JINSI YA KUPIKA DONUTS ZA HAMIRA KWA SUKARI YA KUGANDA (Glazed Sugar)

Vipimo
Unga mweupe - 2 ½ Vikombe vikubwa (mugs)
Siagi - 2 vijiko vya supu
Hamira - 2 vijiko vya chai
Yai - 2
Mtindi - 1 kijiko cha supu
Nazi ya unga - 2 vijiko vya supu
Maji - 1 ¼  takriban                                    
Mafuta ya kukaangia       
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Ikiwa hamira ni ya kuumua haraka (instant yeast) weka vitu vyote pamoja katika bakuli uchanganye vizuri uwe uzito wake kama wa mkate wa ufuta na sio mlaini sana kama wa kaimati.
Funika uumuke mchanganyiko kisha teka vidonge uchome katika mafuta makali kiasi.
Epua zichuje mafuta  kisha mwagia sukari uliyokwishatayarisha iliyokwishapoa.
Shira ya kuganda
Sukari - 2  gilasi
Maji - ½ gilasi
Hiliki - ½ kijiko cha chai
Namna ya kutengeneza Shira 
Weka katika sufuria, weka katika moto mdogo mdogo ichemke huku unakoroga usiachie mkono.
Endelea kukoroga mpaka ifanye povu na inate.
Epua ipowe umimine katika donuts uchanganye changanye mpaka shira igeuke sukari nyeupe ya kuganda (glazed)
Vidokezo:
Unaweza kutia nazi ya chenga
Unaweza kutia shira aina nyenginezo  kama caramel, shira ya kawaida, maziwa mazito (condensed) au shira ya tende.

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

0 Comments