عَنْ
أَبي ذَرٍّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ
عَلَيهِ وَسَلَّمَ:((مَنْ صَامَ مِنْ كُلِّ شَهْرٍ ثَلاثَةَ أَيَّامٍ
فَذَلِكَ صِيَامُ الدَّهْرِ)) فَأَنْزَلَ اللهُ تُصْدِيقَ ذَلِكَ في
كِتَابِهِ الْكَرِيمِ: ((مَنْ جَاءَ بِالْحَسَنَةِ فَلَهُ عَشْرُ أَمْثَالِهَا))، الْيَوْمُ بِعَشَرَةِ أَيّامٍ. أخرجه أحمد والترمذي وقال حديث حسن ، والنسائي وابن ماجه وابن خزيمة
Imepokelewa
kutoka kwa Abuu Dharr (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah
(Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Yeyote
atakayefunga swawm kila mwezi siku tatu, ni sawa na swawm ya milele))
Kisha Allaah Akateremsha Aayah ithibitishayo hayo: “Atakayekuja kwa 'amali nzuri basi atapata (thawabu) kumi mfano wa hiyo.” Siku moja kwa malipo ya siku kumi.
[Imepokewa na At-Tirmidhiy na amesema Hadiyth Hasan, An Nasaaiy na Ibn
Maajah, Ibn Khuzaymah na ameisahihisha Shaykh Al-Albaaniy katika Al-Irwaa (4/102)]. Aayah: Suwrat Al-An’aam (160)]
Maana Ya Biydhw: Masiku hayo yameitwa ‘Biydhw’ (meupe) sababu usiku wa siku hizo hung'aa kutokana na mwanga wa mwezi. Ayyaam Al-Biydhw (Masiku Meupe) tarehe zake ni 13, 14 na 15 katika kila mwezi wa kalenda ya Kiislamu.
عَنْ
جريرٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ عَن النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيهِ وَسَلَّمَ
قَالَ: ((صِيَامُ ثَلاثَةِ أَيَّامٍ مِنْ كُلِّ شَهْرٍ صِيَامُ الدَّهْرِ،
أَيَّامُ الْبِيضِ صَبِيحَةَ ثَلاثَ عَشَرَةَ وَأَرْبَعَ عَشَرَةَ
وَخَمْسَ عشَرَةَ))
Imepokelewa
kutoka kwa Jariyr (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu
‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Swiyaam siku tatu kila mwezi ni
sawa na swiyaam ya milele; na masiku meupe ni tarehe kumi na tatu, kumi
na nne na kumi na tano [13, 14, 15])) [An-Nasaaiy (2420) na ameisahihisha Al-Abaaniy katika Swahiyh At-Targhiyb (1040)]
عن أبي ذر رضي الله عنه: قال لي رسول الله صلى الله عليه وسلم : ((يَا أَبَا ذَرٍّ، إِذَا صُمْتَ مِنَ الشَّهْرِ ثَلاثَةَ أَيَّامٍ فَصُمْ ثَلاثَةَ عَشَرَ وَأَرْبَعَةَ عَشَرَ وَخَمْسَةَ))
Imepokelewa
kutoka kwa Abuu Dharr (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Rasuli
wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliniambia: ((Ee
Abuu Dharr! Endapo utafunga swawm siku tatu za kila mwezi, basi funga
swawm siku ya 13, ya 14, na ya 15)) [Imepokewa na At-Tirmidhiy na kasema Shaykh Al-Albaaniy kuwa ni Swahiyh]
قال صلى الله عليه وسلم: ((أَلا أُخْبِرُكُمْ بِمَا يُذْهِبُ وَحَرَ الصَّدْرِ صَوْمُ ثَلاثَةِ أَيَّامٍ مِنْ كُلِّ شَهْر))
Rasuli
wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Je,
nikujulisheni jambo litakaloondosha uovu wa moyo? Ni kufunga swawm siku
tatu kila mwezi)) [An-Nasaaiy (2/2386) na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh An-Nasaaiy (2249)]
Asw-Swuyuutwiy (Rahimahu Allaah) amesema katika An-Nihaayah: “Uovu wa moyo ni; udanganyifu, wasiwasi, na imesewma pia ni uhasidi, chuki, na imesemwa pia uadui na imesemwa ghadhabu”
عن أبي هريرة رضي الله عنه: تُعرَضُ الأعمالُ يومَ الاثنينِ والخميسِ فأحبُّ أن يُعرَضَ عملي وأنا صائمٌ
Imepokelewa
kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla
Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Amali zinapandishwa siku
ya Jumatatu na Alkhamiys, basi napenda kwamba zipandishwe amali zangu
nikiwa mimi nina Swawm.” [Swahiyh At-Tirmidhiy 747, Swahiyh At-Targhiyb 1041]Na kuhusu Swiyaam ya Jumatatu:
عَنْ
أَبِي قَتَادَةَ الْأَنْصَارِيِّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ
اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ سُئِلَ عَنْ صَوْمِ
الِاثْنَيْنِ فَقَالَ: ((فِيهِ وُلِدْتُ وَفِيهِ أُنْزِلَ عَلَيَّ)).
