(Pamoja Na Ayyaamut-Tashriyq; 11, 12, 13)
Inatupasa
tumshukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa neema Aliyotujaalia ya
kutuwekea miezi mitukufu, au siku tukufu au nyakati tukufu ambazo ‘amali
njema huwa na thawabu nyingi mno. Na hivi tunakaribia kabisa kuingia
katika mwezi mwingine mtukufu wa Dhul-Hijjah. Katika mwezi huu, siku
kumi za mwanzo ni siku bora kabisa mbele ya Allaah ambazo 'amali yoyote
inayotendwa humo ni yenye kupendwa mno na Allaah:
عن
ابن عباس رضي الله عنهما، أن النبي صلى الله عليه وسلم قال: ((مَا مِنْ
أَيَّامٍ الْعَمَلُ الصَّالِحُ فِيهَا أَحَبُّ إِلَى اللَّهِ مِنْ هَذِهِ
الْأَيَّامِ)) يَعْنِي أَيَّامَ الْعَشْرِ قَاُوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ
وَلَا الْجِهَادُ فِي سَبِيلِ اللَّهِ؟ قَالَ: ((وَلَا الْجِهَادُ فِي
سَبِيلِ اللَّهِ إِلَّا رَجُلٌ خَرَجَ بِنَفْسِهِ وَمَالِهِ فَلَمْ
يَرْجِعْ مِنْ ذَلِكَ بِشَيْ)) البخاري
Ibn
'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) ameahadithia kwamba Nabiy (Swalla
Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Hakuna siku ambazo ‘amali
njema zinazotendwa humo, zinapendwa mno na Allaah kama (‘amali
zinazotendwa katika) siku kumi hizi.” Yaani: Siku kumi za mwanzo wa
mwezi wa Dhul-Hijjah. Wakauliza: Ee Rasuli wa Allaah! Je, hata kuliko
jihaad katika njia ya Allaah? Akajibu: “Hata Jihaad katika njia ya
Allaah isipokuwa mtu aliyekwenda na nafsi yake na mali yake ikawa hakurudi na kimojawapo.” [Al-Bukhaariy]
Zifuatazo
ni fadhila kuu za masiku hayo kumi ya Dhul-Hijjah. Ee ndugu Muislamu!
Utakapojipwekesha katika 'ibaadah na kutenda ‘amali njema zenye ikhlaasw
na zinazotokana na mafunzo sahihi ya Sunnah za Nabiy (Swalla Allaahu
‘alayhi wa aalihi wa sallam), basi bila shaka utajichumia thawabu
maradufu na ambazo zitakuwa nzito In Shaa Allaah katika mizani yako.
-Allaah Ameziapia Siku Kumi Hizi:
Kwa
jinsi zilivyokuwa na umuhimu mkubwa siku hizo kumi, hadi kwamba Allaah
(Subhaanah wa Ta'aalaa) Ameziapia katika Qur-aan Anaposema:
بِسْمِ اللّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ ((وَالْفَجْرِ)) ((وَلَيَالٍ عَشْرٍ))
Kwa Jina la Allaah, Mwingi wa rahmah, Mwenye kurehemu. ((Naapa kwa Alfajiri)) ((Na kwa masiku kumi)) [Al-Fajr: 1-2]
Wanachuoni wafasiri wa Qur-aan wamekubaliana kwamba zilokusudiwa hapo ni siku kumi za Dhul-Hijjah.
-Siku Za Manufaa Na Kumdhukuru Allaah:
Inapasa kumdhukuru mno Allaah (Subhaanah wa Ta’alaa) kwa kukumbuka neema Zake zisizohesabika:
((لِيَشْهَدُوا مَنَافِعَ لَهُمْ وَيَذْكُرُوا اسْمَ اللَّهِ فِي أَيَّامٍ مَّعْلُومَاتٍ))
((Ili washuhudie manufaa yao na kulitaja Jina la Allaah katika siku zinazojulikana)) [Al-Hajj: 28]
Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kasema: “Hizo
ni siku kumi za Dhul-Hijjah.” Na Amesema: “Manufaa ya dunia hii na ya
Aakhirah.” Manufaa ya Aakhirah yanajumuisha kupata radhi za Allaah.
