بسم الله الرحمن الرحيم
Hapa chini tutaona hoja au madai tata za wanaotetea kuburuza/ kuburura nguo na majibu dhidi ya madai hayo.
Hoja Mojawapo:
Kuwa Isbaal Inawahusu Wenye Kuvaa Kwa Kiburi Au Kwa Fakhari Tu
Baadhi
ya watu wanarukhusu Isbaal kwa kudai kuwa makatazo yaliyokuja katika
Hadiyth mbalimbali ni kwa wale tu wanaovaa kwa kiburi au kujifakharisha.
Ima kwa wale wanaovaa tu bila kukusudia kiburi basi inafaa na hakuna
ubaya wowote. Wakitoa hoja kwa kutumia baadhi ya Hadiyth, mojawapo ya
Hadiyth hizo ni Hadiyth maarufu ya kumhusu Abu Bakr (Radhiya Allaahu
kuwa nguo yake ilikuwa ikiburuza, ambayo Mtume ‘anhu) anasema:
“Mwenye
kuburuza nguo yake kwa kiburi, Allaah Hatomtazama siku ya Qiyaamah” Abu
Bakr akasema: Ee Mjumbe wa Allaah! Upande mmoja wa kikoi changu
unashuka hadi niuvute na kuuzuia, Mtume akamjibu: Wewe si mwenye kufanya
kwa kiburi” Imesimuliwa na al-Bukhaariy
Majibu Ya Hoja Hiyo:
Kwa
kujibu hoja yao ya kutegemea Hadiyth hiyo kuonyesha kuwa Abu Bakr
alikuwa akiburuza nguo yake, tunajibu kwa maneno ya Wanachuoni ambao
wameunganisha Hadiyth za pande zote kuhusiana na suala hilo na kuweka
ufahamu ulio sahihi:
1-
Ametaja Mwanachuoni Ibn Hajr kuwa, katika masimulizi ya Imaam
At-Tirmidhiy kuna ziada baada ya maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi
wa aalihi wa sallam):
“Atakayeburuza
nguo yake kwa fakhari (kiburi), Hatomtazama Allaah mtu huyo siku ya
Qiyaamah), akasema Ummu Salamah: Je, watafanyaje wanawake na mikia yao
(nguo zao zenye kuburuza)? Akasema (Mtume): Waongeze shibri (kiasi cha
kiganja kimoja), Akasema (Ummu Salamah): Hata hivyo bado miguu yao
itakuwa wazi. Akajibu (Mtume): Basi wazidishe dhiraa na si zaidi ya
hapo.”
Ibn
Hajar akasema: Alivyofahamu – yaani Ummu Salamah – ni kuwa makatazo ya
kuburuzwa kwa nguo makusudio yake ni kwa hali zote; iwe kwa kiburi au
bila kiburi. Ndipo alipomuuliza Mtume hukumu ya wanawake kuhusiana na
hilo kwa kuhitajia kwao kuburuza ili waweze kujistiri vizuri miguu yao
ili isiwe uchi… kisha akaendelea kusema Ibn Hajr katika uchambuzi wake:
Na Qaadhi ‘Iyaadhw amenukuu ‘Ijmaa’ (makubaliano) ya kuwa makatazo ya
Isbaal ni kwa wanaume na si wanawake, na makusudio yake ni kuwa
kukatazwa kwa Isbaal ni kwa kukariri kwake Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi
wa aalihi wa sallam) kwa Ummu Salamah ili kumfahamisha. Fat-hul Baariy
Mj. 10, uk. 259.
2- Na
akasema Ibn Hajr (Allaah Amrehemu): Ama Isbaal bila ya kiburi, ni wazi
kutokana na Hadiyth mbalimbali kuwa ni Haraam. Kisha akasema: Na ikiwa
nguo ni ndefu kuliko urefu wa mtu mwenyewe basi hiyo huenda ikapelekea
kwenye makatazo kwa ajili ya israfu na kufikia kwenye uharamu. Na
vilevile inapelekea makatazo kwa kufanana nako na mavazi ya wanawake, na
hii inawezekana zaidi kuliko sababu ya mwanzo. Na kadhalika ameeleza
Al-Haakim usahihi wa Hadiyth iliyopokelewa na Abu Hurayrah kuwa Mtume
(Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amemlaani mwanamme anayevaa
mavazi ya mwanamke. Vilevile yanapelekea makatazo ya Isbaal kwa mwenye
kuvaa kutosalimika na kupatwa vazi lake na najisi kwa upande mwengine.
Fat-hul Baariy Mj. 10, uk. 263.
