JINSI YA KUPIKA SAMAKI WA KUOKA WA ROJO VIAZI NA BILINGANI YA KUKAANGA

Vipimo
Samaki Kolekole au changu mkubwa - 1
Bilingani - 1 kubwa
Viazi - 3
Tomato paste - 1 kikopo kidogo
Nyanya freshi - 2 kubwa
Kitunguu maji - 1 kikubwa
Kitunuu saumu (thomu/galic) iliyosagwa - 1 cha supu
Tangawizi - 1 cha chai
Pilipili manga - 1 cha chai   
Pilipili mbichi iliyosagwa - 1 Kijiko cha supu                   
Masala ya samaki - 1 kijiko cha supu
Ndimu - 1
Chumvi -  Kiasi
Mafuta ya masala  -  1/3 kikombe
Mafuta ya kukaangia - kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
  1. Msafishe samaki vizuri na mpasue pasue na kisu sehemu ya mnofu ili viungo viweze kuingia ndani na awive vizuri
  1. Changanya masala ya samaki pamoja na chumvi, thomu, tangawizi, pilipilipi mbichi, ndimu kisha mpake samaki vizuri akolee. Mroweke kwa muda wa saa tu hivi.
  1. Muweke samaki katika grill kwa moto wa wastani. Akiwiva juu, mgeuze upande wa pili.
  1. Samaki akiwa tayari kuiva basi mtoe na muweke kando
  1. Katakata bilingani na viazi vipande vipande vya duara.
  1. Weka kikaango jikoni na tia mafuta na subiri mafuta yapate moto. Kisha kaanga kwanza bilingani, zikiwiva na kugeuka rangi toa chuja mafuta, weka kando. 
  1. Kaanga viazi pia, chuja mafuta weka kando.
  1. Weka sufuria jikoni na tia mafuta na yakipata moto tia kitunguu na kanga hadi kuwa hudhurungi
  1. Kisha tia nyanya freshi kaanga kwa muda na tia tomato paste na chumvi na pilipili manga kidogo
  1.  Chukua chombo kama sahani kubwa ya shepu ya yai (oval shape) Weka kwanza samaki. Kisha mwagie rojo la nyanya. Kisha pambia bilingani na viazi pembeni, akiwa tayari.

0 Comments