MADHARA YA ZINAA KISAYANSI


Wengi katika wanadamu wanajaribu kuhoji kwa nini Mwenyezi Mungu anakataza zinaa wakati kuingiliana baina ya mke na mume na kuingiliana baina ya hawara na hawara mambo ni yale yale, sasa kwa nini akataze??? Kwanza ifahamike kwamba Mwenyezi Mungu akikataza jambo basi ujue lina hasara kwetu kwa kulifuata na lina faida kubwa kama tukiliacha. Tofauti na wanadamu, kwa mfano; Serikali inakataza pombe ya Gongo kwa madai kuwa ni haramu wakati Bia pia ni pombe lakini ni halali! Hiyo ni kwa mujibu wa serikali za ulimwengu. Lakini katika UISLAMU Mwenyezi Mungu akisema pombe ni haramu basi iwe Gongo,Bia,n.k zote ni HARAMU. Ndivyo pia ilivyo ZINAA, leo ulimwenguni kuna zinaa ya halali wenyewe wanaita “zinaa salama ya kutumia Condom” lakini uislamu umeharamisha kabisa zinaa, iwe ya Condom au bila Condom huo ndio uislamu na ndiyo amri za Mwenyezi Mungu.

Mwenyezi Mungu anasema katika Qur’an, sura ya 17 Bani Israil aya ya 32;

“Na wala msiikaribie ZINAA, hakika ya hiyo zinaa ni uchafu na njia mbaya”

Hapo Mwenyezi Mungu amekataza Zinaa, tena amesema hiyo zinaa ni uchafu. Haya ni maneno aliyosema Mwenyezi katika karne ya saba (7). Je? Watu wa kanuni za maumbile wanakubaliana kwamba ndani ya zinaa kuna uchafu? Na kama upo ni upi? Hatuwezi kuujua uchafu wa zinaa mpaka tutazame katika mafundisho ya wanasayansi wa sasa yaani MODERN SCIENTISTS ili tujue wamekubaliana vipi na Qur’an bila wenyewe kujua. 

Wakati tunatafuta kujua uchafu wa zinaa na madhara yake kisayansi lazima kwanza tujue vitu vikuu vine:
(1) Uchafu ni nini?
(2) Manii yanatoka wapi kwa mwanaume.
(3) Manii yanatoka wapi kwa mwanamke.
(4) Na ndani ya manii mna nini.


Tunapozungumzia uchafu kwa tafsiri ya jumla ni kitu kilichowekwa mahala pasipostahili. Mfano; kuchukua kiatu chenye thamani ya laki moja ukakanyaga matope kisha kiatu kile ukakiweka juu ya kitanda cha kawaida na godoro la sufi ambacho thamani yake kwa ujumla havifiki elfu arobaini; lakini pamoja na thamani ya kiatu kuwa kubwa kuliko kitanda na godoro mtu akija atauliza huu uchafu aliyeweka hapa juu ya kitanda ni nani? Kwa nini aite kiatu cha gharama uchafu? Ni kwamba kimekaa pahala pasipostahili. Hivyo kitendo cha mwanaume au mwanamke kupokea au kupeleka manii yake pahala pasipokuwa halali yake huo ni uchafu.

Kwa upande wa mwanaume tunapozungumzia utoaji wake wa manii ni mfinyo wa glands(tezi) za aina tano; ambao mfinyo huu unapatikana baada ya mwanaume kupata stimulation(msisimko) na hapo ndipo tezi hizi hujibinya na kutoa maji ya aina tano tofauti yanayokutana katika makende na kuchukua mbegu kisha yanatoka katika hali na rangi ambayo wengi tunaifahamu. Glands hizi za mwanaume zimefungwa baina ya kifua na mgogo.


Kwa mwanamke manii yake yanatoka katika Glands za aina mbili tu ambazo hizi zimefungwa katika kifua chake. Hivyo maji haya yanayotoka katika glands hizi mbili yakichanganyika na ya mwanaume jumla yanakuwa maji ya aina saba (7) yakikaa katika pahala panapokusudiwa kwa mwanamke na kwa muda maalum hapo ndipo inapopatikana mimba na kizazi cha binadamu kinaendelea.