3- Ibn
Al-‘Arabiy (Abu Bakr) naye kasema: Haijuzu kwa mwanamme kuachia nguo
yake kuvuka mafundo ya miguu, na akasema: Siburuzi kwa kiburi, kwa kuwa
makatazo yanaweza kuhusu hali hiyo kimatamshi, na wala haijuzu kwa
mwenye kuchukulia matamshi hayo ya makatazo kwa kiburi kuwa ndio hukumu
akasema: Mimi hukumu hiyo hainihusu kwa kuwa ‘ilah (sababu)
yake hainihusu. Hakika anayesema hivyo, ajue kuwa madai hayo
hayajasalimika, bali ni kuwa kurefusha nguo na kuvuka mafundo
kunaonyesha kiburi chake (huyo mwenye kurefusha). Fat-hul Baariy Mj.10,
uk. 264.
4-
Isbaal ni mwelekeo wa kiburi. Anasema Ibn Hajr (Allaah Amrehemu): Isbaal
inalazimu kuburuzika kwa nguo, na kuburuzika kwa nguo kunalazimu kiburi
japo ikiwa mwenye kuvaa hajakusudia kiburi. Na yanaungwa mkono maneno
yake hayo na aliyosimulia Ahmad bin Muniy’i kwa upande mwengine kutoka
kwa Ibn ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhuma) kutoka katika Hadiyth ambayo
inasema,
“Ole wako na kuburuza nguo (kuvuka mafundo ya miguu), kwani kuburuza nguo ni alama ya kiburi”. Fat-hul Baariy Mj.10, uk. 264.
5- Amesema Mwanachuoni Shaykh Muhammad bin Swaalih bin Al-‘Uthaymiyn (Allaah Amrehemu) kuhusu Hadiyth hii,
“Mwenye kuburuza nguo yake kwa kiburi, Allaah Hatomtazama siku ya Qiyaamah” na Hadiyth hii, “Chenye kuwa chini ya mafundo ya miguu katika mavazi, basi ni motoni”:
Kwa kuwa kumekhitilafiana adhabu hizo mbili, basi kunakatazika kuifanya
hukumu hiyo (ya Isbaal) kuwa ‘Mutwlaq’ (iliyo wazi ya moja kwa moja) ni
yenye kuwa juu ya ‘Muqayyad’ (iliyofungamanishwa na kitu), kwani kanuni
ya kubeba ‘Mutwlaq’ juu ya ‘Muqayyad’ ni sharti kukubaliana ‘Nasw’
(maandiko) mbili katika hukumu. Ama ikitofautiana hukumu (kama ilivyo
kwenye hizo Hadiyth mbili juu) basi haibebeshwi mojawapo juu ya
mwenzake. Na hivyo ndivyo hata Aayah ya kutayamamu ambayo Amesema Allah:
“Na mpanguse nyuso zenu na mikono yenu kwayo” haikufunganishwa na Aayah ya Wudhuu ambayo Allaah Amesema:
“Na muoshe nyuso zenu na mikono yenu hadi kwenye viwiko” maana haiwi Tayammum hadi kwenye viwiko.
6-
Naye Mwanachuoni Shaykh Al-Albaaniy (Allaah Amrehemu) katika baadhi ya
vikao vyake kwamba haijuzu Muislam kukusudia kurefusha vazi lake miguuni
kwa madai kuwa hafanyi hivyo kwa kiburi, na anaunganisha hayo kwa
maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)
aliyomwambia Abu Bakr, “Wewe si mwenye kufanya kwa kiburi”, kwa sababu
Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) hakuwa akivaa nguo ndefu, na Mtume
akamwambia, “Wewe si mwenye kufanya kwa kiburi”, ila hayo majibu ya
Mtume kwa Abu Bakr yalikuwa ni kwa sababu Abu Bakr vazi lake lilikuwa
lamshuka lenyewe, na akawa akionekana ni kama mwenye kurefusha nguo. Na
Mtume akamjibu kumwambia kuwa hilo ni jambo ambalo huchukuliwi kwalo,
kwani hujakusudia na wala hukulifanya kwa kiburi. Hivyo, ni makosa
kabisa watu kuuunganisha tukio la Abu Bakr na kuburuza kwao nguo kwa
makusudi kisha wakadai kuwa: ‘Sisi hatufanyi kwa kiburi’! Tukio la Abu
Bakr haliwezi katu kuwa hoja ya wanayoyafanya.
