VIPIMO
Kabeji 1/2
Karoti 2
Tango 1
NAMNA YA KUTAYARISHA
1. Kata kabeji nyembamba sana
2. Zikune karoti zitoke nyembamba
3. Kata tango vipande vidogo vidogo.
3. Kisha changanya pamoja tia kwenye bakuli
UKWAJU
VIPIMO
Ukwaju 1 paketi moja (gm 100)
Maji 2 vikombe
Kitunguu saumu(thomu/galic) chembe tatu
Tangawizi kipande kidogo tu
Tende 3
Kitunguu maji 1 kidogo
Nyaya 1 ndogo
Pili pili mbichi 3
NAMNA YA KUTAYARISHA
1. Toa kokwa katika ukwaju
2. Rowanisha na maji kisha kamua na utupe kokwa
3. Tia katika sufuria na tia vitu vyote vingine ndani ya sufuria.
4. Chemsha, na ikianza kuchemka ipike kwa muda wa dakika 5.
5. Epua na uache upoe kisha usage katika mashine ya kusagia (blender) – uko tayari kuliwa na kuku na saladi.
Post a Comment