NASAHA KWANGU NA KWAKO!! SIMU ZETU ...


Moja ya jambo gumu kabisa ktk karne ya 21 ni Vijana kutumia dakika 30 bila "kushika" simu zao!
Karibia kila mmoja sasa ni mlevi wa simu.
Simu ni kitu cha mwisho unachokishika kabla hujalala usiku.
Simu ni kitu cha kwanza unachokishika pindi unapoamka asubuhi.
Wengine hata huweka visikilizio kwenye masikio yao usiku kucha.
Wengine bado huamka usiku na kudownload filamu lakini hawawezi kuamka kwa ajili ya tahajud.
Wengine muda wote wapo "online" wanachat.
Asubuhi mapema ya saa 12 wapo hewani na wanabaki hewani mpaka usiku wa manane.
Wana maelfu ya marafiki hewani ambao wanachat nao lakini hawasuhubiani na familia zao nyumbani.

Wamejitenga wenyewe peke yao ndani ya vyumba vyao.
Wengine hubishana usiku wa manane kuhusu mas'ala ya aqidah, na bado unapofika muda wa Alfajr amelala na anakoroma.
Mara tu baada ya salamu katika Swala utawaona watu wakibonyeza simu zao tena, hawana muda wa kumtaja Allaah!
Utadhani wameshasamehewa madhambi yao yaliyopita na ya mbeleni!
Pindi ajali zinapotokea, badala ya kuokoa maisha ya watu, utawaona watu wakiwapiga picha majeruhi kwa kutumia simu zao.

Pindi nyumba inapoungua moto, badala ya kuuzima moto huo, utawaona watu wakipiga picha ili wawe wa kwanza kuweka kwenye mitandao ya kijamii.
Pindi mtu anapompoteza kipenzi chake, badala ya kufikiria mas'ala ya maziko, kitu cha kwanza ni kusambaza taarifa za kufiwa kwenye mitandao ya kijamii, ili huenda apate maoni/ kufarijiwa!
Tumekuwa walevi mno na simu, mpaka tunafikia kuchat tukiwa kwenye pikipiki.
Wengine bado wanachat ndani ya vyumba vya mitihani / wakiwa wanafanya mitihani.
Wengine hucheza game kwenye simu zao Msikitini. 

# Subhanallah
Wengine huangalia filamu Msikitini.
Ni fitnah kiasi gani imeukumba Ummah.

Barabarani wengine huenda wakibonyeza simu zao mpaka wanasababisha ajali.
Hata pindi tunapokuwa na wageni bado tumeshughulishwa na simu zetu kuliko mgeni wetu.
Wengine huwapuuza Wenza wao kwa sababu wanachat na marafiki zao kwenye Facebook!
Wengine hutumia Suratul Asr kuharakisha Sala kwa sababu ya simu zao, hawajuwi kuwa Suratul Asr inazungumzia matumizi ya muda kwa ajili ya amaal njema.
Wengi simu zao zimewafanya kuwa wambeya/ wasengenyaji. Simu zinawapeleka wengi motoni. Kwa sababu ya simu yako, wewe ni mtu wa mwisho kufika kwenye Swala ya Juma'ah na mara zote wewe ni wa kwanza kutoka!

Allah anasema, "Imewakaribia watu hesabu yao (Qiyamah) nao wamo katika mghafala; wanakengeuka tu, wanapuuza." (Sura Al-Anbiyaa aya ya 1)
Sheikh Uthaymeen rahimahuLlah amesema, Yeyote asiyetumia muda wake kwa ajili ya Allaah, kilicho bora kwake ni KIFO!
Tunamuomba Allaah atusamehe madhambi yetu mbalimbali, Aaamiyn.
Tafadhali waelimishe wengine.
Jazaakumullaahu khayra!

TAFADHALI... USISOME TU BALI TAFAKARI KUHUSU HILI

0 Comments