HUKUMU YA KUFUTURU KABLA YA KUZAMA JUA

Hukumu Ya Kufuturu Kabla Ya Kuzama Jua
Shaykh Yahyaa Al-Hajuwriy


SWALI:
Tulikuwa katika Swawm ya Ramadhwaan, akaadhini muadhini kabla ya kuzama jua kwa makosa sisi tukafuturu, lipi la wajibu kwetu? 
JIBU:
Ni wajibu kwenu kulipa siku hio kutokana na kauli sahihi ya Allaah (´Azza wa Jalla): َ
“Kisha timizeni Swiyaam mpaka usiku.”  [Al-Baqarah: 2:187] 
Na ataefuturu kabla ya kutimia Swawm ni wajibu kwake kurudi siku hio.

0 Comments