Imeandaliwa na : Khalid Kutoka Mkoani Arusha : Masjid Taqwa
As salaam aleikum
warahamatullah wabarakatuh ndugu zetu katika iymaan
Yanapotokea makubwa
katika jamii ya kiislamu sisi kama waislamu ni jukumu letu kupeana
nasaha na kurudishana katika mwenendo wa uislamu, katika siku za hizi
karibuni waislamu tumeanza kushuhudia baadhi ya makundi mbalimbali
yanayojihusisha na mihadhara yenye anuani zenye maudhui za kiislamu.
Lakini tunapofika
katika mihadhara hiyo tunashuhudia mambo ambayo ni kinyume na anuani
husika iliyotangazwa pia ni kinyume na matarajio ya waislamu
waliohudhuria katika muhadhara huo, na ni kinyume na taratibu za
mihadhara ya kiislamu, pia ni kinyume na mafundisho ya Uislamu.
Mfano wa mambo
yanayofanyika katika mihadhara hiyo ni shirki, Allaah anasema katika
Qur’an tukufu ( 9:17. Hawawi washirikina ndio
wenye kufaa kuamirisha misikiti ya Mwenyezi Mungu, na hali wao
wangali kuendelea na ukafiri wao, na wanautangaza khasa! Vitendo vyao
washirikina havitiwi hisabuni, wala hawatolipwa thawabu kwavyo! Wao
ni wenye kudumu Motoni Siku ya Kiyama. )
sheikh anaye hutubia huanza kufanya miujiza ya mizimu (yaani humloga
mtuu kisha humtibu papo kwa papo) kisha husema ndio mafundisho ya uislamu
Jambo ambalo si sahihi kwa mujibu wa mafundisho ya Dini yetu tukufu
ya Uislamu,
Haifai kwa muislamu
na viongozi wetu wanaotangaza dini yetu tukufu ya kiislamu , kutumia
mihadhara kupotosha Ummah na badala ya kutangaza dini na Tawhiyd
badala yake wamekuwa wakitangaza Tiba za madawa na miujiza ya
kishirina na kisha kuitibu papo kwa papo, kwa njia ambazo si sahihi kwani wanakuwa wametoka katika
lengo na mafndisho ya Uislamu katika mihadhara yao hiyo.
hali hii imeleta athari
kubwa katika ummah kwa ujumla tumekuwa tukipokea jumbe mbalimbali
kutoka kwa watu ambao ni waislamu na wasio waislamu wakitaka
tuwapatie huduma ya tiba kama za masheikh hawa ambazo ni kinyume na
mafundisho ya uislamu , jumbe hizo ni kama kumtumia mtu majini N.K
Ambapo utaratibu
kama huo ni Haram na ni katika madhambi makubwa, Muislamu kutumia
majini , mizimu na kutegemea chochote asiyekuwa Allaah. Lengo la
nasaha hizi si kila muhadhara haufai lakini mihadhara ya namna hii
haifai Kuhudhuria kwa mafundisho yake si katika njia ya uislamu,
Mihadhara ya namna hii inaleta fitna na mkanganyika katika jamii ya
kiislamu
Hivyo
utakapohudhuria muhadhara na ukakuta viashiria vya shirki ni bora
ukaondoka kwani hapo kuna hasira za Allaah katika mihadhara kama hiyo.
na Allaah ndiye Mjuzi
Post a Comment