Manufaa ya vitu vya dunia inajumuisha wanyama wa kuchinjwa na biashara. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
-'Amali Zake Ni Bora Kuliko Kwenda Katika Jihaad Fiy SabiliLLaah:
Kutokana
na ilivyotajwa katika usimulizi wa Hadiyth ifuatayo, kwamba amali
yoyote utendayo katika masiku kumi hayo, ni bora kuliko kwenda kupigana
jihaad vitani. Ukizingatia kwenda kupigana jihaad ni jambo zito mtu
kuliitikia, kwani huko kuna mashaka mbali mbali, ikiwemo kupoteza mali,
khofu ya kujeruhiwa na kupoteza viungo vya mwili, kufariki, n.k. Ila
hilo si zito kwa mwenye iymaan ya hali ya juu kabisa kutaka kuyakabili
mashaka hayo na kutamani kufa shahidi. Kwa hiyo usidharau ‘amali yoyote
hata iwe ndogo vipi itekeleze kwani Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) ni
Al-Jawwaad (Mwingi wa Ukarimu), Al-Kariym (Mkarimu), Al-Wahhaab (Mwingi
wa kutunuku, Mpaji wa yote), Al-Majiyd (Mwingi mno wa vipawa na
ukarimu).
عن
ابن عباس رضي الله عنهما، أن النبي صلى الله عليه وسلم قال: ((مَا مِنْ
أَيَّامٍ الْعَمَلُ الصَّالِحُ فِيهَا أَحَبُّ إِلَى اللَّهِ مِنْ هَذِهِ
الْأَيَّامِ)) يَعْنِي أَيَّامَ الْعَشْرِ قَاُوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ
وَلَا الْجِهَادُ فِي سَبِيلِ اللَّهِ؟ قَالَ: ((وَلَا الْجِهَادُ فِي
سَبِيلِ اللَّهِ إِلَّا رَجُلٌ خَرَجَ بِنَفْسِهِ وَمَالِهِ فَلَمْ
يَرْجِعْ مِنْ ذَلِكَ بِشَيْ)) البخاري
Ibn
'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) ameahadithia kwamba Nabiy (Swalla
Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Hakuna siku ambazo ‘amali
njema zinazotendwa humo, zinapendwa mno na Allaah kama (‘amali
zinazotendwa katika) siku kumi hizi.” Yaani: Siku kumi za mwanzo wa
mwezi wa Dhul-Hijjah. Wakauliza: Yaa Rasula-Allaah! Je hata kuliko
jihaad katika njia ya Allaah? Akajibu: “Hata Jihaad katika njia ya
Allaah isipokuwa mtu aliyekwenda na nafsi yake na mali yake ikawa hakurudi na kimojawapo.” [Al-Bukhaariy]
-'Ibaadah Zote Zimejumuika Katika Siku Hizi
'Ibaadah
zote zimejumuika katika siku kumi hizi nazo ni Swalaah, kufunga
Swiyaam, Swadaqah, Hajj, wala hazijumuiki pamoja wakati mwingine.
-‘Amali Za Kutenda Katika Siku Kumi Hizi:
1- Kutekeleza Hajj na 'Umrah (kwa mwenye uwezo):
عَنْ
أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم
قَالَ: ((العُمْرَةُ إِلَى العُمْرَةِ كَفَّارَةٌ لِمَا بَيْنَهُمَا،
وَالحَجُّ الـمَبْرُورُ لَيْسَ لَهُ جَزَاءٌ إِلَّا الجَنَّةُ))
Abuu
Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah
(Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kasema: “'Umrah hadi 'Umrah
hufuta (madhambi) baina yake, na Hajjum-Mabruwr haina jazaa ila Jannah)
[Al-Bukhaariy na Muslim]
عن
أبي هريرة رضي الله عنه قال: "سئل رسول الله صلى الله عليه وسلم: أي
الأعمال أفضل؟ قال: ((إيمان بالله ورسـوله)). قيل: ثم مـاذا؟ قال: ((الجهاد
في سبيل الله)) قيل: ثم ماذا؟ قال: ((حج مبـرور)) متفق علية
Abuu
Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba aliulizwa Rasuli
wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ‘Amali gani ni
bora kabisa? Akasema: “Kumuamini Allaah na Rasuli Wake.” Akaulizwa:
Kisha nini? Akasema: “Jihaad katika njia ya Allaah.” Akaulizwa: Kisha
