nyama huku unakaanga hadi nyama isiwe nyekundu tena.
5.    Tia maji gilasi 1½ - 2 ichemke mpaka nyama iwive na karibu kukauka.
6.    Mimina mtindi na iachie moto mdogo ikauke kidogo.
7.    Kwenye sufuria nyingine chemsha mchele pamoja na chumvi na mafuta kidogo mpaka uive.
8.    Mimina wali juu ya nyama, kisha nyunyiza rangi (ukipenda) kama vile wali wa biriani na ufunike kwa dakika kumi hivi.
9.    Changanya  wali na nyama pamoja ikiwa tayari kuliwa.

0 Comments