Baada ya kujua hatua ya mwanzo yanapotokea manii sasa tuingie katika hatua ya pili ya kujua je? Ndani ya manii mna kitu gani kitaalamu. Ndani ya manii mna vitu vikuu vine:
• PROTEIN
• ACID
• SPERM/CHROMOSOME
• VIRUS


PROTEIN: Ni aina mojawapo ya “Food Substance” inayorutubisha mwili. Substance hii inapatikana ndani ya manii na pia watu wa mambo ya reproduction system (mfumo wa uzazi) wanakubali kwamba manii yanatokana na aina hii ya chakula na ndiyo maana kama una njaa shughuli ya Jimai inashindikana, au kama utajilazimisha utapata madhara.

ACID: Ni mfano wa tindikali, yaani kitu chenye ladha ya ukali mfano ndimu. Na kitu chenye tindikali kina kawaida ya kuunguza na pia kulegeza kwa itakayompata au kumuingia, ndiyo sababu kitaalam ukimlinganisha mwanamke aliyeolewa na asiyeolewa kisha akawa hafanyi zinaa maumbile yao yanatofautiana. Yule aliyeolewa mwili wake unakuwa laini zaidi sababu ya acid inayopatikana ndani ya manii. Nitakupa mifano mingi iliyo hai ili akili yako ikubali kwamba vyote vinavyotajwa vinapatikana ndani ya manii. Ukitaka kuthibitisha zaidi acid ya katika manii ambayo inaunguza nakulegeza hata ukiwa na kidonda kibichi ukitia manii kitauma mara mbili zaidi sababu ya acid. Mfano mwingine tazama kwa wale watoto wa kiume ambao wanaingiliwa kinyume na maumbile (mashoga) hata kama zamani alikuwa strong (imara) kiasi gani akiingiliwa tu, basi analegea kuanzia kutembea, kuzungumza na kila kitu sababu ni Acid inayopatikana ndani ya manii. Pia ndio maana inakatazwa kumuingilia mwanamke anayenyonyesha sababu ukimuingilia ukamuingizia manii ambayo yana acid, acid ile itapanda katika maziwa na kuyaharibu maziwa na hapo mtoto akinyonya atanyonya maziwa yenye acid. Itasababisha mtoto kulegea au kwa watu wa pwani wanaita kubemendwa, hivyo mtakua mmemharibu mtoto. Lakini kama atakula acid ya baba yake hatadhurika sana, sababu atakula acid ambayo kwa asili ndiyo iliyomtengeneza. Ila mkeo akiziniwa na mtu mwingine mtoto ataathirika sana na pengine itakuwa ni sababu ya kifo chake kwa kuwa amekula acid ambayo si ya asili kutoka kwa wazazi wake hivyo itakuwa ni POISON (sumu) kwake. Kazi kubwa ya acid kwenye manii ni kuua bacteria zisizohusika zinazopatikana wakati zikitoka kuelekea katika virginal wall.

SPERM: Ni mbegu za kiume zinazopatikana ndani ya manii na hizi mbegu haziishi ndani ya mwili kwa sababu ya hali ya joto la mwili, kwani mtu wa kawaida ambaye haumwi anakuwa na nyuzi joto 37 hivyo mbegu zitakufa kutokana na joto la ziada. Wataalamu wa mambo ya reproduction na gynecology wanatueleza kwamba mshindo mmoja una wastani wa watoto milioni 200 hadi 300. Lakini yanayofanikiwa kulifikia yai ni mia moja tu. Na yanayofanikiwa kuingia kwa kawaida ni moja au mawili yakizidi sana manne tu, na si zaidi ya hapo, lau kama yakizidi basi ni kwa miujiza yake Mwenyezi Mungu.

