KUFUTURU TENDE KWA IDADI YA WITR


Imaam Ibn ‘Uthyamiyn (Rahimahu-Allaah)


SWALI:
Nimesikia kwammba mwenye swawm anawajibika pale anapofuturu tende, iwe ni idadi ya witr yaani iwe tano au saba  na kadhaalika Je ni waajib?
JIBU:
Si waajib bali si Sunnah mtu afuturu kwa witr; tatu au tano au saba au tisa, isipokuwa Siku ya ‘Iyd pia kwani imethibiti kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa hatoki kwenda Swalaah Siku ya ‘Iydul-Fitwr mpaka ale kwanza tamar (tende) na alikuwa akila kwa witr. 
Ama nje ya hayo Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hakukusudia kula tamar kwa witr.
 [Fataawa Nuwr ‘Alad-Darb 11/2]

0 Comments