SWALI:
Shukurani zote zina mustahiki Allah subhanahu wataalla!
Swali langu nikuhusu muislam kuingiya kanisani, nasi kama
anapenda ila hulazimusha na mahala anapo fanya kazi kwakushindikiza awo
wasiye jiweza kwa sababu ana pasha kuwalisha. Na ayo mambo yote niliyo
yauliza ninalazimika kuyafanya katika programme ya shule niliyo
ichanguwa, ambayo niya u nurse, na mimi napenda sana kusomeya iyo kazi, ila tatizo ni hiyo. Tashukuru sana mukinisahidiya. Ahsante, Maasalam
JIBU:
Sifa
zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote,
Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu
‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu kwa swali lako kuhusu kuingia katika Kanisa.
Hakika
Uislamu haujamkataza Muislamu kuingia katika Kanisa ikiwa kuna udhuru
wa kufanya hivyo. Ikiwa ni kujua wanayofanya Wakristo ili uwe na
maalumati ya moja kwa moja kuhusiana na ‘Ibaadah zao au kwa shughuli
nyingine kama msaada wa Waislamu kuwasaidia masikini waliokumbwa na
misukosuko na wakapata hifadhi katika Kanisa.
Hata hivyo, si vyema kwa Muislamu kuingia katika chuo chochote kile kama
ni cha unesi au chengineko kukawa na utaratibu wa programu wa chuo kwa
wanafunzi kulazimishwa kuingia huko. Kufanya hivyo vyuo hivyo ni kwa
malengo ya kuwavuta Waislamu na kuwatoa katika Dini yao. Hivyo, ni vyema kwako kutafuta chuo ambacho haitakuwa na ulazima huo wa kuingia makanisani.
Tunaamini
kuna vyuo vingi Ulaya ambavyo havina mambo ambayo umeyataja hayo kwa
sharti la kuwa nesi. Hatujui vyuo vyote vinginevyo umeviacha na kuingia
hicho chenye masharti kama hayo kwanini?
Hivyo
tunakushauri ndugu yetu, uepukane na mambo ya haraam na mashaka mashaka
katika Dini yako na utafute yale yenye usalama na Dini yako na kupata
radhi za Allaah ambalo ndilo lengo kuu la kuwepo kwako hapa ulimwenguni.
Post a Comment