JINSI YA KUPIKA TAMBI ZA KUKAANGA

Vipimo
Tambi                                        pakti moja
Sukari                                       ¾ kikombe cha chai
Mafuta                                       ½ kikombe cha chai
Iliki                                             kiasi
Maji                                           3 Vikombe vya chai
Vanilla / Arki rose                    1-2 Tone
Zabibu                                       Kiasi (Ukipenda)
Namna ya kutayarisha na kupika
Zichambue tambi ziwe moja moja.
Mimina mafuta kwenye sufuria yakisha pata moto mimina tambi,zigeuzegeuze mpaka zibadilike rangi na kuwa brown.
Punguza mafuta kwa kuyachuja na zirudishe jikoni.
Nyunyizia iliki zilizosagwa koroga kidogo na mimina maji na tia arki na acha zichemke mpaka maji yakikaribia kukauka mimina sukari koroga kidogo na punguza moto.
Kisha tia zabibu ukipenda, zifunike ili  zikaukie vizuri.
Zikishakauka pakua kwenye sahani tayari kwa kuliwa
Kidokezi:
Itategemea na aina za Tambi unazopika kwa kukisia maji, kama utaona hazijaiva unaweza   kuongeza maji kidogo. 

0 Comments