nini? Akasema: “Hajj Mabruwr.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
2- Kuomba Tawbah ya kweli na kujiepusha na maasi:
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
(( يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا تُوبُوا إِلَى اللَّهِ تَوْبَةً نَّصُوحًا))
((Enyi mlioamini! Tubuni kwa Allaah tawbah iliyo ya kweli!)) [At-Tahriym: 8]
Na
Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametupa matumaini
makubwa ya kufutiwa madhambi na makosa yetu katika usimulizi ufuatao:
عن
أَنَسُ بْنُ مَالِكٍ قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ
عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: ((قَالَ اللَّهُ تَبَارَكَ وَتَعَالَى يَا
ابْنَ آدَمَ، إِنَّكَ مَا دَعَوْتَنِي وَرَجَوْتَنِي غَفَرْتُ لَكَ عَلَى مَا كَانَ فِيكَ وَلَا أُبَالِي، يَا ابْنَ آدَمَ لَوْ بَلَغَتْ ذُنُوبُكَ عَنَانَ السَّمَاءِ ثُمَّ اسْتَغْفَرْتَنِي غَفَرْتُ لَكَ وَلَا أُبَالِي،
يَا ابْنَ آدَمَ إِنَّكَ لَوْ أَتَيْتَنِي بِقُرَابِ الْأَرْضِ خَطَايَا
ثُمَّ لَقِيتَنِي لَا تُشْرِكُ بِي شَيْئًا لَأَتَيْتُكَ بِقُرَابِهَا
مَغْفِرَةً))
Anas
(Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba: Nimemsikia Rasuli wa
Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Allaah
(Tabaaraka wa Ta’aalaa) Amesema: Ee bin-Aadam! Hakika ukiniomba na
ukanitaraji (kwa malipo) Nitakughufuria yale yote uliyonayo na wala
Sijali, Ee bin-Aadam! Lau zingefikia dhambi zako ukubwa wa mbingu, kisha
ukaniomba maghfirah, Ningekughufuria bila ya kujali (kiasi cha madhambi
uliyoyafanya). Ee bin-Aadam! Hakika ungenijia na madhambi yakaribiayo
ukubwa wa ardhi, kisha ukakutana nami na hali hukunishirikisha chochote,
basi Nami Nitakujia na maghfirah yanayolinga nayo.” [At-Tirmidhiy na Shaykh Al-Albaaniy kaipa daraja ya Hasan]
3-Kumdhukuru Mno Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
Kwa Tasbiyh, Tahmiyd, Tahliyl, Takbiyr: Maana yake ni: kusema: Subhaana Allaah, AlhamduliLLaah, laa Ilaaha illa Allaah, Allaahu Akbar.
عن
ابْنِ عُمَرَ عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَال: ((
مَا مِنْ أَيَّامٍ أَعْظَمُ عِنْدَ اللَّهِ وَلَا أَحَبُّ إِلَيْهِ مِنَ
الْعَمَلِ فِيهِنَّ مِنْ هَذِهِ الْأَيَّامِ الْعَشْرِ، فَأَكْثِرُوا
فِيهِنَّ مِنَ التَّهْلِيلِ وَالتَّكْبِيرِ وَالتَّحْمِيدِ )) أخرجه أحمد
Ibn
'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amehadithia kwamba Nabiy (Swalla
Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Hakuna siku zilizokuwa
tukufu kwa Allaah na zilizokuwa ‘amali vyake vipenzi kabisa Kwake kama
siku hizi, basi zidisheni Tahliyl na Takbiyr na Tahmiyd.” [Ahmad]
Inavyopasa kufanya Takbiyr:
اللَّهُ أَكْبَرُ، اللَّهُ أَكْبَرُ، لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ، اللَّهُ أَكْبَرُ، اللَّهُ أَكْبَرُ، وَلِلَّهِ الْحَمْد
Allaahu Akbar, Allaahu Akbar, laa Ilaaha illa Allaah, Allaahu Akbar Allaahu Akbar WaliLLaahil-Hamd
Takbiyr hii ni aina mbili:
Takbiyratul-Mutwlaq - Za Nyakati Zote:
Takbiyr
wakati wote usiku au mchana tokea Magharibi unapoingia tu mwezi wa
Dhul-Hijjah na inaendelea mpaka siku ya mwisho ya Tashriyq (tarehe 13
Dhul-Hijjah) inapoingia Magharibi.