Kutoka
kwa Abuu Qataadah Al-Answaariyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli
wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliulizwa kuhusu
Swawm ya Jumatatu akasema: “Nimezaliwa siku hiyo na siku hiyo nimeteremshiwa (Qur-aan).” [Muslim]
Baadhi ya fadhila nyinginezo za Swawm:
1. Kuepushwa na moto masafa ya miaka sabiini.
عَنْ
أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ رضي الله عنه قَالَ : قَالَ رَسُولُ اللَّهِ
صلى الله عليه وسلم: مَنْ صَامَ يَوْماً فِي سَبِيلِ اللَّهِ بَعَّدَ
اللَّهُ وَجْهَهُ عَنْ النَّارِ سَبْعِينَ خَرِيفًا .
Imepokelewa
kutoka kwa Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema:
“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Atakayefunga Swawm siku moja kwa ajili ya Allaah, Allaah Atamweka
mbali uso wake na moto masafa ya miaka sabiini)) [Muslim 2/208]Na katika Hadiyth nyengine pia:
عن جابر رضِي الله عنه عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم قال: ((الصِّيام جُنَّة يَستَجِنُّ بها العبدُ من النار))
Imepokelewa
kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kutoka kwa Nabiy (Swalla
Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Swiyaam ni kinga
itamukoa mja kutokana na moto [wa Siku ya Qiyaamah])) [Ahmad 2/402, Swahiyh At-Targhiyb 1/411 na Swahiyh Al-Jaami’ 3880] 2. Mwenye kufunga Swawm atafunguliwa mlango wa Rayyaan huko Jannah.
عَنْ
سَهْلٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ
وَسَلَّمَ قَالَ: ((إِنَّ فِي الْجَنَّةِ بَابًا يُقَالُ لَهُ الرَّيَّانُ
يَدْخُلُ مِنْهُ الصَّائِمُونَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ لَا يَدْخُلُ مِنْهُ
أَحَدٌ غَيْرُهُمْ يُقَالُ أَيْنَ الصَّائِمُونَ فَيَقُومُونَ لَا يَدْخُلُ
مِنْهُ أَحَدٌ غَيْرُهُمْ فَإِذَا دَخَلُوا أُغْلِقَ فَلَمْ يَدْخُلْ
مِنْهُ أَحَدٌ ))
Imepokelewa
kutoka kwa Sahl (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kutoka kwa Nabiy (Swalla
Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika katika Jannah
kuna mlango unaitwa Rayyaan, wataingia humo siku ya Qiyaamah wenye
kufunga Swawm, hatoingia yeyote mwingine. Itasemwa: “Wako wapi waliokuwa
wakifunga Swawm? Watasimama kuingia hatoingia yeyote mwingine,
watakapoingia, utafungwa, basi hatoingia mwengine)) [Al-Bukhaariy 1763, Muslim 1947]3. Swawm ni kwa ajili ya Allaah Pekee na mwenye Swawm hupata furaha mbili; anapofuturu na atakapokutana na Rabb Wake. Na harufu ya mdomo wake ni nzuri mbele ya Allaah kuliko harufu ya misk.
