Vipimo
Viazi 1kg
Ndimu 2
Rai 2 vijiko vya chai
Unga wa ngano au wa dengu 2 vikombe vya chai
Bizari ya majano 1 Kijiko cha chai
Chumvi Kiasi
Pilipili ya unga Kiasi upendavyo
Mafuta ya kukaangia
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Osha viazi vizuri na viweke katika sufuria
- Tia maji ndani ya sufuria iliyokuwa na viazi na hakikisha maji niyakutosha kuweza kuivisha viazi
- viweke jikoni vichemke na kuiva baada ya hapo viweke viazi pembeni vipoe kwanza
- Kisha menya maganda na uviponde ponde hadi vilainike
- Tia chumvi kiasi, ndimu, rai na pilipili na vichanganye pamoja vizuri.
- Kata madonge madonge na yazungushe zungushe katika mikono ili yawe duara
- Chukua unga na tia bizari ya majano, chumvi kiasi na maji kiasi
- Changanya mchanganyiko huo hadi uchanganyike vizuri uwe mzito mzito
- Weka kikaango jikoni na subiri mafuta yapate moto
- Kisha chukua donge moja moja na lichovyee lote katika unga ulio tengeneza hakikisha donge hilo limeenea unga huo sehemu yote
- Kisha tumbukiza katika kikaango na fanya hivyo kwa madonge mengine yaliyo bakia
- Baada ya kumaliza yote tia katika sahani na tayari kwa kuliwa
Post a Comment