Takbiyratul-Muqayyad - Za Nyakati Maalum:
Takbiyr kuanzia Alfajiri ya siku ya 'Arafah mpaka inapoingia Magharibi ya siku ya mwisho ya Tashriyq.
4- Kufufua Sunnah ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
Wanaume
wanatakiwa waseme kwa sauti ili kuwakumbusha wengine na wanawake waseme
kimya kimya isipokuwa wakiwa na mahaarim wao. Kufufua Sunnah ya Nabiy
(Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni
muhimu kwa sababu bila ya kufanya hivyo ni kukosa fadhila zake, na pia
ni kupoteza Sunnah za kipenzi chetu Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa
aalihi wa sallam).
مَنْ
سَنَّ فِي الْإِسْلَامِ سُنَّةً حَسَنَةً فَعُمِلَ بِهَا بَعْدَهُ كُتِبَ
لَهُ مِثْلُ أَجْرِ مَنْ عَمِلَ بِهَا ، وَلَا يَنْقُصُ مِنْ أُجُورِهِمْ
شَيْءٌ .
Nabiy
(Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kasema: “Atakayetenda
kitendo kizuri (Sunnatun-Hasanah) katika Uislaam kisha nacho kikafuatwa
kutendwa, ataandikiwa mfano wa ujira wa yule atakayekitenda baada
yake bila ya kupungukiwa thawabu zao.” [Muslim]
كَانَ
إبْن عَمَر وَأبُو هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّه عَنْهُما يَخْرُجَانِ إِلَى
السُّوقِ فِي أَيَّامِ العَشْرِ يُكَبِّرَانِ، وَيُكَبِّرُ النَّاسُ
بِتَكْبِيرِهِمَا .
Ibn
'Umar na Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) walikuwa wakienda
sokoni katika siku kumi (za Dhul-Hijjah) na kutamka Takbiyr kwa sauti na
watu wakiwaigiza. [Al-Bukhaariy]
5- Kufunga Swiyaam siku hizi khaswa siku ya 'Arafah:
Kufunga Swiyaam siku hii ni kufutiwa madhambi ya miaka miwili:
عَنْ
أَبِي قَتَادَةَ رضي الله عنه أن النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ
وَسَلَّمَ قَالَ: ((صِيَامُ يَوْمِ عَرَفَةَ أَحْتَسِبُ عَلَى اللَّهِ أَنْ
يُكَفِّرَ السَّنَةَ الَّتِي قَبْلَهُ وَالسَّنَةَ الَّتِي بَعْدَهُ )) أخرجه مسلم
Abuu Qataadah (Radhwiya
Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa
aalihi wa sallam) kasema: “Swawm ya 'Arafah nataraji (kwa Allaah) kufuta
madhambi ya mwaka uliopita na wa baada yake.” [Muslim]
Swawm inamweka mtu mbali na Moto.
عَنْ
أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ رضي الله عنه قَالَ : قَالَ رَسُولُ اللَّهِ
صلى الله عليه وسلم : مَنْ صَامَ يَوْماً فِي سَبِيلِ اللَّهِ بَعَّدَ
اللَّهُ وَجْهَهُ عَنْ النَّارِ سَبْعِينَ خَرِيفًا.
Abuu
Sa'iyd Al-Khudhwriyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba Rasuli
wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
“Atakayefunga Swiyaam siku moja kwa ajili ya Allaah, Allaah Atauweka
uso wake mbali na moto masafa ya miaka sabiini.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
Na Swawm ina thawabu maradufu.