VIRUS: Hivi ni vijidudu ambavyo kila mtu anavyo vya kwake na pia haviingiliani baina ya mtu na mtu na hapa ndipo tutaeleza kwa kina madhara ya zinaa kisayansi. Lazima pia tujue kuwa Virus wanafanya kazi gani na pia wanakwenda wapi. Katika virginal wall kuna vijistomata (vitundu) maalum kwa ajili ya kupokea virus; sababu mwanaume anapotoa manii yake yenye protein,acid,sperm/chromosomes na virus kila kimoja huchukua nafasi yake kwenda kunapohusika. Nafasi ya virus ni kuingia katika vitundu vilivyo katika virginal wall ili vipate kuishi humo kwa kuwa ndipo alipowapangia Mwenyezi Mungu. Hivyo basi ukiwa unamuingilia mkeo na ukitoa manii basi moja kwa moja virus wako watakwenda kuingia katika vijitundu vilivyo kwenye virginal wall ili kuishi humo. Ina maana virus watakaoingia kuishi kwa mkeo ni wale ambao wamezoeana. Sasa ikija kutokea mkeo akazini na mwanaume mwingine ataingiziwa virus wasiokuwa wako. Hivyo hawa wapya wakiingia nao pia watataka kuingia katika yale matundu ili nao wakaishi. Kwa kuwa ndivyo alivyowapangia Mwenyezi Mungu, hawa wapya wakiingia tu wale wa zamani ambao ni wa mume, watawashangaa, watajiuliza hawa nao wametokea wapi? Mbona si katika wale tuliozoeana? Kwa kushangaa huku wale virus wenyeji watawashambulia virus wageni kama antibody bacteria (kitu kinachotoka nje ya mwili). Na katika mapigano haya watapelekea kundi moja kufa na kundi moja likifa lazima wale waliokufa watoke, watatoka vipi? Au watatokea wapi? Jibu ni pale pale walipoingilia. Hapo sasa ndipo mtu anapoanza kutokwa uchafu. Na pia virus wapya waliosalimika wakiona wanazidi kushambuliwa na virus wa zamani itabidi watoboe sehemu nyingine zisizohusika ili wakimbie na kujificha katika nyama laini.

Hapo ndipo mtu anapoanza kupata maumivu makali wakati wa kukojoa na pia ndio chanzo cha magonjwa mbalimbali ya zinaa, na wakati huo mume akimuingilia mkewe naye pia atapata ugonjwa wa zinaa sababu atakutana na virus wageni waliojificha kujihami katika sehemu laini zisizohusika watamuingia mume kupitia mrija wa urinary truck (mrija wa mkojo). Ndio sababu Mwenyezi Mungu akasema zinaa ni uchafu. Na uchafu unaokusudiwa ni kuchanganya mifumo tofauti ya mwili yaani mwanamke kuingiliwa na mwanaume zaidi ya mumewe pekee. Na hapa ndipo tunapoona hekima ya Mwenyezi Mungu kwamba kwa nini ameamrisha mwanamke kuolewa na mwanaume mmoja na mwanaume kuoa mwanamke zaidi ya mmoja. Hii ni kwa sababu mwanamke anapokea manii yenye kubeba VIRUS wa asili kutoka kwa mumewe. Hapa ndipo inapopatikana hekima ya  mwanamke aliyefiwa na mumewe au aleyeachwa kwa talaka lazima akae eda. Eda si tu kuangalia kama mwanamke ana mimba, bali pia katika kipindi cha miezi mine na siku kumi ambacho mwanamke anakaa eda kwa kuwa katika kipindi hicho haingiliwi ina maana wale virus watakosa protein inayopatikana katika manii ambayo ndio chakula chao, hivyo kwa kukosa chakula watakufa. Kwa hiyo katika kipindi hicho mwanamke anaandaliwa ili kama ataolewa tena na mume mwingine huyu mume mpya ajitengenezee mifumo yake mipya ambayo haitapingana na ile ya mwanzo. Hivyo Mwenyezi Mungu alipokataza ZINAA anajua kwa kina madhara yake.


Ndio sababu twasema kwamba sera bora za kupambana na magonjwa mbalimbali ya zinaa kama UKIMWI n.k dunia nzima ni kufuata UISLAM tu hakuna la zaidi. Hivyo tunapenda watu walifahamu hilo na kulifanyia kazi kwa kuwa UISLAM siyo ugaidi wala si dini ya vurugu bali ni dini ya AMANI ambayo inaweza kumfaa mtu kimwili na kiroho. Tunatoa wito kwa watu ulimwenguni kote kumuamini Mwenyezi Mungu wa kweli na Mtume wake wa karne ya sayansi na teknolojia Nabii Muhammad (Rehema na amani ziwe juu yake) ili kupata nusra ya mitihani mizito na majanga yanayotukumba wanadamu hivi sasa.

0 Comments