عنْ
أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ
صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((كُلُّ عَمَلِ ابْنِ آدَمَ يُضَاعَفُ
الْحَسَنَةُ عَشْرُ أَمْثَالِهَا إِلَى سَبْعمِائَة ضِعْفٍ قَالَ اللَّهُ
عَزَّ وَجَلَّ إِلَّا الصَّوْمَ فَإِنَّهُ لِي وَأَنَا أَجْزِي بِهِ يَدَعُ
شَهْوَتَهُ وَطَعَامَهُ مِنْ أَجْلِي لِلصَّائِمِ فَرْحَتَانِ فَرْحَةٌ
عِنْدَ فِطْرِهِ وَفَرْحَةٌ عِنْدَ لِقَاءِ رَبِّهِ وَلَخُلُوفُ فِيهِ
أَطْيَبُ عِنْدَ اللَّهِ مِنْ رِيحِ الْمِسْكِ))
Imepokewa
kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu): ((Kila 'amali njema
ya mwana Aadam inalipwa mara kumi na inaongezewa thawabu kutoka kumi
hadi mia saba, na Allaah (‘Azza wa Jalla) Anasema: Isipokuwa Swawm,
kwani hiyo ni kwa ajili Yangu na Mimi Ndiye Nitakayemlipa; ameacha
matamanio yake na chakula chake kwa ajili Yangu. Kwa aliye na Swawm
atapata furaha mbili; furaha anapofuturu na furaha atakapoonana na Rabb
wake, harufu inayotoka kinywani mwa aliye na swawm ni nzuri mbele ya
Allaah kuliko harufu ya misk)) [Muslim na Ahmad]
4. Du’aa ya mwenye Swawm inakubaliwa.
عَنْ
أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى
اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((ثَلاَثَةٌ لاَ تُرَدُّ دَعْوَتُهُمْ,
الإِمَامُ الْعَادِلُ, وَالصَّائِمُ حَتَّى يُفْطِرَ, وَدَعْوَةُ
الْمَظْلُومِ ...))
Kutoka
kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Rasuli wa Allaah
(Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: (([Watu] Watatu
hazirudishwi du'aa zao; Imaam muadilifu, mwenye Swawm mpaka afuturu, na
du'aa ya aliyedhulumiwa…)) [Ahmad na ibn Maajah. Pia Al-Bayhaqiy 3/345 na As-Silsilah Asw-Swahiyhah 1797]
5. Swawm itakuombea shafaa-‘ah Siku ya Qiyaamah.
عَنْ
عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو رضي الله عنهما أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى
اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((الصِّيَامُ وَالْقُرْآنُ يَشْفَعَانِ
لِلْعَبْدِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ، يَقُولُ الصِّيَامُ: أَيْ رَبِّ مَنَعْتُهُ الطَّعَامَ وَالشَّهَوَاتِ بِالنَّهَارِ فَشَفِّعْنِي فِيهِ. وَيَقُولُ الْقُرْآنُ: مَنَعْتُهُ النَّوْمَ بِاللَّيْلِ فَشَفِّعْنِي فِيهِ. قَالَ : فَيُشَفَّعَانِ))
Imepokelewa
kutoka kwa 'Abdullaah bin ‘Amr (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) kwamba
Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Swiyaam na Qur-aan zitamuombea shafaa’ah mja siku ya Qiyaamah. Swiyaam
itasema: “Ee ee Rabb! Nimemzuia chakula chake na matamanio wakati wa
mchana, basi nnamuombea shafaa-‘ah.” Na Qur-aan itasema: “Nimemzuia
usingizi wake wakati wa usiku basi nnamuombea shafaa-‘ah.” Akasema:
((Basi [viwili hivyo] vinaombea shafaa-‘ah na kukubaliwa]. [Ahmad (174/2) Al-Haakim (1/554), Al-Bayhaqiy (3/181) na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh Al-Jaamiy’ 7329]
6. Swawm hakuna mfano wake.
عَنْ
أَبِي أُمَامَةَ قَالَ: أَتَيْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ
عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقُلْتُ: مُرْنِي بِأَمْرٍ آخُذُهُ عَنْكَ قَالَ:
((عَلَيْكَ بِالصَّوْمِ فَإِنَّهُ لَا مِثْلَ لَهُ))
Kutoka
kwa Abuu Umaamah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Nilimwendea Rasuli
wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) nikasema:
“Niamrishe jambo [litakalonifaa Aakhirah] nilichukue kwako.” Akasema:
((Shikilia Swawm kwani hakika hakuna mfano wake)) [An-Nasaaiy]
7. Ukifariki ukiwa na swawm utaingia Jannah nayo ni Husnul-khaatimah.
عن حذيفة رضي الله عنه أن النبي صلى الله عليه وسلم قَال: ((مَن خُتِمَ له بصيام يومٍ دخل الجنة))
Imepokelewa
kutoka kwa Hudhayfah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kutoka kwa Nabiy (Swalla
Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakayekuwa 'amali yake
ya mwisho kabla ya kufariki ni Swiyaam ataingia Jannah)) [Ahmad 5/391. Swahiyh At-Targhiyb 1/412, Swahiyh Al-Jaami’ 6224]
Post a Comment