عنْ
أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ
صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((كُلُّ عَمَلِ ابْنِ آدَمَ يُضَاعَفُ
الْحَسَنَةُ عَشْرُ أَمْثَالِهَا إِلَى سَبْعمِائَة ضِعْفٍ قَالَ اللَّهُ
عَزَّ وَجَلَّ إِلَّا الصَّوْمَ فَإِنَّهُ لِي وَأَنَا أَجْزِي بِهِ يَدَعُ
شَهْوَتَهُ وَطَعَامَهُ مِنْ أَجْلِي لِلصَّائِمِ فَرْحَتَانِ فَرْحَةٌ
عِنْدَ فِطْرِهِ وَفَرْحَةٌ عِنْدَ لِقَاءِ رَبِّهِ وَلَخُلُوفُ فِيهِ
أَطْيَبُ عِنْدَ اللَّهِ مِنْ رِيحِ الْمِسْكِ))
Abuu
Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah
(Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): “Kila 'amali njema ya
mwanaadamu inalipwa mara kumi na inaongezewa thawabu kutoka kumi hadi
mia saba, na Allaah (‘Azza wa Jalla) Anasema: Isipokuwa Swawm, kwani
hiyo ni kwa ajili Yangu na Mimi Ndiye Nitakayemlipa. Ameacha matamanio
yake na chakula chake kwa ajili Yangu. Kwa aliyefunga Swawm atapata
furaha mbili; furaha anapofuturu na furaha atakapoonana na Rabb wake,
harufu inayotoka kinywani mwa aliyefunga ni nzuri mbele ya Allaah kuliko
harufu ya misk.” [Muslim na Ahmad]
6- Kuzidisha ‘amali njema mbali mbali:
Kuanzia
kuswali Swalaah za fardhi kwa wakati wake kisha kuswali Swalaah za
Sunnah, kusoma Qur-aan, kutoa swadaqah, kuomba du’aa kwa wingi, kutii
wazazi na kuwafanyia wema, kuwasiliana na jamaa (kuunga undugu),
kuwafanyia wema jirani, kuamrishana mema na kukatazana maovu, kufanyiana
wema na ihsani na kadhalika.
7- Kuchinja baada ya Swalaah ya 'Iyd:
Anasema Allaah (Subhaanahu Wa Ta'aalaa):
((فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ))
((Basi Swali kwa ajili ya Rabb wako na uchinje)) [Al-Kawthar: 2]
Na usimulizi ufuatao tunapata maelezo ya aina ya mnyama wa kuchinja na uchinjaji wake.
فعَنْ
أَنَسٍ رضي الله عنه قَالَ: ضَحَّى النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ
وَسَلَّمَ بِكَبْشَيْنِ أَمْلَحَيْنِ أَقْرَنَيْنِ ذَبَحَهُمَا بِيَدِهِ
وَسَمَّى وَكَبَّرَ وَوَضَعَ رِجْلَهُ عَلَى صِفَاحِهِمَا متفق عليه
Anas
(Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba: Nabiy (Swalla Allaahu
'alayhi wa aalihi wa sallam) alichinja kondoo wawili weupe* wenye pembe,
amewachinja kwa mikono yake, akasema BismiLLaah na Allaahu Akbar na
akaweka mguu wake upande wa nyuma yao. [Al-Bukhaariy na Muslim]
*Baadhi ya Wanachuoni wamesema kuwa ni weupe ulio na alama nyeusi, wengine wamesema uliochanganyika na wekundu.
‘Amali
hii ya kuchinja ni 'ibaadah tukufu na ni Sunnah iliyosisitizwa hata
wanachuoni wameona kuwa ni waajib kwa kila aliyekuwa na uwezo wa
kuchinja.
Yanayompasa kufanya mwenye kutaka kuchinja:
Baada
ya kutia niyyah ya kuchinja, asikate mtu nywele wala kucha mpaka
amalize kuchinja kama tulivyoamrishwa katika Hadiyth ifuatayo:
عن
أم سلمة رضي الله عنها، أن النبي صلى الله عليه وسلم قال: (((ِذَا
رَأَيْتُمْ هِلَالَ ذِي الْحِجَّةِ وَأَرَادَ أَحَدُكُمْ أَنْ يُضَحِّيَ ،
فَلْيُمْسِكْ عَنْ شَعْرِهِ وَأَظْفَارِهِ))) وفي راوية: ((فَلَا يَأْخُذْ
مِنْ شَعْرِهِ وَلَا مِنْ أَظْفَارِهِ شَيْئًا، حَتَّى يُضَحِّيَ)) مسلم
Ummu
Salamah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) amehadithia kwamba Nabiy (Swalla
Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Mtakapoona mwezi
umeandama wa Dhul-Hijjah na ikiwa yuko anayetaka kuchinja basi azuie
(asikate) nywele zake na kucha zake).” [Muslim na wengineo] Na katika riwaayah nyengine: "Asikate nywele wala kucha mpaka akimaliza kuchinja."
