KUFUNGA SIKU YA ARAFA:

Usipitwe na funga ya Arafa kesho siku ya jumapili.
Siku ya arafa ni siku ya tisa ya mwezi wa Dhul hijjah,siku ambayo mahujaji wanakuwa wamesimama katika viwanja vya arafa.
Kwa yule ambaye hakushiriki katika ibaada hii ya hijjah ni suna kwake kufunga siku hii.


Mwaka huu funga hii imedondokea siku ya jumapili,
ambayo ni tarehe 9/Dhul Hijjah/1437
Inayo afikiana na tarehe 11/9/2016

DALILI YA KUFUNGA SIKU HII NA FADHILA ZAKE:
Kapokea imamu Tirmidhiy hadithi iliyo simuliwa na Abu Katada-Radhi za Allah ziwe juu yake-anasema:
رُوِيَ الْامَامِ الْتِّرْمِذِيُّ عَنْ أَبِيْ قَتَادَةَ الْأَنْصَارِيِّ رَضِيَ الْلَّهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُوْلَ الْلَّهِ سُئِلَ عَنْ صَوْمِ يَوْمِ عَرَفَةَ ، فَقَالَ : (يَكْفُرْ الْسَّنَةَ الْمَاضِيَةَ وَالْسَّنَةَ الْقَابِلَةِ)
Mtume (rehma na amani ziwe juu yake) aliulizwa juu ya funga ya siku ya arafa akajibu: (Inafuta madhambi ya mwaka ulio pita na mwaka ujao)

Madhambi haya yanayo futwa na ibada hii na mfano wake,
Ni madhambi madogo madogo,ama madhambi makubwa,
Kama vile:Shirki,uchawi,uzinzi,kuto watendea wema wazazi wawili N.K 


madhambi haya huitaji toba maalumu.

0 Comments