HIJAAB YA KISHAR'IAH INAHUSU KUFUNIKA USO NA MIGUU?

SWALI:
Naomba nifahamishwe hijabu ipasavyokuwa, je uchi wa wa mwanamke does it include miguu?since summer is nearing most of us are shoping for open shoes, is it allowed, I know other madh-habs say we should infact cover our whole faces but I don’t think the qur'an specifies that in particular?.

JIBU:
Sifa zote njema anastahiki Allah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Kuhusu kufunika Miguu:
Naam miguu ya mwanamke inalazimu kufunikwa. Imepokewa kutoka kwa Ummu Salamah amesema: nilimuuliza Mtume (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wakati lilipozungumzwa suala la kipimo cha nguo ya chini ya mwanamume (ambayo inatakiwa isivuke mafundo ya miguu), ewe Mjumbe wa Allaah na ipi hukumu ya kipimo cha nguo ya mwanamke? Akasema: "Ataiteremsha (kiasi cha) shubiri) akasema Ummu Salamah kwa maana hiyo si itaonekana (miguu yake)? Akasema: (Na aiteremshe) kiasi cha dhiraa moja wala asizidishe zaidi ya hapo" (Abuu Dawuud: 4117 na Maalik katika Muwatwa: 2017).

Shaykhul-Islaam Ibn Taymiyah (Rahimahu Allaah) amesema katika Majmuul-Fataawa 22/110: 
“…….inavyoonyesha kuwa rai ya Imaam Ahmad ni dhahiri kabisa kuwa kila kiungo cha mwanamke ni ‘awrah’ (uchi) hata pia kucha zake. Na hii pia ni rai ya Imaam Maalik”
Dalili ni kutoka katika Aayah ifuatayo: 
((وَلَا يَضْرِبْنَ بِأَرْجُلِهِنَّ لِيُعْلَمَ مَا يُخْفِينَ مِن زِينَتِهِنَّ))
((Wala wasipige chini miguu yao ili yajulikane mapambo waliyoyaficha)) [An-Nuur: 23:31]

 Imaam Ahmad amesema“…. Mapambo ambayo yaliyodhihirika ni nguo ….. kila kiungo cha mwanamke ni ‘awrah’ hata kucha zake. Imesimuliwa katika Hadiyth “Mwanamke ni ‘Awrah”. Hii ni umbo lote la mwanamke. Na sio makruuh (haichukizi) kufunika mikono yake wakati wa kuswali, kwa hiyo pia ni sehemu ya ‘awrah kama ilivyo miguu. Hivyo Qiyaas (Analogy) imekusudiwa kwamba uso pia ni ‘awrah’ japokuwa haukutakiwa kufunikwa wakati wa Swalah na sio kama mikono…” [Sharh al-‘Umdah 4/267-268]
Dalili anayoichukulia Imaam Ahmad ni hii:
Imesimuliwa na ‘Abdullaah kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ambaye amesema: ((Mwanamke ni ‘awrah’ na anapotoka nje basi matumaini ya shaytwaan huwa juu)) [At-Tirmidhiy, 1173 na Shaykh Al-Albaaniy kasema Swahiyh katika At-Tirmidhiy 935.]
Kuhusu kufunika uso:
Maulamaa wamekhtilafiana kuhusu mas-ala haya. Maelezo kamili utayapata katika Jibu la Swali kwenye kiungo kifuatacho ambalo limeshaulizwa  Alhidaaya:

Mwanamke wa Kiislamu analazimika kuyafahamu masharti ya hijabu yanavyopasa kuwa, nayo ni haya yafuatayo:
1.      Inatakiwa hijabu ikisitiri kiwiliwili chote cha mwanamke, (pamoja na khilafu iliyopo kati ya wanachuoni kuhusu suala la uwajibu wa kuufunika uso na kutoufunika);
2.      Jilbaab la mwanamke lisiwe na mapambo.
3.      Kitambaa cha jilbaab kinatakiwa kiwe kizito (kisioneshe vazi la ndani);
4.      Jilbaab linatakiwe liwe pana (isibane); 
5.      Jilbab halitakiwi kutiwa manukato;
6.      Jilbaab halitakiwi lifanane na mavazi ya kiume;
7.      Jilbaab halitakiwi lifanane na mavazi ya makafiri;
8.      Jilbaab halitakiwi liwe ni katika mavazi ya fakhari.

Na Allaah Anajua zaidi

0 Comments