JINSI YA KUPIKA SAMBUSA ZA VIAZI


Vipimo

Viazi                                                                          4Vitunguu nyasi vilokatwakatwa                                    3 micheKitunguu maji kilokatwakatwa                                     1Chumvi                                                                     1 kijiko cha chaiBizari ya pilau nzima ( jeera)                                      1 kijiko cha chaiMafuta                                                                       Nusu kiloManda za tayari                                                         10 - 20                                Yai                                                                            1 au 2Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Menya viazi, vioshe vikate slesi kisha  vikatekate vipande vidogo vidogo.


   

Chemsha maji kidogo ukiwa umeyatia chumvi , kisha vimimine viazi ndani ya maji yawache paka uwone tena yachemka kwa mara ya pili acha kwa dakika 10 - 15, kisha ondoa jikoni.

Mimina katika chujio uchuje maji .Roweka bizari kwenye maji kwa muda wa dakika 20 hivi.

Chukua bakuli kubwa lenye nafasi mimina viazi, vtunguu nyasi na maji,   chumvi, mafuta vijiko 2 – 3 vya supu, na bizari. Changanya vizuri.
Tandaza manda mezani au kwenye kibao fanya mkunjo wa sambusa kisha paka yai kwa brashi, kunja upate pembe moja . Tazama picha.

 Jaza viazi sehemu ulokunja kisha funga sambusa.
Tia mafuta katika karai, yakipata moto, tia sambusa ziikaange hadi zigeuke rangi ya dhahabu.  
Zitoe na zichuje mafuta tayari kuliwa

0 Comments