Vipimo
Vitu Vya Samaki
Samaki mkubwa wa chango 1
Thomu na Tangawizi iliyosagwa 1 kijiko cha supu
Pilipili mbichi iliyosagawa 1 kijiko cha supu
Bizari ya pilau ya unga ½ kijiko
Ndimu 1 kamua maji
Chumvi
Vitu Vya Rojo
Vitunguu maji 2
Nyanya 2
Tuwi la nazi zito 1 ½ kikombe
Nyanya ya kopo 1 kijiko cha chai
Bizari ya manjano ½ kijiko cha chai
Pilipili mbuzi 1 au mbili
Ndimu 1 kamu maji
Chumvi kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Mroweke samaki kwa viungo hivyo kisha muweke katika tray na mchome (grill) katika jiko (oven), akiwiva upande mmoja mgeuze upande wa pili.
- Saga vitunguu na nyanya kidogo tu kwa kutumia tui kidogo katika mashine (blender). Na ukipenda iwe kali zaidi tia pia pilipili mbuzi moja, kisha mimina katika sufuria utakayopikia.
- Tia tui na bizari zote pamoja na nyanya ya kopo, chumvi, pilipili mbuzi nzima na pika moto mdogo mdogo.
- Rojo likianza kuwa zito tia ndimu.
- Epua na mwagia juu ya samaki. Tayari kuliwa.
0 Comments