Hii
ni fadhila na neema kwetu maana tunakuwa kama vile tumo katika ihraam
ndogo kama vile wanavyokuwa Mahujaji katika ihraam zao, ingawa ihraam
zao zimeshurutishwa kwa kuharamishwa mambo mengineyo. Ikiwa amesahau
mtu, mfano akakata kucha basi aendelee tu na niyyah yake mpaka amalize
kuchinja.
8- Kuhudhuria Swalaah ya 'Iyd:
Kwenda
kuswali Swalaah ya ‘Iyd ni jambo lilosisitizwa mno na Nabiy (Swalla
Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Lakini Waislaam wengi wamepuuza
‘amali hii na hali Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)
amehimiza mpaka wanawake walio katika hedhi na wazee waende kusikiliza
khutbah ya Swalaah. Wakati wa Swalah ukifika, wanawake hao wenye hedhi
wajitenge kando hadi itakapomalizika Swalaah na kisha wajiunge na wenzao
kusikiliza khutbah.
9-‘Amali za Kutenda Siku Ya ‘Arafah Ambayo Ni Siku Ya Tisa Dhul-Hijjah
a) Mwenye kufunga Swawm, atafutiwa madhambi ya miaka miwili!
Siku hii tukufu ni siku iliyokamilika Dini yetu. Thawabu za kufunga siku hii ni kufutiwa madhambi ya miaka miwili.
عَنْ
أَبِي قَتَادَةَ رضي الله عنه أن النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ
وَسَلَّمَ قَالَ: ((صِيَامُ يَوْمِ عَرَفَةَ أَحْتَسِبُ عَلَى اللَّهِ أَنْ
يُكَفِّرَ السَّنَةَ الَّتِي قَبْلَهُ وَالسَّنَةَ الَّتِي بَعْدَهُ )) أخرجه مسلم
Abuu
Qataadah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba Nabiy (Swalla
Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Swawm ya 'Arafah,
nataraji kwa Allaah kuwa afute madhambi ya mwaka uliopita na wa baada
yake.” [Muslim]
b) Siku ambayo huachiliwa watu wengi huru kutokana na moto
عَنْ
عَائِشَةَ (رضي الله عنها) أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ
عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((مَا عَمِلَ آدَمِيٌّ مِنْ عَمَلٍ يَوْمَ
النَّحْرِ أَحَبَّ إِلَى اللَّهِ مِنْ إِهْرَاقِ الدَّمِ, إِنَّهَا
لَتَأْتِي يَوْمَ الْقِيَامَةِ بِقُرُونِهَا, وَأَشْعَارِهَا,
وَأَظْلَافِهَا وَأَنَّ الدَّمَ لَيَقَعُ مِنْ اللَّهِ بِمَكَانٍ قَبْلَ
أَنْ يَقَعَ مِنْ الْأَرْضِ فَطِيبُوا بِهَا نَفْسًا))
Mama wa Waumini, 'Aaishah
(Radhwiya Allaahu 'anhaa) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla
Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Hakuna
kitendo cha bin Aadam kilichokuwa ni kipenzi kabisa kwa Allaah siku ya
kuchinja kama kumwaga damu. Atakuja (huyo mnyama) siku ya Qiyaamah na
pembe zake, kucha zake na nywele zake. Damu yake itamwagika
mahali fulani Allaah Anapajua kabla ya kumwagika katika ardhi.
Hivyo zipendezesheni nafsi kwayo.” [At-Tirmidhiy, Sunan Ibn Maajah]
Na alipoulizwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
مَا
هَذِهِ الْأَضَاحِيُّ؟ قَالَ: ((سُنَّةُ أَبِيكُمْ إِبْرَاهِيمَ))
قَالُوا: فَمَا لَنَا فِيهَا يَا رَسُولَ اللَّهِ؟ قَالَ: ((بِكُلِّ
شَعَرَةٍ حَسَنَةٌ)) قَالُوا: فَالصُّوفُ يَا رَسُولَ اللَّهِ؟ قَالَ:
((بِكُلِّ شَعَرَةٍ مِنْ الصُّوفِ حَسَنَةٌ))
Nini hivi vichinjo?