7- Amesema Mwanachuoni Faqiyh Shaykh Muhammad bin Swaalih bin Al-‘Uthaymiyn (Allaah Amrehemu):
“Hakika
Abu Bakr katakaswa na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa
sallam) na akatoa Mtume ushahidi kuwa Abu Bakr si katika wale wanaofanya
hivyo (kuvaa nguo ikaburuza) kwa fakhari. Sasa je, hao wanaovaa nguo
zikavuka mafundo (zikaburuza) wamepata utakaso au ushuhuda kama huo wa
Abu Bakr?!
Lakini
Shaytwaan anawafungulia baadhi ya watu milango ya kufuata yale maandiko
yenye utata kwenye Qur-aan na Sunnah ili yaendane na matashi yao na
yale wayafanyayo, na Allaah Ndiye Humuongoza Amtakaye katika njia
nyoofu, tunamuomba Allaah Atupe sisi na wao hidaaya”
Na
tunakhitimisha jibu la hoja hiyo ya watetezi wa Isbaal kwa Fatwa ya
Mwanachuoni mkubwa wa miaka ya karibuni, aliyekuwa Mufti wa Saudi
Arabia, Shaykh ‘Abdul-‘Aziyz bin ‘Abdillaah bin Baaz (Allaah Amrehemu)
kuhusiana na maudhui hii, alipojibu swali lifuatalo:
Swali:
Katika
Hadiyth ambayo maana yake inakusudia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi
wa aalihi wa sallam) kasema kuwa mwenye kuburuza vazi lake basi ni
motoni, na sisi mavazi yetu yanazidi chini ya mafundo ya miguu na
hatukusudii kuvaa kwa kiburi au kwa fakhari bali ni ada ambayo
tumeizoea, je, kuvaa kwetu namna hiyo ni Haraam? Na je, vipi yule mwenye
kuburuza vazi lake na hali yeye ni mwenye kumuamini Allaah. Naomba
faida?
Jibu:
Imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa kasema:
“Chenye kuvuka chini ya mafundo ya miguu katika vazi hupelekea motoni” Ameisimulia Imaam al-Bukhaariy katika Swahiyh yake.
Na akasema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
“Watu
watatu Hatowasemesha Allaah siku ya Qiyaamah, na Hatowatazama, na
Hatowatakasa, na watapata adhabu iumizayo; (Hao ni) al-Musbil – Mwenye
kuburuza nguo yake, Mwenye kutoa na kukizungumzia alichokitoa, Na mwenye
kuuza bidhaa zake kwa kutumia kiapo cha uongo” Imesimuliwa na Imaam Muslim katika Swahiyh yake.
Na
Hadiyth zenye maana hizi ni nyingi nazo zinakataza (zinaharamisha)
Isbaal (kuburuza nguo) moja kwa moja japo mwenye kuburuza atadai kuwa
yeye hajavaa kwa kiburi au kwa fakhari, kwani japo mvaaji atakataa hilo,
lakini ajue kufanya hivyo ndiko kunakopelekea kwenye kiburi. Na pia
katika hilo kuna israaf na kuzipelekea nguo kupata uchafu na kukomba
najisi. Na ikiwa aliyevaa makusudio yake ni kiburi, basi hatari inakuwa
kubwa na madhambi yanazidi kama anavyosema (Swalla Allaahu ‘alayhi wa
aalihi wa sallam):
“Atakayeburuza nguo yake kwa kiburi Allaah Hatomtazama siku ya Qiyaamah”.
Na mipaka ya nguo ni kufika kwenye mafundo mawili ya miguu. Haijuzu
kwa Muislam mwanamme kuachia nguo yake kuvuka chini ya mafundo ya miguu
kama zilivyotaja Hadiyth zilizotangulia. Ama mwanamke yanatakiwa mavazi
yake kishari’ah yafunike miguu yake. Kuhusiana na Asw-Swiddiyq (Radhiya
Allaahu ‘anhu) yeye alimwambia Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi
wa sallam) kuwa vazi lake linamteremka na yeye si mwenye kutaka hivyo,
na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema, “Wewe si mwenye kufanya kwa kiburi” Na
makusudio yake ni kuwa mwenye kushuka nguo yake bila makusudio na huku
akijitahidi kuizuia isishuke kama alivyokuwa Abu Bakr (Radhiya Allaahu
‘anhu) basi anakuwa haingii katika yale maonyo na makemeo yaliyokuja
kwenye Hadiyth kwa sababu hakuacha nguo ishuke kwa makusudi. Na pia
hakukusudia kiburi na hali hiyo ni kinyume na ile hali ya yule ambaye
anaachia nguo yake iburuze kwa makusudi bila kuonyesha juhudi zozote za
kuipandisha au kuizuia isiburuze, na kwa hivyo, mtu wa aina hii ataingia
katika kundi la wanaofanya kwa kiburi na Allaah Anajua yaliyomo kwenye
nyoyo za watu (japo watu watakuwa wanatoa visingizio mbalimbali).
