Kaghadhibika Sana Mchana Wa Ramadhwaan Akafungua Swawm
´Allaamah Zayd bin Haadiy Al-Madkhaliy
SWALI:
Kuna mtu alighadhibika mchana wa Ramadhwaan ghadhabu kubwa akala, nini juu yake?
JIBU:
Ni juu yake kulipa Swawm na ni juu yake kufanya tawbah. Kwa kuwa ghadhabu haimfanyi mtu akala, lakini jambo kama hili ni nadra kupatikana kwa watu. Kufanya jambo kama hili ni juu yake kutubu kwa Allaah na ni juu yake kulipa siku moja Swawm.
Post a Comment