Akajibu: “Ni Sunnah ya baba yenu Ibraahiym.”. Wakasema, "Nini umuhimu
wake kwetu?” Akasema: “Katika kila unywele kuna jema moja.” Wakasema: Na
sufi? Akasema: “Katika kila unywele wa sufi kuna jema moja.” [Ahmad, Ibn Maajah]
c) Du'aa bora kabisa ni Du'aa katika siku ya 'Arafah
Inapasa kumdhukuru mno Allaah siku hii kama alivyosema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa:
((خَيْرُ
الدُّعَاءِ دُعَاءُ يَوْمِ عَرَفَةَ، وخَيْرُ مَا قُلْتُ أنَا
وَالنَّبيُّونَ مِنْ قَبْـلِي: لَا إِلَهَ إِلاَّ اللهُ وَحْدَهُ لا
شَرِيْكَ لَهُ، لَهُ الـمُلْكُ، ولَهُ الـحَمْدُ، وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيءٍ
قَدِير)) روى الترمذي
“Du’aa bora kabisa ni du’aa katika siku ya 'Arafah, na yaliyo bora kabisa niliyosema mimi na Manabii kabla yangu ni:
Laa Ilaaha illa Allaah Wahdahu laa shariyka Lahu, Lahul-Mulku Walahul-Hamdu wa Huwa 'alaa kulli shay-in Qadiyr. [At-Tirmidhiy]
10-Amali Za Kutenda Siku Ya Kuchinja Ambayo Ni Sikukuu Ya ‘Iyd
Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((إِنَّ أعظمَ الأيامِ عندَ اللهِ تباركَ وتعالى يومُ النَّحْرِ ، ثمَّ يَومُ القَّرِّ)) سنن أبي داود
“Siku iliyo tukufu kabisa kwa Allaah ni siku ya kuchinja, kisha siku ya kutulia.” (yaani siku ya kukaa Minaa) [Sunan Abi Daawuwd]
11-Amali Za Kutenda Ayyaamut-Tashriyq (Siku Za Tashriyq) 11, 12, 13
Ni
siku ya kumi na moja na kumi na mbili na kumi na tatu ya Dhul-Hijjah
yaani siku tatu baada ya siku ya 'Iyd. Na siku hizi tatu zimeitwa kuwa
ni siku za tashriyq kwa sababu watu walikuwa wakikatakata nyama na
kuzianika juani. Na pi siku hizi hujulikana kwa 'siku za Minaa'.
a) Kumdhukuru mno Allaah
Katika siku hizi inampasa Muislamu azidishe kumdhukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kama Anavyosema:
((وَاذْكُرُواْ اللّهَ فِي أَيَّامٍ مَّعْدُودَاتٍ)
((Na mdhukuruni Allaah katika siku za kuhesabika.)) [Al-Baqarah: 203]
Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema: Siku za kuhesabika ni siku za tashriyq (11, 12, 13 Dhul-Hijjah) na siku zinazojulikana ni siku za kumi za mwanzo za Dhul-Hijjah. [Al-Qurtwubiy: 3.3]
b) Haifai kufunga Swawm katika siku za tashriyq.
Haifai
kufunga katika siku za tashriyq hata kama mtu alikuwa na mazowea ya
kufunga Swiyaam za Sunnah kama vile Jumatatu, Alkhamiys au Ayyaamul-Biydhw. Dalili ni makatazo katika Hadiyth ifuatayo:
عن أبي هريرة أَنَّ
رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بَعَثَ عَبْدَ اللَّهِ
بْنَ حُذَافَةَ يَطُوفُ فِي مِنًى أَنْ: ((لَا تَصُومُوا هَذِهِ
الْأَيَّامَ فَإِنَّهَا أَيَّامُ أَكْلٍ وَشُرْبٍ وَذِكْرِ اللَّهِ عَزَّ
وَجَلَّ))
Abuu
Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah
(Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimtuma 'Abdullaah bin
Hudhaafah azunguke Minaa na atangaze: "Msifunge siku hizi, kwani hizi ni
siku za kula na kunywa na kumdhukuru Allaah ‘Azza wa Jalla.” [At-Twabariy 4: 211]
Tunamuomba
Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Atupe umri na afya na uwezo wa kuweza
kutekeleza ‘amali nyingi zenye kumridhisha katika siku hizi tukufu na
Atuwezeshe pia katika masiku yote mengineyo, Atulipe thawabu nyingi na
Atujaaliye tuwe wenye kusikia na kufuata yaliyo mazuri. Aamiyn.
0 Comments