Na
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) vilevile ametoa
maelezo (Hadiyth) mbalimbali kuonya kuhusu Isbaal na akasisitizia sana,
na hivyo ni waajib kwa Muislam kujihadhari na yale Aliyoyaharamisha
Allaah, na ajiepushe na vile vyenye kusababisha ghadhabu ya Allaah, na
akome katika mipaka ya Allaah na ataraji thawaab na akhofu adhabu Zake
kwa kuyafanyia kazi maneno ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
“Na anachokupeni Mtume chukueni, na anachokukatazeni jiepusheni nacho. Na mcheni Allaah. Hakika Allaah ni Mkali wa kuadhibu” [Al-Hashr: 7]
Na kauli Yake Aliyetukuka: “Na
anayemuasi Allaah na Mtume Wake, na akaipindukia mipaka Yake, (Allaah)
Atamtia Motoni adumu humo, na atapata adhabu ya kudhalilisha.” [An-Nisaa: 14]
Allaah Awawafikishe
Waislam katika yale yenye Radhi Zake na yenye manufaa kwenye mambo ya
Dini yao na dunia yao, Naye ni Mbora wa Usimamizi. [Mwisho wa kumnukuu
Shaykh Ibn Baaz].
Wasiya Wa ‘Umar Bin Al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ‘Anhu) Baada Ya Kuchomwa Upanga Kabla Hajafariki:
Amesimulia Imaam
al-Bukhaariy katika Swahiyh yake kutoka kwa ‘Amru bin Maymuun –
kuhusiana na kisa cha kuuliwa Khaliyfah Mwongofu ‘Umar bin Al-Khattwaab
(Radhiya Allaahu ‘anhu) – amesema: “Mimi nikiwa nimesimama baina yangu
na yake (yaani ‘Umar [Radhiya Allaahu ‘anhu]) ila ‘Abdullaah bin ‘Abbaas
(akiwa katikati) asubuhi aliyoshambuliwa, na alikuwa akipita baina ya
Swaff mbili akisema: Nyookeni, hadi akawa haoni penyo, akatangulia
(kuswalisha) akapiga Takbiyrah na nikamsikia akisema: Ameniua - wakati
alipodungwa – kisha akataja kisa cha kubebwa na kupelekwa nyumbani kwake
kisha akasema: Wakaja watu huku wanamuombea. Akaja kijana mmoja
akamwambia: Kuwa na bishara njema Ee Amiyrul Muuminiyn kwa bishara ya
Allaah kwako kuwa utasuhubiana na Mtume Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa
aalihi wa sallam); umetangulia katika Uislam kadiri nielewavyo, ukapewa
uongozi na ukafanya uadilifu, kisha mwisho umepata Shahaadah (umekufa
shahidi). Akasema (‘Umar): Napendelea yangekuwa hayo yananitosha si
kwangu tu au dhidi yangu. Na wakati kijana huyo alipogeuka kuondoka,
huku vazi (kikoi) lake kinavuka mafundo kwa urefu na kuburuza chini,
(‘Umar [Radhiya Allaahu ‘anhu]) akasema mrudisheni huyo kijana, na
(aliporudishwa) akamwambia: Ee mwana wa ndugu yangu, nyanyua (pandisha)
kikoi chako; kufanya hivyo kunaidumisha nguo yako, na kunakupa uchaji
Allaah.
Ndugu Muislam,
tuzingatie wasiya huu wa ajabu na wakati ambao umetolewa! Wakati damu
yake Amiyrul Muuminiyn ikiwa inavuja kwa wingi baada ya kuchomwa upanga
na Abu Luuluu al-Majuusiy Mfursi adui wa Allaah, na akiwa anayakabili
mauti, lakini pamoja na yote hayo hakuweza kuvumilia pindi alipoona vazi
la kijana yule likiburuza na akampatia wasiya huo ilihali yeye taabaan
na yuko kwenye kuhudhuria mauti! Tukio hili linatujulisha kuwa kitendo
cha Isbaal (kuburuza vazi) ni tendo zito na ovu ambalo halipasi
kunyamaziwa.
Isbaal – Vazi La Mwanamme Lenye Kuvuka Mafundo Ya Miguu (Uburuzaji Au Kuburura) - 1
Meat Tarts With White Sauce
-
Ingredients:
Dough:
1½ cups flour
½ tsp salt
½ cup chilled butter pieces
4-5 Tbsp cold water
The filling:
Cooked minced meat (or chicken pieces), ...
Post a Comment