UJUMBE MZITO KWA WAISLAMU WOTE

Kila mmoja alikuwa ni chembe ya manii, Mola wetu Mlezi Akatupatia maumbo mazuri, tunayoringia na kuwa majeuri hutaki kumsujidia Mola wako Mlezi? Allaah {{سبحانه وتعالى}} Amekuumba akakusawazisha sawa kabisa na kukupa neema ya viungo mbali mbali unavyotumia kufanyia madhambi? Subhaana Llaah, wapi utaipata rehema za Allaah {{سبحانه وتعالى}}?

Basi kumbuka kuwa namna unavyomuasi Mola wako ndivyo uchungu wa kutolewa roho utakavyozidi. Je umewahi kufikiria uchungu wa maumivu wa mwanaadamu aliyechunwa ngozi yake, kisha akagaragizwa katika mchanga wa moto? Hiyo ndio hali ya kutolewa roho.

قال الله تعالى:
كَلَّا إِذَا بَلَغَتِ التَّرَاقِيَ﴿٢٦﴾ وَقِيلَ مَنْ ۜ رَاقٍ﴿٢٧﴾ وَظَنَّ أَنَّهُ الْفِرَاقُ﴿٢٨﴾ وَالْتَفَّتِ السَّاقُ بِالسَّاقِ﴿٢٩﴾ إِلَىٰ رَبِّكَ يَوْمَئِذٍ الْمَسَاقُ﴿٣٠﴾
La, hasha! {{Roho}} itakapofikia kwenye mafupa ya koo; Na pakasemwa: Nani wa kumganga? Na mwenyewe akajua kwa hakika kuwa huko ndiko kufariki; Na utapoambatishwa muundi kwa muundi; Siku hiyo ndiyo ya kuchungwa kupelekwa kwa Mola wako Mlezi!
{}Al-Qiyaamah: 26-30{}

Hiyo siku utamwita Mama/Baba... yuwapi kukusaidia? Unamwangalia Mkeo/Mumeo ... yuwapi kukuliwaza? Unamwita mwanao... yuwapi kukufadhili? Waite ndugu zako, rafiki, maraisi, mapolisi na wengineo, hakuna wa kukusaidia. Dakika zako za kuishi zimekwisha ndugu yangu. Pumzi na riziki zako zimeshafika tamati. Huna kitu tena. Leo ndio siku yako ambayo ulikuwa unaikimbia.

قال الله تعالى:
إِنَّ الْمَوْتَ الَّذِي تَفِرُّونَ مِنْهُ فَإِنَّهُ مُلَاقِيكُمْ ۖ ثُمَّ تُرَدُّونَ إِلَىٰ عَالِمِ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ
“Hakika {{hayo}} mauti mnayoyakimbia, hakika ni yenye kukuteni tu! Kisha mtarudishwa kwa Mjuzi wa siri na dhahiri. Atakujulisheni kwa yale mliyokuwa mkiyatenda.
{}Al-Jumua'h: 8{}

Na hiyo ni Ahadi ya Allaah {{سبحانه وتعالى}} itafika kwani ahadi za Allaah {{سبحانه وتعالى}} ni kweli.
Wapi basi unakimbilia ewe ndugu yangu Muislamu? Hiyo ndio nyumba yako ya muda ukisubiri kufufuliwa kwenda kuhisabiwa. Hakuna kwengine isipokuwa ni Moto ama Pepo. Motoni ndimo wengi wa viumbe watamalizikia.

Ya Allaah tunaomba hifadhi ya siku hii nzito

0 Comments